Nawe pia unalalaga na make-up usoni?

Screenshot_2015-11-17-14-33-13-1Madam Rita juzi kati aliweka hii picha na kuweka maneno haya “good night”! Licha ya kupenda picha na mazingira ya kitanda chake lakini nikajikuta najiuliza hili swali, “inamaana madam Rita analala akiwa amepaka make-up usoni, au ni mapozi ya picha tuu?”

Hii ilinikumbusha mmoja ya wadada ambao nilisoma nao secondary. Yeye alituambia kuwa hawezi lala bila kupaka wanja na kuakikisha anaonekana mrembo kwani anaogopa kama ikatokea amelala usingizi wa mauti basi alale akiwa amependeza! ?? je nawewe ni mmoja ya watu wanao lala na poda usoni? Basi ngoja nikujuze, wataalamu wanasema upakaji wa poda wakati wa kulala si mzuri kwani unafanya ngozi yako izeeke haraka. Pia kupaka poda kila wakati napo si nzuri kwa ngozi yako. Ndo maana unaona hawa ma-celebrity wengi wanaishia kufanya ‘medical skin enhancement’ kwani ngozi zao zinajikunja na kuzeeka haraka kuliko umri wao.

Jalibu kupaka make-up pale inapobidi siyo kila wakati. Jiamini na ujikubali jinsi ulivyo that’s the best make-up any woman can wear. Nothing like self confidence! Mbarikiwe!

Leave a Reply