Family time-the Sarungis

FB_IMG_1448218676759-1Picha nzuri sana, nimependa mno! Hapa ni baba akimpongeza kijana wake Peter Sarungi kwa kuthubutu! Peter Sarungi alikuwa mmoja wa wagombea walio gombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akiwakilisha makundi maalum  (walemavu). Soma hapa? Inatia  moyo, faraja, na busara ya hali ya juu kuona mzazi akimpa moyo kijana / au  binti yake kufanikisha ndoto alizo nazo. Ubarikiwe sana mzee wetu Prof. Sarungi.

Prof. Sarungi ni baba yake mdogo na Peter Sarungi  (kulia). Baba yake Peter mzee Obwago Sarungi yeye ni marehemu kwa sasa. Na kushoto ni binadamu yetu Saba-saba (Sabi) Sarungi. Yeye ni mtoto wa marehemu Saida Sarungi ambaye alikuwa ni dada yake Professors Sarungi. Saba-saba yeye alizaliwa na kulelewa ujombani hivyo ndiyo maana amerithi jina la ukoo wa mama. FB_IMG_1448218676759

Nilishawahi kuelezea huko nyuma undugu wangu na mzee Sarungi nimesahau ilikuwa nipost ipi  hivyo nimeshindwa kui-attach hapa. Kwa kifupi kama ulipitwa ni hivi; Professor Sarungi na baba yangu mzazi wamechangia babu mzaa baba zao. Baba zao wote ni watoto wa marehemu Chief Igogo isipokuwa bibi zao ni tofauti. Chief Igogo alikuwa na wake 19 ?? na kati yao mmoja ni bibi yake mzee Sarungi, na mwingine ni bibi yake baba yangu.

Okay, mbarikiwe wa ndugu ? Undugu ni hazina muhimu lakini tukumbuke undugu si kufanana undugu ni kufaana!!

Leave a Reply