NIMEKUENZI FIDEL CASTRO KWA JINA LAKO-Peter Sarungi

Peter Sarungi (Next Speaker-Baba Pilato)
Peter Sarungi (Next Speaker-Baba Pilato)

Kuna watu hawawezi kupotea dunia kwa sababu ya alama walizoweka wakati wa maisha yao. Mmoja wa watu hao ni aliyakuwa muasisi mkombozi na raisi wa kwanza wa CUBA Fidel Castro.

Fidel Castro alifanya jambo ambalo lilifanywa na watu wa zamani waliokuwa na ujasiri mwingi, uthubuti mwingi, uzalendo mwingi, utu mwingi na maono ya kuifanya nchi yake ijitegemee. Hawa ni kizazi cha Kwame Nkuruma, Julius Nyerere, Nelson Mandela, Patric Lumumba, Samora Mashel na wengine wengi waliokuwa wakipambana katika kutimiza maono yao kwa nchi. Hivyo ndo vizazi vilivyokuwa na hisia za ukweli za uzalendo kwa taifa lao.fb_img_1480340327658Huyu Fidel ndio chanzo cha mimi kumwita mwanangu jina la FIDEL PETER SARUNGI nikimwenzi Jasiri wa CUBA. Historia ya Fidel ni kubwa na imebeba vitu vingi ingawa natamani kama mwanangu akirithi ujasiri, uzalendo, utu, uthubutu na uwezo wa kutawala. fb_img_1480257721064Mungu ailaze roho ya Fidel Castro mahala pema, yeye amekwisha maliza kutimiza maono yake na ameacha alama kwa jamii yake. Mungu atusaidie na sisi tutimize maono tuliyobeba.

R.I.P FIDEL CASTRO

Leave a Reply