Muwe na wiki njema: Mchumia juani hulia kivulini!

img-20161008-wa0000fb_img_1472436063790Mchumia juani hulia kivulini!!………. Najua kwa wenzangu wa Tanzania na East Africa au Africa kwa ujumla sasa hivi ni asubuhi siku ya JumaTatu, watu wameanza na maangaiko ya wiki pamoja na kufanya kazi! Basi naomba niwakumbushe kuwa tafuta tena kwa bidii zote lakini kiwe halali siyo vya mkato wa njia za “panya”! Najua ni ngumu sana kuchumia juani lakini siku zote matunda yake ni matamu sana!! Usiwe na tamaa kwasababu unawaona wengine wanasonga mbele kwa speed ya mwendo kasi ukadhani kuwa wewe unamatatizo, hapana! Siyo vyote ving’aavyo ni dhahabu au almasi!!……..  Usitoe wala kupokea rushwa! Rushwa ni adui wa haki! Rushwa inarudisha maendeleo ya nchi yako na maendeleo yako binafsi nyuma! Rushwa inaondoa amani! Mla rushwa ni wakuogopa kama ukoma!……….Swali la kizushi; nasikia Dr. Magufuli siku hizi wala rushwa wote anawatupia Kigoma mwisho wa reli ??? Muwe na wiki njema. Mbarikiwe sana!

Leave a Reply