“SI KWAMBA NI MCHAPA KAZI TU BALI PIA NI MZURI WA MUONEKANO” Mkuu wa kaya

Peter Sarungi (The next Speaker)

 Moja ya sifa ya Mkuu wa kaya katika hotuba zake ni kupenda kutoa mifano ama utani yenye chembechembe za ukweli. Sifa kama hizi akipewa mama, mke, dada au hata bibi inaleta furaha na inajenga kujiamini kwao.

Nitumie fursa hii kumpongeza Mama Salma Kikwete (Malkia wa nguvu wa Taifa) kwa kuteuliwa kuwa mbunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Naamini sifa ulizo pewa na Mkuu zita akisi uwezo wako wa kutetea maslahi ya Taifa na wananchi wake.

Nafasi uliyopata sasa inakusogeza karibu zaidi na matatizo ya wana wa nchi lakini pia inakupa uwezo zaidi ya kuleta suluhisho ya matatizo hayo tofauti na ulivyokuwa First Lady. First Lady ni ceremonie title, ulikuwepo kwaajili ya kupamba kazi ya baba, kumshauri na kusapoti kazi zake kupitia WAMA. Uwezo wako binafsi ulifichwa ndani ya mafanikio na sifa za baba. Sasa ni zamu yako kuonesha ushujaa wako kwa nchi na hasa kwa wale wanao beza uteuzi huu, onyesha umuhimu wa fursa kwa wamama kama alivyo onesha Mama Hilary Clinton.

Nakutakia Kazi njema na utendaji mzuri katika kutumikia wananchi wa tanzania kupitia Bunge. Mama usiogope kukemea na kusema ukweli. Ni Haki yako kusema ukweli hata kama utabaki peke yako, bado ukweli huo ulio usema utaishi zaidi yako.

Asanteni.

Leave a Reply