Asanteni sana the Kakoschke na Kimesera

screenshot_2016-11-27-21-25-56-1Very good msg! Love it!
screenshot_2016-11-27-19-12-55-1Sio kwa mahaba haya jamaniiii! Mnatutesa siye wakina single mama ?? …….Wapendwa ni nyakati za ule muda wa mwisho wa mwaka wa kusema asante kwa watu ambao kwa namna moja ama nyingine wamekuwa mbaraka kwa maisha yako. Basi naomba mniruhusu niseme asante kwa familia hizi mbili. Hawa ni watu ambao siku zote nitawashukuru sana kwani wote wamenipa first experience ya ndoto zangu bila hata kusitita au kuweka vikwazo! Wote walikuwa hawajawahi niona wala nisikia lakini walinipa heshima kubwa sana kwa kutoa muda wao na hata pesa pale ilipo bidi.

Zawadi Kakoschke ndio alikuwa mtu wa kwanza kabisa kufanya naye interview yangu  ya maandishi. Somahapa. Na Linda alikuwa ndio mtu wa kwanza kufanya naye interview ya ku-record  (video taped) tazama hapa. Nasio hivyo tu hawa watu walinipa uhuru wa kutumia picha zao na za familia zao pasipo na pingamizi lolote. Sasa nakaribia mwaka wa pili tangu nifungue blog hii na wamenipa 100% support hadi leo hii. Kwani mimi ni nani hata wanijali hivyo?! Sina cha kuwalipa zaidi ya kusema mbarikiwe milele zote. I love you soooooooo much! Nawatakieni siku kuu njema. Mkabarikiwe katika kila jambo jema mlifanyalo! ❤❤❤

Leave a Reply