Nawatakieni Mwaka Mpya mwema!

Screenshot_2015-12-07-19-41-52-1Wapendwa wasomaji wangu, ndugu, jamaa na marafiki. Napenda kuwatakieni kheri ya kuufunga mwaka 2015 na kufungua mwaka 2016. Nasema asanteni sana kwa kutembelea hii blog bila kuchoka, sina cha kuwalipa zaidi ya asante. Naomba mnisamehe wale wote niliyo wakwaza kwa namna moja ama nyingine. Sidhani kama nilikusudia kumuumiza mtu na sina huwakika kama nimemuumiza mtu yoyote! Lakini kama binadamu huwezi jua hivyo najishusha kwa kusema I am sorry! Tuzidi kupendana, tuombeane, na tutakiane mema siku zote! ……………….Mdogo wangu ? Blessing naye anawatakieni mwaka mpya mwema. Anasema yeye ni mpenzi wa hii blog hivyo siku zote anatembelea na kuwasoma hapa kwa kutumia mtandao wenye mawasiliano na Internet ya kuaminika. #Halotel ndiyo habari ya mujini na vijijini!

Nawaacheni na huu wimbo. Nimoja ya nyimbo ninazo zipenda sana sana. Yani huwa nausikiliza kwenye gari karibia kila siku!

Happy New Year wapendwa. Tukutane 2016 ???

Leave a Reply