Ukifunga “nira” na mchawi basi nawe ni mchawi tuu!

Ngoja niende moja kwa moja kwenye point yangu, kwasababu wote tunajua sasa “hot topic” kwenye siasa za Tanzania. Uwamuzi wa Chadema / UKAWA kusema kuwa watamsimamisha Edward Lowassa kuwa mgombea urais upande wa upinzani ni sawa na “kufunga nira” na mchawi ambapo wote aliyeolewa na muoaji watakuwa wachawi tuu!

Sababu ya kusema hivyo ni kwamba hawa hawa Chadema / UKAWA ndo waliowaambia Tanzania kuhusu ufisadi wa Edward Lowassa, kwandimi zao wakatamka (tazama video hapo chini) na tena wakasema wanaushahidi! Kwamba wao wako kupigania kukomesha ufisadi na rushwa Tanzania, na kulikoni leo mtuhumiwa yule ambaye alikuwa kati ya vinara ndiye mnayetaka kumsimamisha kuwa mgombea urais?! SMH! Watu walioshuhudia wamesema Edward Lowassa amemuhonga Freeman Mbowe 10bilioni ili aweze kuwashawishi viongozi wa UKAWA wampe hiyo nafasi. Cha kushangaza mpaka leo hii sio Mbowe au Lowassa aliyekanusha tuhuma hizi, ambapo inatufanya tulio wengi tuamini ni kweli!!

Wanasema kuwa E.Lowassa alionewa, swali langu alionewa na nani? Maana CCM haikumuita Lowassa fisadi bali ni upinzani! Wanasema kama ni fisadi mbona hakupelekwa mahakamani, swali langu nani alikua anatakiwa kwenda mahamani kumshitaki? Sio wao waliokuwa na ushahidi ndo wangeenda kufungua kesi kama viongozi wa upinzani ambao wanapenda maendeleo ya taifa lao?! Na kama Lowassa alisingiziwa na alikuwa na haki ya kwenda mahamani kupata haki yake, mbona hakufanya hivyo?

Wengine pamoja na Lowassa mwenyewe wanasema jina la Lowassa lilikatwa kwasababu za chuki binafsi nda ya CCM. Sasa hivi nini maana ya DEMOKRASIA? Hivi ule si ulikuwa ni mchakato ambao wengi waliingia na demokrasia ikatumika kukata majina yao kulingana na katiba na kanuni za CCM? Kwanini yeye ndiyo aone kuwa ndiye aliye stahili kushinda? Na aliposhindwa anaona CCM mbaya?! Hiko wapi hiyo demokrasia ambayo anasema anaimpenda kama alitaka jina lake ndiyo lipitishwe na mengine yakatwe?! Alijipangia na kutangaza matokeo ya ushindi kabla ya ‘mechi’ kuanza! SMH!

Inashangaza sana na kichekesho kikubwa sana kuona Chadema na UKAWA wakisema kua tatizo ni “mfumo wa utawala” ambao hupo chini ya CCM ndiyo unamatatizo. Kwamba mfumo wa utawala uliopo ndiyo unalea na kulinda mafisadi. Sasa jiulize Edward Lowassa amekulia na kulelewa wapi? Si kwenye mfumo huohuo ndipo alipoalizaliwa na kukulia huyo ambaye mnataka asimame kugombea kiti cha urais? Sasa yeye atakuja na mfumo hupi zaidi ya ule aliyokulia na kulelewa nao?! Nakama mmemuamini mtu aliye zaliwa na kulelewa na CCM kuwa ndiye anafaa kupeprusha bendera ya upinzania sasa kunahaja gani ya kuitoa CCM madarakani wakati viongozi bora wanatoka ndani ya CCM?

Uchu wa madaraka na umasikini wa fikra wa Watanzania ndiyo utakao liangamiza taifa la Tanzania. Hivi mtu kama Dr. Slaa atatuambia nini kuhusu aliyoyasema juu ya ufisadi na wizi wa Lowassa? Watanzania ambao wanashabikia hii ndoa ya UKAWA na Lowassa ni watu ambao hawana uchungu na wala hawalitakii mema taifa. Huwezi funga nira na mchawi halafu ukasema wewe si mchawi! Hiyo haiwezekani hata kidogo! Kama walisema Lowassa ni fisadi na sasa wanaunganisha damu na fisadi basi hata UKAWA NI MAFISADI TUU!

Hatma ya Tanzania ipo mikononi mwa Watanzania wenyewe. Kura yako ndio mkombozi wa inchi yako! Mwenyezi Mungu awatangulie katika kipindi hichi cha uchaguzi, wawe na hekima ya kutosha na kufanya maamuzi yatakayo isaidia Tanzania kuzaliwa upya na si kuiteketeza!

MUNGU IBARIKI TANZANIA. MUNGU IBARIKI AFRICA!

Leave a Reply