Nini faida za hirizi wanazo fungwa watoto?

FB_IMG_1441135967436Jamani kama kuna mtu anajua naomba kuelimishwa kuhusu hizi hirizi ambazo wanafungiwa watoto. Nimesha ona wengine wanafungiwa shingoni kama cheni na kunawanao valishwa mkononi kama Princess Lattifa (mtoto wa Diamond na Zari).  Naamini hizi huwa zinatoka kwa waganga wa kienyeji wale wanao roga watu (siyo wanao uza madawa ya kienyeji). Kama nitakuwa nimekosea basi nielimishe tafadhari. Sasa naomba kuliaza inamaana mtoto huwa anapelekwa kwa waganga na kufungiwa au zinauzwa tuu mahala fulani na watu wanaweza kununua? Na nini haswa faida zake katika ukuwaji wa mtoto.

Naomba uwelewe kuwa na heshima sana imani za watu na uhuru wa kuabudu kitu wanacho kiamini. Hivyo nataka kuelimishwa tuu na siyo kumkashifu mtu. Asante.

2 thoughts on “Nini faida za hirizi wanazo fungwa watoto?”

    1. Mie nafikiri zinafaida ambazo siye ambao hatuamini katika hirizi hatuzijui wala kuziona. Maana kama karne hii 21st bado wanafungia watoto basi kunakitu. I hope wata share nasisi tuzijue ?

Leave a Reply