HIZI KESI ZINA DHOOFISHA SANA UPINZANI- Peter Sarungi

Kuna msemo unasema “Adui mwombee njaa, atainua mikono juu hata kama ni Shujaa”

Msemo huu unatukumbusha kwamba siku zote binadamu umuombea mabaya mpinzani wake, ndivyo tulivyo umbwa na hata katika siasa ndivyo ilivyo tena ni zaidi ya kuomba mabaya na kutenda mabaya kwa mpinzani wake.

Upinzani una kabiliwa na kesi nyingi sana katika mahakama zetu. Kesi hizi zipo kwa viongozi kuanzia ngazi ya ya mwenyekiti Taifa hadi kwa wenyeviti wa vijiji mikoani. Uwepo wa kesi hizi zina athiri upinzani kwa njia tatu.

1. Ki Uchumi: Uendeshaji wa kesi una gharama kubwa mno na kwa nchi zilizoendelea, kesi ni njia moja wapo ya kufilisi au kupunguza uchumi wa mtu ama kampuni. Mfano: Mike Tyson pamoja na mambo mengine ali filisika baada ya kugharamia kesi yake ya kubaka.

2. Ki Siasa: Baada ya uendeshaji wa kesi, kinacho fuata ni hukumu. Hukumu yaweza kuwa nzuri ama mbaya kwa upinzani, inapokuwa mbaya inaleta pengo kubwa la kisiasa kwa upinzani. Mfano: Mh. Peter Lijualikali (MB Kilombero) anatumikia hukumu ya kifungo cha miezi sita jela. Hukumu hii ina dhoofisha nguvu ya siasa na hata kuleta pengo la utendaji wa mwanasiasa huyu kwa walio mchagua.

3. Ki Jamii: Inapotokea kiongozi wa kisiasa anapatwa na tuhuma, anashitakiwa na kuhukumiwa basi wanao umia kisaikolojia ni jamii yenye imani kubwa na kiongozi huyo. Mfamo Mh. Mbowe (MB Hai, KUB na M/kiti Chadema) anapopatwa na tuhuma ya kukwepa kulipa kodi au kujihusisha na Dawa, wanao umia zaidi kisaikolojia ni wakereketwa, wapenzi, mashabiki, wananachama na viongozi wa Upinzani walio chini yake.

Hizo njia tatu kwa pamoja zinaleta athari za kudhoofika kwa wanasiasa mahiri na machachari wa upinzani

#Kumbuka Dhamani sio ushindi, Tunaye kaimu judge mkuu kwa mhimili huu, Kuna wanasiasa walio nyamaza baada ya kesi. Pole G. Lema (MB Arusha) na wananchi wa Arusha kwa mateso ya kisaikolojia mliyo yapata kwa muda wote.

Leave a Reply