Muhtasari -sehemu ya mwisho: Jambo lililo umiza moyo wangu!

Maisha yamejaa changamoto ambazo hazikwepeki, na mbaya zaidi zinakuja bila taharifa. Mwezi wa kumi.mwaka huu dada yangu mkubwa (pichani juu) alipatwa na ajali ya kuungua moto.

Akiwa hospitalini

Nisingependa kuelezea undani wa ajali hii kwani huo ni ushuhuda wake yeye, mimi namshukuru Mungu kwa miujiza ya uponyaji wa haraka ambao kwa imani yetu haba hatukuweza kuona ukija. Hali ilikuwa mbaya sana sema ni vile tu siwezi kuweka picha zake humu kwani kama nilivyosema ni ushuda wake yeye. Alilazwa hospitali ya Tabora (Tabora ndipo makazi yao yalipo kwa sasa) kwa muda kisha akahamishiwa Muhimbili ambapo alilazwa takribani zaidi ya mwezi mmoja.

Baada ya kutoka hospitali wanandugu walikusanyika nyumbani kwao huko Yombo Vituka kwaajili ya kumshukuru Mungu kwa maajabu ya uponyaji wake aliyompatia dada yetu.

Mungu ni mwema sana na siku zote anajibu maombi yetu zaidi ya imani yetu. Tutalisifu na kulitukuza jina lake milele na milele.

Leave a Reply