First Lady by default! Sasa ni Mbunge wa kuteuliwa!

Malkia wetu wa nguvu anarudi tena kwenye macho ya jamii! Mama Salma Kikwete anarudi tena baada ya kuteuliwa na Rais Dr. Magufuli kuwa Mbunge wa bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania hapo jana!

Wengi tulimzoea kumuona akitumikia jamii kama First Lady lakini sasa atatumikia jamii kama Mbunge. Ile nafasi ya kwanza ya kuwa First Lady ilitokea tu (by default) kwasababu ni mke wa JK. Lakini sasa lazima atakuwa ameombwa na Rais Magufuli na amekubali kwa hiyari yake mwenyewe! Hata hivyo, nani ajuae?! yawezekana hata akapewa wizara fulani kuiongoza ambapo binafsi naamini atafanya kazi nzuri sana kwani ametuonyesha kwa vitendo alivyo kuwa First Lady! Haswa natamani apewe wizara inayo husiana na mambo ya maendeleo ya wamama na watoto!

Katika maisha kila mtu ana ndoto zake na wito wake. Watu wengine wamebahatika kuweza kutimiza ndoto zao wakiwa na umri mdogo. Lakini kuna wengine kwasababu ambazo pengine ni Mungu tu ndio ajuae ndoto zao huchelewa kutimia na wengine zisitimie kabisa! Basi si ajabu kumuona Malkia wetu wa shoka akitumikia jamii tena akiwa na cheo cha chini. Kwani hiyo ni dalili nzuri ya mtu mnyenyekevu ambaye yupo teyari kujishusha kwa faida ya taifa lake. Pia bado haja chelewa kutimiza ndoto zake ndio maana hata Hilary Clinton alikubali kufanya kazi ya kuwa Secretary of State chini ya uongozi wa Rais Baraka Obama.

Hivyo basi, tunamtakia utumishi mwema kwa kuweka uzalendo kwanza. Natumaini ile kauli mbiu yake ya “Mtoto wa mwenzio ni wako” ataiendeleza ili kuokoa vijana wa taifa hili kutoka kwenye madawa ya kulevya!

**Huko nyuma niliwahi sema hivi juu ya mama Salma Kikwete,  “Kwaheri ya kuonana mama Salma Kikwete ” **

Leave a Reply