Wazazi tizameni watu kwa macho matatu!

Screenshot_2015-11-29-08-08-19-1Sijui nieleze vipi ili nieleweke na iwaingie akilini kweli kweli pale ninaposema wazazi siku zote “treat everyone as a suspect!” Kamwe usiamini mtu na mtoto wako awe wa kiume au wakike! Hii story imekuja mwanzoni mwa wiki iliyopita November 20th, huyu daktari wa meno ajulikanaye kama Dr. John Wolf (mh! Hiyo last name yake tells all about him) amekamatwa na kufikishwa mahakamani kwa makosa ya kuuza/ kusambaza picha za uchi za watoto (child pornography), kuuza na kusambaza madawa ya kulevya (drugs; meth), na uwenezaji wa HIV! Screenshot_2015-11-29-08-13-09-1Hiyo picha juu ??ndipo office yake na hospitali yake ilipo. Hivi unaweza amini kuw mtu mwenye hospitali nzuri kama hiyo anaweza kufanya mambo ya mna hiyo?#SMHOH! Wazazi mtazame na uwadhibiti watu wote wanao mzunguka mwanao au wanao kana kwamba wote ni WAHALIFU MACHONI PAKO mpaka siku utakapojua hawana hatia. Any the only way ya wewe kujuwa kuwa hawana hatia pale mwanao atakapofika at least umri wa miaka 18. Mimi nasema umri wa miaka 20!! Nasisitiza hili swala haswa wazazi wenye “ngozi nyeusi” wanao wageuza “wazungu” mungu mtu! Yani unakuta mtu yeye kitu labda kifanywe na mzungu ndo anaona kipo sahihi lakini akifanya mwafrika mwenzie hapana! Yani ni utumwa na umasikini wa fikra uliopindukia! Usiniambie eti “Mungu yupo” huo ni upungufubwa hekima! Kwani hata Mungu amesema tujilinde kwanza naye atatulinda. Huwezi ukafanya makosa ya kizembe kwa madai ya “Mungu yupo” huo ni ukichaa!! Tazameni watu kwa macho matatu bila kujali usomi wake, rangi yake, ukarimu wake, wala pesa yake!

Screenshot_2015-11-29-08-11-12-1

Unaweza soma hiyo story yote hapa ✌

3 thoughts on “Wazazi tizameni watu kwa macho matatu!”

  1. MMH DUNIA INATISHA SANA HATA KUKAA NA NDUGU MBONA NAOGOPA KAMA HALIJAKUPATA UWEZI KUELEWA NAOMBA MWENYEZI MUNGU ATUSIMAMIE KWA YOTE.

Leave a Reply