Tatizo la technology

Jamani hakuna kitu kina nikera na ninaweza kusema sikipendi kabisa kama ninavyo ona watu wako busy wakati wa mambo ya muhimu kama hapo kwenye picha chini!!

2015-04-11 19.48.14Mwanzoni nilifikiri ni mwanangu tuu ndo anahii tabia mbovu laakini kumbe watu wengi tuu; inawezekana hili likawa “janga la dunia.” Kwani si watoo, si vijana, na wala si watu wazima yani wote wana hili tatizo. Najiuliza why? Ndo madhara ya technology au ni watu tuu kujiendekeza? Mie sielewi kwani hii tabia sina, labda kutoka na field niliosoma imenifanya kidogo niwe mwangalifu sana wa tabia kama hizi.

Utakuta mtu kaalikwa kwenye sherehe, lakini yupo busy na simu it’s just so rude! Wewe umealikwa kwenye sherehe ya mwenzio kwanini usiweke mawazo pale, onyesha heshima kwa wenye shughuli. Na kama unaona ina ku bore si uondoke kimya kimya?

Wengine bila aibu wala hofu ya Mungu utakuta kanisani (not sure about Msikitini) yupo busy na simu utafikiri ni standby surgeon!! Na wengine hata kwenye ibada za mazishi wao wapo busy, yani roho ngumu kama kazaliwa na Farao!!

Embu kama unaweza badilika basi jitahidi ubadilike. Mie hapa napiga kelele sikuhizi amepunguza kidogo ila sito nyamaza mpaka atakapo acha  😉    😉

Leave a Reply