NIMESHAWAHI KUWA MWANAFUNZI, MWALIMU NA SASA NI MZAZI- Peter Sarungi

Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)
Na Peter Sarungi (Next Speaker, Baba Pilato)

Tusiishie kuwalaumu walimu pekee………

Siku kadhaa zilizopita mitandao yetu ilipatwa na mshituko kwa video iliyosambaa inayoonesha mwanafunzi akipata kipigo cha kuheshimiana kutoka kwa walimu zaidi ya tano. Video hiyo ilifanya wananchi wahoji na kushutumu usimamizi wa mfumo wa elimu nchini. Kalele zilizopigwa ziliwachanganya wanasiasa na viongozi hadi baadhi yao wakafanya maamuzi magumu na ya gafla na hata ya kuharibu maisha ya walimu ili tu kushusha hasira za walalamikaji. Tukio hili liliendeshwa kisiasa hadi hukumu ikatolewa kwa walimu na kudhalilisha taaluma ya ualimu kwa jamii yao. Taaluma ya Ualimu ambayo ilikuwa ikieshimika kipindi cha Baba wa Taifa Nyerere sasa imeanza kugeuka kuwa chungu kwa jamii na kwa walimu wenyewe.

Lawama na hukumu zilizotolewa kwa walimu hazisaidii kama hatuta angalia chanzo cha matukio haya. Mimi niliwahi kuwa mwalimu wa kurasini sekondari kwa miaka 4 yaani 2006 hadi 2010, naju nini maana ya kuwa mwalimu kwa shule za sekondari za serikali hasa shule za kata na za mijini. Kuna msemo unasema “Kitanda usicho kilalia uwezi jua kunguni wake” wengi wanao lalamika kwa kuhukumu taaluma ya Ualimu ni wale wasio jua mahusiano yaliyopo kati ya mwalimu, taaluma ya ualimu na mfumo wa Elimu uliopo nchini. Mfumo wetu wa elimu una mwacha Mwalimu kuwa mpweke asiyekuwa na utetezi wa changamoto anazokutana nazo kila siku akiwa kazini. Jamii ina mfikiria mwalimu kama vile ni malaika ambaye akikosewa anyamaze na yeye mwenyewe asikose wala asishiriki makosa, wanaamini kuwa mwalimu ni wito kama wa kiongozi wa dini ambaye hata akitukanwa, akapigwa na hata kudhulumiwa aishie kuomba na kushukuru Mungu. Yaani bora hata viongozi wa dini wa siku hizi wanapata maslahi ya kufurahia wito wao hadi wanamiliki magari, machopa na majumba ya kifahari na wana miradi mikubwa yenye kuwapa uhakika wa kuishi kwa furahi wao hadi kizazi cha vitukuu, lakini kwa walimu wito huu ni tofauti kabisa. Wito huu kwa walimu umegeuka kuwa ni adhabu na mateso ya maisha, wanashukuru jana yao kupita lakini hawajui kesho yao ikoje huku wakiugulia leo yao, maslahi yao yamewekwa kuwa ya mwisho kiasi kwamba hata mwanafunzi anathaminiwa kupita mwalimu anayemfundisha. Mwanafunzi atasomeshwa bure, atajengewa mabweni ya kulala, akimtukana mwalimu na kumpiga hafanywi chochote hadi ushaidi upatikane na hata akifeli atafanyiwa sherehe na bado atasingizia ufundishaji wa walimu.

Mfumo wetu wa Elimu una wadau wakuu 4 ambao ni walimu, wanafunzi, wazazi na serikali. Walimu wamekuwa wakilaumiwa na jamii bila kuangalia mchango wa wadau wengine mfano wazazi ndio walezi wenye mamlaka ya kifundisha tabia mbaya ama nzuri za watoto wao, wanafunzi ambao wanatengenezwa ki taaluma na ki tabia nao wengi wao wamekuwa wahuni wasiojali elimu, serikali nayo kama baba mlezi wa mwalimu imemtelekeza mwalimu kiasi kwamba anaishi kama shetani katika nchi yake. Sasa ni kwanini tuwaaumu walimu pekee na kupiga kelele ya hukumu kwa taaluma ya ualimu wakati wadau wengine nao wana sababisha haya? Ikumbukwe hakuna sekta yenye waajiriwa wengi kuliko Walimu, nahofia kama jamii ikiendelea kuwahukumu kwa makosa machache kama haya na ikawa kimya katika kuwa tetea maslahi yao ya kuishi, ipo siku walimu watachukia na kuhuzunika na huo ndio utakuwa ni anguko kuu la Elimu Tanzania(naomba siku hiyo isifike).

