Hongera Nancy Sumari na Jokate Mwegelo

God is able. God is able to dream bigger dreams for you, than you can ever dream for yourself. Mungu anaweza. Mungu ana uwezo wa kukunyanyua kwa namna haukuwahi kutarajia maishani mwako. #Amini #Trust #Believe #Thankful #Grateful #Blessed #HappyWednesday #HeIsAble #MIYA100Awali ya yote napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu katika kila jambo, familia, marafiki na Watanzania wote kwa ujumla. Siku zote hakuna mafanikio yaliyokosa changamoto,na ili ufikie kilele cha mafanikio hunabudi kutumia jitihada, maarifa na nguvu zaidi. Na maombi ya nguvu juu bila kusahau heshima kwa wote wakubwa na wadogo. Napenda kuwashukuru wananchi wote kwa ujumla mnaonipa support na kunipa moyo juu ya niyafanyayo. Nikiwa kama mwanamke kijana nimejitahidi kuiinua #Kidoti katika daraja la juu zaidi, ni nyinyi mnaonipa motisha na chachu ya mafanikio yangu, kwa maombi yenu na sapoti yenu kwa hakika nitazidi kusonga mbele na kuwapa hamasa vijana wengi. Wanasema katika kila jambo mshukuru Mungu. Liwe dogo au kubwa, baya au zuri maana kila kitu kina mchango katika kutengeneza wewe unayesimama leo. Nashukuru Mungu juhudi zangu zinazidi kutambulika nje ya mipaka. Sio jambo jepesi kama mwanamke na kijana kusimama katika kile unachoamini na kujitengenezea njia mahali ambapo hiyo njia haikuwepo. Naomba niseme hii ni kwa ajili ya vijana wote wa Kitanzania wanaokatishwa tamaa katika kufuata kitu tofauti na matarajio ya wengi, katika kufuata ndoto zao. Utabezwa ila usikate tamaa, kaza moyo. Maisha ni safari hakuna kukata tamaa mpaka mwisho wa maisha yako duniani. Kuna siku nitazungumzia safari ya maisha yangu kuna vitu vingi sivisemi ila siku hiyo nitavisema ili tu wewe kama kijana na Mtanzania uweze kuhamasika na safari yako katika kile unachokifanya. #BeYou #BeKidotified #MISA100 ???

Leave a Reply