Cheka urefushe maisha yako!

Eti na wewe unajiita Mwanaume,Mwanaume kumnunulia Zawadi mwanamke wako ni mpaka uone Valentine’s Day imekaribia ndio unajishaua na Shopping ili kusafisha nyota. Nani aliyekwambia Usela unalipa kwenye Mapenzi?? Unahisi ukimnunulia Zawadi na kumuonyesha unampenda utaonekana Bwege, Kuna kosa gani kuwa bwege kwa mtu unayempenda?? Hata wanafiki wakisema umeshikwa waambie NDIO NIMESHIKWA NIMESHIKAMANA! 
Make your Woman Smile……..Wala huna haja ya kutumia fedha nyingi kwenye Shopping za Mariedo. Ukiona kitu kizuri Karume NUNUA Mpelekee. Ukiona Gauni zuri Posta NUNUA mpelekee. Hamna kitu kizuri Wanawake wanapenda kama ZAWADI, hata kama umenunua JERO mtumbani, ile Feeling kwamba Ulipokiona ULIMKUMBUKA YEYE inampa impression kwamba She is On ur Mind na hilo ndo wanawake wanataka……..
Surprise her pale asipotarajia. Mpigie Simu aje, akifika una Parcel ya Saa nzuri. Utapendwa hadi ushangae……..Hawa watu wanaitwa mafataki hakuna Miujiza yoyote wanayofanya kumuiba mwanamke wako zaidi ya hii. Wanajua Wanawake wanapenda nini na wanawapa hicho. Wewe jifanye Msela halafu Mafataki wakufundishe Caring ni nini. USione Couple zinadumu ukajua jamaa anatumia heeelaaaa nyiiiiingi, walaaa…….Mijisapraiz tu,mwanamke anajiona Malkia masaa 24. Sio kila Limbwata imetengenezwa na Mganga wa Kienyeji,Ukitumia Akili tu sometimes ni Limbwata tosha.

Credit to #ChekaUsipasuke

Leave a Reply