Lakini inawezekana kelele na lawama hizi zipo mijini hasa Dar kwa wanaume wanaoshinda gym kwa chips soda kisha wakitaza na kukaa kimya wakimuona Scorpion mtoa macho akijitokeza hadharani kufanya yake ???… sio kule kwetu Mara aisee…

#Mytake Tusilaumu na kuhukumu taaluma iliyotupa uelewa wa kupambanua mambo katika jamii hadi kufikia wengine wana tukana taaluma hiyo badala yake tukemee tabia ya mwalimu kama binadamu na tupige kelele za kuimarisha mazingira ya walimu na ufundishaji kwa niaba ya walimu ili nao wafurahie wito huo kama wachungaji na mashekh wanavyo furahia wito wao.

Bado nakuheshimu mwalimu wangu uliyenitoa tongotongo usoni kwa viboko, vifinyo na vibao ili mradi nipate elimu uliyo kusudia na ndio maana nipo hapa kwa nguvu ya elimu nikitaka kuwa Spika wa Bunge letu. Nakushukuru sana Mwl. Alexander Robert.

Kama na wewe bado una imani na walimu basi washukuru walimu wako kwa kukoment.

Asanteni sana.

fb_img_1472436063790Well! Well! Well! My brother! Nimesoma hiyo article yako nikajihisi maumivu ya uchungu wa kuzaa mtoto!!! Hapa nilipo natetemeka! Najaribu kumuomba Mwenyezi Mungu anisaidie nikuandikie huu ujumbe kwa lugha ya kawaida maana lasivyo hasira zangu zote kuhusu huu ukatili usio elezeka zitaishia kwako!!………. Ati??!! What are you trying to say??!! Are you out of your mind??!! Seriously, are you trying to justify these MONSTERS’ act with what?! Ati wanafunzi wakorofi?!! Kwani hawakujua kuwa uwalimu ni wito!! Ati mazingira ya kufundishia?!! Well, waache kazi ya uwalimu wakauze chips wakatengeneze mazingira wanayo taka!! Ati case zinachukua muda mrefu kupata ufumbuzi?! So what?! Hiyo inakupaje wewe haki ya kuweka mikono yako (kumpiga) mwanadamu mwingine achilia mbali kuwa ni wanafunzi!! …….. Hivi umeona hawa mashetani walivyokuwa wakimpiga huyu mtoto?? KICHWANI NA USONI!! Hiyo ndiyo adhabu mwanafunzi anatakiwa apewe kisa hakufanya HOMEWORK???!! My brother are you OKAY!!! Walimu 6 mwanafunzi mmoja mwenye uzito chini ya 200LB na urefu usiyo fika 5ft?!!  Don’t you see kuwa hawa watu walikuwa wamekusudia KUUWA HUYU MWANAFUNZI!!!  Kichwa cha mtu si ndiyo ubongo wake ulipo sasa kumbonda namna ile kichwani kwake nia ilikuwa ni nini kama si kuuwa?? Je huyu mtoto akija pata matatizo ya kudumu kwasababu ya hiki kipigo wewe unaona ni sawa?! Who knows kama amepata itilafu yoyote kichwani mwake au internal  bleeding yoyote ile?! Au any kind of brain trauma?! ……….My brother! Were you drunk ulipokuwa unaandika au?! How cold is this!! How low for a father of two!! Wow! Umenishangaza mno, umenifanya nikutafakari mara mbili mbili kuhusu ubaba wako!!! Something isn’t right with you brother!!…….. Hakuna sababu yoyote itakayotolewa ambayo itaweza kuhalalisha huu unyama waliofanya hawa mashetani!! Huu unyama lazima upingwe vikali mno!! Na mimi kama ingekuwa ni amri yangu!! Hawa monsters wangepewa kifungo cha maisha jela tena bila kuwa na msamaha wowote! Hata Mwalimu Mkuu wa shule anatakiwa ahukumiwe at least 30+ jela!!

MUNGU IBARIKI TANZANIA. MUNGU IBARIKI AFRICA!!

Leave a Reply