Usikate tamaa!

watu tunapitia maisha tofauti inategemea na chimbuko la kila mmoja wetu alipotokea yani background yako. Wapo watu ambao wamezaliwa na kukuta kila kitu kipo. Yani mazingira mazuri anayoishi na anauwezo wa kupata maitihitaji ya ziada. Kuna wanao zaliwa na kukutana maisha ya yakawaida, yani si mazuri sana na wala si mabaya. Wanauwezo wa kupata mahitaji muhimu lakini huwezo wa kupata vya ziada hawana. Na wapo wale ambao wamezaliwa katika dhiki na shida nyingi. Yani hata kupata mlolongo wa siku ni tabu. Hivyo wanajikuta wanatumia nguvu za ziada siyo tu kutimiza ndoto zao bali kujikwamua kutoka katika hali duni ya maisha na kupata maisha ya kawaida. Chamuhimu katika yeto ni kuto kukata tamaa. Mungu ndiye mtowaji wa yote naye amesema, ‘watu wangu hawatokuwa mkia’ hivyo ‘ukigangamara’ na kumuweka yeye mbele basi ipo siku utavuka vikwazo! Screenshot_2015-12-07-19-47-50-1Jana usiku niliweka hii picha kwenye Facebook yangu na kuuliza swali “je ulishawahi kuishi kwenye nyumba ya kupanga ndani ya bongoland? Experience yako ilikuwaje?” Basi baadhi ya watu watoa maoni yao kama ifiatavyo ? Screenshot_2015-12-08-12-59-00-1

Screenshot_2015-12-08-12-59-46-1Screenshot_2015-12-08-13-00-01-1Kwakweli mtu ukishapitia mambo fulani magumu au vikwazo ukavivuka salama mara nyingi huwa ukikaa chini na kutafakari unakuwa ni kichekesho au kitu cha kukufanya ucheke! Ninachoweza kusema ni kwamba; umasikini si kilema. Wenye lugha zao wanasema “it is just a condition” na kitu chochote ambayo ni conditional inamaana inaweza change anytime! Haidumu! Hivyo usikate tamamaa wala kusikiliza watu waliopungukiwa na hekima!

 

 

 

 

Leave a Reply