Peter Sarungi atoa shukrani zake za dhati!

HITIMISHO LA HATUA ZA KUELEKEA KUWA SPIKA WA BUNGE: KURA HAZIKUTOSHA. FB_IMG_1447783174533Ndugu jamaa marafiki na wadau wangu wote na popote walipo, nitoe shukrani zangu za dhati kwa sappoti yenu toka nilivyoanza hatua ya kwenda kuwa spika wa bunge. Ki ukweli nimefarijika sana na mapenzi yenu makubwa kwangu na kunichangia kwa hali na mali pamoja na ushauri mliokuwa mkinipa na kunifariji. Nilikwenda kushindana lakini pia nilikwenda kuzindua hatua zangu nyingi za mbele katika siasa. Nashukuru malengo yangu yamefanikiwa kwa 90% na huu ni ushindi kwangu kwa kuweza kufanikisha sauti yangu ya siasa kusikika kwa nchi nzima na kwa watawala wa nchi kwa mara ya kwanza. Niwashukuru sana Chama changu cha AFP kwa kunipa fursa pasipokujali hali yangu ya ulemavu, niwatie moyo kwamba mmefanya maamuzi sahihi kwa jamii ya walemavu na Mungu awabariki sana. Pia nimshukuru mama yangu mzazi kwa kunilea katika ujasiri huu mkubwa ulioweza kunifikisha hapa. Nichukue fursa hii kusema kwamba; nimeanzisha rasmi safari yangu ya kisiasa Tanzania. Hivyo mtarajie mengi ya kujenga jamii ya watanzania kutoka kwangu. Nawashukuru sana na Mungu awabariki zaidi ya jana. Amen… Share, Like, Comment na Tag kusambaza ujumbe huu ili kuwatia moyo watu wa makundi maalum wanaotamani kusikilizwa sauti yao. FB_IMG_1447783206038

2 thoughts on “Peter Sarungi atoa shukrani zake za dhati!”

Leave a Reply