“MUDA huongea sana…..Muda hutenganisha ukweli na Uongo” ~~~~ Dina Marios

MUDA huongea sana.....
muda huponya..
muda hutibu majeraha...
Muda hutenganisha ukweli na Uongo....
Muda Hutoa majibu
Muda hukomaza n.k

Katika jambo lolote lile lipe muda 
Hata ukishika mimba si unaipa muda ili ikue na mtoto azaliwe?
Hata ukipanda mbegu shambani si unazipa muda zichipue na baadae mazao yakue na kuja kuvunwa.
Hakuna jambo linakwenda kwenda tu yoote yanakwenda na muda. Basi hata maswali ujiulizayo ambayo hujapata majibu,yape muda ipo siku utapata majibu.

Kuna mambo huko nyuma nilikuwa sina ujuzi nayo....sina taarifa nayo lakini baada ya MUDA nikayajua na kujifunza.

Hivi unajua uliwahi kuwa mtoto mchanga?unaelishwa na kunyonya?unavalishwa nepi ya vipande vya khanga lakini MUDA ulipita sasa upo hivyo ulivyo.
Katika kila jambo lipe muda.....good morning

Leave a Reply