Tegemeo Sambili: Ili tuendelee kwa haraka na watu wayaone maendeleo, nashauri tuongeze nguvu kwenye yafuatayo:-

Moja ya Makosa tunayoyafanya ni Kutaka Kuendelea kama Walivyoendelea Wajeruman, Wamarekan, China, France……. Kwa Upande wangu, Maendeleo yanaanza kwa Kula vizuri, Kulala vizuri, Kuvaa vizuri na kuwa na Afya njema. Ili tuendelee kwa Haraka na Watu Wayaone Maendeleo, nashauri tuongeze nguvu kwenye Yafuatayo:-

1. Kilimo Tulime sana kiasi cha kuwawezesha Watanzania kupata Chakula bora na cha kutosha. Nataman kuona Chakula kinakuwa kingi kiasi cha kilo 1 ya unga iwe Tsh 500, kilo 1 ya mchele iwe Tsh 1200, Karoti 1 iwe Tsh 50,pilipili hoho iwe Tsh 50, Nyanya fungu 1 liwe Tsh 200, Vitunguu Tsh 50, Nyama, Samaki….vipatikane kwa bei nafuu. Ikiwa Watu watapata Chakula bora, kwanza watakuwa na Afya , Miili yao itakuwa na uwezo wa Kujikinga na magonjwa na Wataweza kuishi miaka mingi. Life span ya Watanzania ni Fupi kwa sababu ya Chakula dhaifu…. JKT itumike kulima Chakula kwa ajili ya Watanzania.

2. Nyumba na Makazi bora Nataman kuona kila Kaya inaishi kwenye Nyumba ya kisasa.Lazima tuhakikishe watu wetu wanalala sehemu nzuri na salala.Katika kutekeleza hilo, serikali kwa kutumia Watalamu wa Majengo na Mipango miji, Wanaweza kuandaa Ramani za Nyumba za Mwongozo, zitakazoelekeza aina ya Nyumba ambazo watu Watatakiwa kujenga na Zigawiwe bure. Vifaa vya ujenzi Viondolewe Kodi na Serikali inaweza kushiriki katika kuvisafirisha hasa maeneo ya Vijijini ili Wakazi wa maeneo hayo Waweze kuvipata kwa gharama Nafuu. Serikali iwahamasishe watu Kujenga nyumba zao..

3. Mavazi Tuongeze nguvu katika kujenga Viwanda vya nguo. Watalamu wa Mavazi, wabuni nguo zinazowafaa Watanzania wa kike na kiume.Watu maarufu kama akina Kikwete watumike kuzitangaza ili kuwahamasisha Vijana kuvaa nguo hizo.Vijana wetu wanavaa uchi Kwa sababu wamehamasishwa kufanya hivyo na Hatuna Mavazi yetu mazuri

4. Huduma za Afya Tuwekeze nguvu kwanza katika kutokomeza vyanzo vya magonjwa…Pili tuhakikishe huduma bora za afya Zinazotibu Maradhi yanayowasumbua watu wetu haraka. Kuongezeka kwa Vituo vya tiba mbadala ni Ishara kwamba Hospital zetu zimeshindwa kutibu Maradhi yanayowasumbua watu wetu. Tukitaka kuendelea kama Wao, Hatutafika Leo wala kesho…… Tukiyafanya Mambo haya, Maendeleo yataonekana kwa kila MTU na kila Kaya ndani ya muda mfupi. Tunataka Kuona Tanzania inakuwa nchi ya kwanza Dunian kwa Watu wake Kula Vizuri…. Kulala vizuri , Kuvaa vizuri…..na kuwa na Afya njema… 

Leave a Reply