WATANZANIA YATUPASA KUBADILIKA

 

Sehemu ya tatu: (Wafanyabiashara Badilikeni)

Peter Sarungi
Peter Sarungi

Wafanyabiashara ni wadau muhimu sana wa amani na ustawi wa nchi. Wao ndio chachu kuu ya ukuaji wa uchumi wa nchi pamoja na mwananchi mmoja mmoja. Nchi yoyote dunia ingependa iwe na wafanyabiashara wazalendo au wafanyabiashara wenye kufuata taratibu na sheria za biashara zilizowekwa ili nchi hiyo iweze kufaidika na biashara husika.

Mfanyabiashara mzalendo sio lazima awe mzawa ila ni yeyote yule mwenye kujali mahala anapofanyia biashara yake kwa kufuata taratibu na sheria za nchi hasa ya kulipa KODI. KODI ndiyo inayo endesha shuguli zote za serikali ikiwa ni mapoja na kuimarisha huduma bora za kijamii na mazingira mazuri ya uchumi kama vile miundombinu, mawasiliano, ulinzi na usalama, huduma za kisheria, kusimamia ushindani wa kibiashara, utawala bora na mengine mengi yanayogusa maslahi ya wafanyabiashara.

Lengo kubwa la biashara ni kupata faida na kuendelea kupata faida miaka ijayo, biashara yoyote ile ni lazima ilipe (ilete faida) kama utaifanya wakati sahihi, mahala sahihi na kwa wateja sahihi na ndio maana imeitwa biashara. Lakini wafanya biashara wengi wamekuwa na tabia mbili mbaya sana kwa maendeleo ya Taifa letu. Kwanza wamekuwa na mazoea na tabia ya kukwepa kodi kwa kufanya kila linalowezekana ili wasilipe KODI kwa lengo la kupata faida maradufu. Hii tabia haikubaliki jamani maana wateja wenu ambao ni wananchi wamekuwa wakikubaliana na bei zenu wakiwa na imaninkuwa kuna sehemu fulani inakwenda katika serikali yao kama kodi kwaajili ya kuendeleza nchi lakini wafanyabiashara hawa wasiokuwa wazalendo wamekuwa wakichukua mapato yote hadi yale ya serikali (KODI). Hii tabia inaleta uchonganishi kati ya serikali na wananchi wake ambayo ni hatari sana na haikubali.

Pili, wafanyabiashara wamekuwa na tabia nyingine ya kulalamika kwa matatizo wanayoyapata katika biashara zao bila kuangalia chanzo. Lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa wasimamizi wa biashara na serikali inapotokea mazingira yao ya kufanyia biashara hayapo vizuri, lakini ukichunguza kwa undani utakuta matatizo haya yamesababishwa na baadhi ya wafanyabiashara wenyewe kwa kukwepa kulipa KODI ambayo ingeweza kuwaondolea matatizo yao. Nakubali sio matatizo yote yanasababishwa na wao lakini mengi wao ndio chanzo.

Nawasihii mbadilike na mjifunze kuwa wazalendo na wenye kufuata taratibu na sheria. BADILIKENI…

Niwakumbushe wafanya biashara kuwa Serikali ya sasa sio ile ya miaka iliyopita, Serikali ya sasa ni ya KAZI NA KODI TU. Mh. Raisi ana maono ya kuifanya Nchi kujitegemea yenyewe kwa kuendesha serikali na kuleta maendeleo kwa fedha zake bila kutegemea misaada, haya ni maono mazuri na ya kuunga mkono. Tufike mahala hata wewe mwenyenyumba ya kupangisha ulipe kodi kwa serikali baada ya kupokea kodi kutoka kwa wapangaji kama alivyoshauri mtaalam wa uchumu Valentine Vedasto alipokuwa anahojiwa na BBC.

Walioteuliwa kumsaidia Mh. Raisi (Dr. JPM) wafanye hiyo kazi kwa spirit kama ya Raisi, wasimuangushe maana tuna imani na maono yake.

Na Peter Sarungi

Leave a Reply