“Taa nyekundu ya mwanadamu si ya MUNGU hicho ndicho ninacho amini”-Loveness Goodluck

Tarehe 18-10-2014
Hakika ni cku iliyokuwa mbaya maishani mwangu ila ubaya huo ulichukua muda mchache sana na kisha ikageuka kuwa siku yakupokea muujiza wangu

Ilikuwa ni siku ya Jmosi majira ya jioni, nilikwenda kumsalimu shangazi yangu aliekuwa amelazwa ktk hospitali ya K.C.M.C. Nikiwa pale ghafla simu yangu iliita nami nikaipoke alikuwa ni mdogo angu, aliniulza dada uko wapi? nikamjibu nipo hosptalini bado, akaniulza tena je wafahamu alipo mwanao? nikamuulza nini maana yako hasa?alinijbu tu nisamehe kisha akakata simu ila aliniacha na maswali.

Nilichukua simu ili kuwatafuta wazazi wangu na mdogo wangu ambae ndiye nilimwacha na mtoto ila hakuna hata mmoja aliyeipa ushirikiano simu yangu kwa kuipokea. Basi nikaamu kuaga ili niondoke kuelekea nyumbani, wakati nikiwa nimempa shangazi mkono il tuagane simu yangu ikaita mda huo alikuwa ni mama yangu mdogo nikaipokea, aliongea huku akilia, naomba uniambie nini kimemuua mjukuu wangu yani mwanangu Brayton(Deodatus) nikamjibu mama mdogo sikuuelewi naomba uniambie vizuri ndipo akajibu kwa kusema nimepigiwa simu mwanao kafariki! Ilikuwa ni vigumu kuamini ujumbe ule, lakini ghafla nikapokea tena simu kutoka kwa dada yangu akiniambia mwanao alianguka kwenye maji tumempeleka zahanati tumeambiwa amefariki hivyo tupo njiani kuja KCMC

Wapendwa cha ajabu sikupata nafasi ya kulia japo nilipokea taarifa ngumu kwangu! Ila nilipata nafasi yakupiga magoti nikanyanyua simu  yangu kuelekeza juu nikiwa nimeweka picha ya mwanangu

Nikasema Ee Bwana mtizame mwanangu Brayton, naomba umtetee na umuokoe kama ulivyo waokoa watumishi wako Meshack, Shedrack na Abernego walipotupwa ktk tanuru la moto, msimamie kama ulivyo msimamia mtumishi wako Daniel alipowekwa katikati ya simba wenye njaa kali, kisha nikasema si niwewe Mungu ulietuahidi ktk kitabu cha Yeremia 33-3 kuwa tukuite nawe utaitika na kutuonesha mambo magumu na mazito tusiyoyajua? Mungu hukuzungumza na Yeremia peke yake hivyo nakuomba ukatende na kwa mwanangu leo, kausha yale maji na uweke uzima ndani yake kwani  bado namuhitaji  mwanangu Mungu.

Nilikuja kushtuka baadae kwani baada ya sala nilipoteza fahamu nikakuta nimezungukwa na watu wengi na wachungaji sikujua walitokea wapi ila walikuwa wakifanya maombi yakupinga roho za mauti

Ghafla nikasikia sauti ikisema kwa mbali mama Brayton njoo mwanao anakuita, waliponifikia walikuwa na ma-nurse tena wanalia, nikawauliza kama mwanangu hajafa na ananita mbona mnalia? fb_img_1477191081255Wakajibu tunalia kwasababu alipoletwa alikuwa teyari alishajisaidia haja zote na kupoa kabisa mwili wake ila mama yako aliomba ampulizie tena pumzi yake kwani anaamini  Mungu hakumpangia mjukuu wake kifo kile. Mama yangu alimpulzia pumzi  mara ya kwanza, ya pili, mara ya tatu akashtuka na kusikika akisema mama yangu njoooo!
Nilipofika alipokuwapo mwanangu nilimkuta baba yangu akiwa analia akaniambia mwanangu nalia kwasababu ya ukuu wa Mungu hivyo ondoa hofu mwanao yu hai, mwanangu aliponiona alilia akisema mama yangu njoo unipe nyonyo mama.

Doctor aliniuliza unaabudu kanìsa gani?nikamjibu RC akaniambia inakpa ukatoe sadaka yakushukuru kwani sijawahi pokea mtoto aliefikia hatua hii kisha akaurudia uhai.
Asubuhi watu walifika kunipa pole ila walishangaa nilipojibu asanteni ila mwanangu yu hai. fb_img_1477191050114Wapendwa taa nyekundu ya mwanadamu si ya MUNGU hicho ndicho ninacho amini
Upitapo ktk magumu wewe mwite Mungu kwani yeye pekee ndie msaada uonekanao kwa nyakati za shida. BARIKIWA WEWE UAMINIE KUWA MUNGU HASHINDWI NA CHOCHOTE. AMINA.

Source: Loveness Goodluck Facebookscreenshot_2016-10-22-22-40-13-1fb_img_1472436063790Nimekwenda kuchungulia zaidi profile ya Loveness ili nione picha za mtoto alizopiga hivi karibuni. Nikakuta kumbe Brayton amezaliwa October 16th!! Hivyo tukio hili lilitokea 2 days after his birthday ?? …… It would have been a very-very sad situation. Losing a child 2 days after his birthday?!!  Can’t imagine! But hey! The answer is ?fb_img_1476441794547

Leave a Reply