Nijambo jema lakini linasikitisha na kuogopesha!

Miaka ya hivi karibu tumeshuhudia vijana wengi wakijiunga na vyama siasa na kua active katika shughuli za kila siku zinazo husiana na siasa na wengine hata kugombea uwongozi katika ngazi mbali mbali za uwongozi kama ubunge. Ni jambo jema sana kuona vijana wakijuhusisha na mambo yanayohusu maisha yapo pamoja na maendeleo ya inchi yao japo ukitizama kwa karibu linasikitisha na kuogopesha!

Kwanini ninasema ni lakusikitisha na kuogopesha; kwanza vijana wengi wanajiunga na siasa kwakufata mkumbo. Yani hawana ufahamu nini maana ya siasa na kwa nini wanajihusisha na siasa.  Sina huwakika ila nahisi kuwa wao wanafikiri siasa ni sare zile wanazo vaa na maandamano wanayofanya kila siku bila kujua kua siasa ndiyo inawafanya wao wawe  jinsi walivyo. Yani ninacho maanisha ni kuwa siasa ndiyo inakupangia maisha yako ya kila siku, na usalama wa inchi yako. Pili siasa imekuwa ni njia moja wapo ya kujipatia ajira, na hili tatizo si tuu kwa vijana bali hata kwa watu wengi walio ingia kwenye siasa. Hii imekuwa njia rahisi ya kujipatia mapato na si kuwa ni wazalendo kama watu wanavyo weza wafikiria.

Tukirudi kwenye point yetu, kinacho sikitisha na kuogopesha si vijana kuingia na kugombea uongozi kwenye siasa bali ni aina ya vijana wanaogombea hizo nafasi za uwongozi. Ukiwaangalia ni vijana ambao wao wenyewe hawajitambui, wala hawajielewi dhamani yao, na wala hajui ni nini wanataka katika maisha yao. Sasa hawa vijana wasio jitambua wala kujua nini wanataka katika maisha yao watawezaje kujua na kutambua nini mahitaji ya wanainchi wa Tanzania?

Hivi watu wanao wapigia debe na raia wanao wachagua wanaelewa ni jinsi gani wanaliweka taifa katika hatari kubwa sana?! Embu jaribu kutafakari, kama tukawachagua wabunge kama kumi tuu wanao toka kwenye Bongo flava, Bongo movie, na rapers wenye tabia kama za Sugu Mbilinyi unafikiri taifa litafika wapi? Niwapi vijana wa kitanzania wanataka kulipeleka taifa? Kwa manufaa ya nani? Kweli hawa wasanii wa Bongo movie na Bongo flava wataweza kujua na kupitisha budget ya inchi kweli? Hivi wataweza kutunga sheria za kulinda inchi yetu. Unajua kama hawa wabunge ndo wataamua kuwa twende vitani au la, sasa kwa kuwangalia tuu hawa wasanii je unafikiri kweli wanaweza fanya haya maamuzi ikiwa tuu wamweshindwa kufanya maamuzi kuhusu maisha yao wenyewe?!

Sikatai ni ukweli usiopingika kuwa watanzania wamechoka na mafisadi na wazee ambao wamekuwa kwenye siasa miaka nenda rudi bila kuleta mabadiliko ya kimaendeleo yoyote kwa inchi yetu, lakini pia lazima tuchunguze ni vijana wa aina gani tunawachagua kwenda kufanya maamuzi yanayo husu inchi yetu na sisi binafsi kama raia wa inchi. Bunge ni mahala patakatifu, bungeni si mahala pakwenda kuuza sura na kufanya fashion show! Bungeni si mahala pakutafuta umaharufu, bunge la Tanzania ndiyo roho au moyo wa Tanzania. Moyo ukiwa unajazwa na vyakula visivyo faa ipo siku utasimama na ukahacha kufanya kazi yani utakufa, na hapo inamaana ndiyo itakuwa kifo cha Tanzania kama inchi. Ni nani atalaumiwa? Hawa wasanii wanao jitokeza kugombea nafasi mbali mbali za uwongozi haswa ubunge ni jambo jema sana lakini linasikitisha na kuogopesha! Tafakari kwa makini na tumia haki yako ya kupiga kura vizuri!!

Leave a Reply