Dawa ya meno ya asili: Nazi na Baking Soda

Nimesoma mahala fulani kuwa hizi dawa za mswaki zinawekewa kiwango kikubwa cha Fluoride kwaajili ya kutungarisha meno lakini si kitu kizuri kwa afya zetu na meno yetu. Vile vile kutokana na maji mengi sikuhizi huwekewa Fluoride ilikuuwa vijidudu vya magonjwa hivyo unapotumia tena toothpaste unakuwa umetumia kiwango kikubwa sana cha Fluoride ambacho kinakuwa ni hatari sana kwa afya zetu, unaweza hata kupata matatizo kwenye uti wa mgongo ambayo ni hatari sana! 832505-coconut-oilSasa nikaona mtu amesema yeye alishaacha miaka mingi kununua dawa za mswaki. Yakwamba huwa anatengeneza mwenyewe! Anachukua mafuta ya nazi halisi ( ambayo hayaja changanywa na kitu chochote) na ana-mix na baking soda basi! how-to-use-baking-soda-to-clean-face-skin-clean-your-hair-whiten-your-teethKwakuwa nilikuwa sijawahi sikia wala ona nikaamua kufanya uchunguzi wangu kidogo. Inasemekana ni dawa ya meno nzuri sana haswa kwa wale wenye matatizo ya fizi na ukakasi wa meno! Nimekuta ni kitu watu wengi wanatumia. Tazama hii video ??

Pia kwa wale wanao sumbuliwa na makovu ya chunusi pia unaweza kutumia mchanganyiko huu kusafishia uso. Unasugulia kama scrub halafu unaosha. Hii ni kitu cha halisi hivyo ni “unisex” yani kwanwote waume kwa wanawake wanaweza kutumia. Pia unaweza tumia maji na baking soda btuu kwa ajili ya uso wako hila coconut oil!  Haya enjoy the product!

N.B: pia unaweza tumia mkaa na chumvi kusafishia meno. Kama unaweza pata mswaki ile ya miti basi ni mbora zaidi kuliko hii ya kisasa.

Leave a Reply