Kwaheri ya kuonana mama Salma Kikwete!

phoca_thumb_l_salma-kikweteKwaheri mama Salma Kikwete. Asante sana mama yetu kwa kuliwakilisha vyema taifa letu na wanawake wa Kitanzania kwa ujumla. BarackObamaJakayaKikweteSep242013Umekuwa mfano bora kwa wanamama wenzio, wanawake wadogo, na mabinti zetu ndani na nje ya Tanzania. Sisi hatuna chakukulipa zaidi ya kusema asante sana mama. Kazi umefanya vizuri na sasa tunakutakia mapunziko mema. FB_IMG_1446730522248Wewe ulikuwa mama ambaye hauna makuu, hauna makeke wala mawenge. Mama mwenye staha unayejua kujishusha! Salma+Kikwete+Camilla+Prince+Charles+Visit+owBbwbefbdfl-2Tuta  ku-miss na mavazi yako ya vitenge. Uliweza uzalendo mbele ukapenda na kutukuza vya kwetu. Wewe unajitambua na kujikubali ndio maana haukuwa limbukeni. Mfano nzuri umeonyesha! 1468740_635714213159231_1778663487_n-1 Najua wewe sasa ni “kungwi” hivyo umemfunda vyema ‘mwali’ wako mama Janeth Magufuli! Tunatumaini naye atafanya vyema napengine  zaidi yako wewe. BveaAMmIQAAl0BM-1 Asante sana, na kwaheri ya kuonana tena. Ubarikiwe siku zote!

One thought on “Kwaheri ya kuonana mama Salma Kikwete!”

Leave a Reply