Wendy Williams ampinga Oprah na Shonda!

Screenshot_2015-12-01-11-07-48-1Katika show yake ambayo imepita karibia wiki mbili sasa, gwiji la talk show ya The Wendy Williams’ Show alisema kuwa kuna wamawake ambao wanawapotosha wasichana wadogo na waliopo college kuwa ukishwa kuwa na elimu nzuri na pesa ya kutosha huitaji mwanaume au kuolewa kwani anakuwa hana faida yoyote! Wendy Williams alisema kuwa huo ni upotoshaji wa watoto wakike na siyo sahii. Kwani anaamini hakuna kitu kizuri kama “the comfort of the man”! Wendy alizidi kusema kuwa zamani alikuwa anaona aibu kusema kuwa she’s “pink and soft” kwahiyo mwanaume ni muhimu kwake! Lakini kwasasa haoni aibu kusema hivyo tena! Amesema wasichana wasijitie ujinga na maisha ambayo Oprah na Shonda wanajaribu kuwaonyesha! Amewasihi wasichana wadogo na ambao wako college kuwa ni vyema kwa mwanamke kuwa na mipango juu ya maisha yako ya career na pia personal life! Embu msikilize mweyewe kweye hii clip wakati akiongelea “hot topic” unaweza kuanzia dakika ya 10.28sec kama hutaki kuangalia yote!

Mimi kwa maoni yangu niseme kuolewa ni MUHIMU LAKINI SI LAZIMA! Sioni kwanini mtu ujifunge kitanzi na ndoa isiokuwa na mbele wala nyuma! Kama ukatokea ukaolewa na una amani na furaha kwenye ndoa yako basi ni vyema na mshukuru Mungu! Kama ukatokea kuolewa halafu ndoa imejaa manyanyaso,  uwonevu, na ukatili wa hali ya juu; mie naona nibora ujikalie mwenyewe! Ndoa inatakiwa iwe jambo la furaha na kama hamna furaha basi nibora “nusu shari kuliko shari kamili!” utajikuta unaishi maisha yasiyo na amani halafu raha ya  Mbinguni usiione na duniani amani ulikosa! Na kama ukatokea kutokuolewa hata mara moja basi napo mshukuru Mungu maisha yanaendelea vile vile kwani kutokuolewa si kifo na wala si kikwazo cha kuuona ufalme wa Mungu! I mean marriage isn’t for everyone!

Katika maswala ya kuwa na mtoto au watoto, kama unaweza basi kuwa na mwanao hata mmoja! I can’t imagine how  life would have been without my daughter! hivyo siwezi kukudanganya kuwa usiwe na mtoto. Lakini kama haujabahatika au Mungu hakukupa uwezo wa kuzaa mtoto basi shukuru Mungu na maisha yanaendelea vilevile! Kuto kuzaa isn’t a Death sentence! Vivica Fox alishawahi kusema anajutia kutokuwa na mtoto wake japo anao nieces na nephews ambao anawalewa kama wanae wa kuzaa lakini anatamani kama angekuwa na mtoto wake mwenyewe! Msikilize akiongea na Oprah Winfrey ?

Naye Rosie O’deal alishawahi sema mtoto wa ku- adopt huwezi juwa kama ni wako kweli mpaka atakapofikisha miaka 18! Kama hatokubadilikia basi hapo utasema ni mwanao! Hivyo basi kama unaweza nakushauri  jipatie mwanao mwenyewe, kwani man comes and goes but your child will forever be there!

Anyway, wewe wasemaje? Funguka! Naomba nikukumbushe huitaji kuweka email wala jina lako kwenye comment! Thanks!

 

One thought on “Wendy Williams ampinga Oprah na Shonda!”

Leave a Reply