Hata shetani naye ni mtu!

Screenshot_2016-04-10-07-04-54-1Jana huyu mtani wangu aliandika hii “status” yake kwa Facebook kama inavyo someka hapo juu ☝. Sasa mie nilimjibu kwenye comment kama inavyosomeka hapo chini ?. Nashukuru kuna binadamu ambao nao wanaelewa kile ambacho mimi naye nakielewa na kuamini kuwa si kila mtu ni mtu kwani hata shetani naye ni mtu!

Sasa ngoja nitolee maelezo. Hata shetani naye ni mtu kama walivyo watu wengine hivyo kuwa muangalifu sana na “watu”! Tafuta kuzungukwa na watu wenye UTU ambao ndiyo wanaitwa “binadamu” lakini kama wewe unataka kuzungukwa na watu? Ndugu yangu nakupa pole sana kwani unaweza ukajikuta umezungukwa na kundi la mashetani au mapepo wewe ukidhani. ni watu!

Kuna na “watu” wenye roho za shetani ambao ukiwaona utadhani ni binadamu! Wanavaa vizuri,  wengine wana elimu nzuri, wana sura na sauti za upole mfano wa malaika, wengine ni warembo sana, wengine wapo mbele  kuwa wanataka kusaidia “watu”. Lakini kaa nao karibu wow! Utajikuta unajiuliza hivi huyu ni mtu au shetani! Kuna watu waongo mfano hakuna, kuna watu ni wataalam wa kusuka na kusamba majungu ambayo yanaweza yakafanya mtu akauliwa  (I’m a living testimony),  watu ambao wana roho mbaya hujawai ona, kuna watu ambao ni serial killers, wachonganishi, etc!

Wapendwa wasomaji wangu, kuweni waangalifu na “watu” siyo kila mtu ni binadamu! Shetani na wafuasi wake wapo hapa duniani nao ni “WATU”! Na anaweza kuwa mtu yoyote yule; ndugu, rafiki, jirani n.k 2016-04-10 07.08.04Mungu atupe uwezo wa kuwatambua hawa “watu” ili ukae nao mbali sana!

TANZIA

 

Ndugu  Wanajumuiya,

Tunasikitika kuwataarifu  juu ya mauti yaliyomkuta mwanajuiya mwenzetu hapa Houston Marehemu Henry Kiherile.  IMG-20160408-WA0022Marehemu alikumbwa na mauti na kuaga dunia jana-April/ 06/2016 usiku saa tano na nusu kwa kupigwa risasi mbili na kuporwa gari lake. Mwili wa marehemu uko chini ya uchunguzi ukisubiri kupelekwa Funeral Home.

Ndugu Wanajumuiya tutakuwa na MKUTANO kwa ajili ya huu MSIBA siku ya Ijumaa (04/08/2016 ) katika anuani hii hapa chini :

Anuani   :    8107  Meadows Pond DR

   Missouri City, TX, 77459

Tarehe   :    April /08/2016 { FRIDAY }

Muda     :    6 PM

Henry ni  Mtanzania mwenzetu hapa Houston na ana Family members hapa.  Marehemu ni mpwa wa Lucy Tenende, na pia ni mpwa wa  Mathew Mohono.

Kwa taarifa zaidi wasiliana na: 

Lennard Tenende (713) 540-6355

Lucy Tenende (832) 338-7222

Matthew Mohono (281) 804-6478

Imetolewa na : THC Spokesman

*Kwa masikitiko makubwa sana, natoa salamu zangu za rambi rambi kwa wana familia wote, ndugu, jamaa, marafiki, pamoja na Attachmentjumuiya ya Watanzania wote waishio Houston, Texas kwa msiba huu. Ni kifo cha kuhuzunisha sana! Mungu awe nanyi nyote katika kipindi hichi cha maombolezo. Apumzike katika amani ya Bwana kaka Henry….. Bwana alitoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe milele zote ?* 

Kusoma juu ya habari ya kifo cha Henry Kiherile  bonyeza hapa.

Ijumaa Kareem

FB_IMG_1460124592020Jumaa Mubarak. Sabato njema. JumaPili njema………sorround yourself with greatness ?❤❤❤

Halotel inawatakieni mapumziko mema

FB_IMG_1460123889165Nimejikuta nime miss matangazo yangu ya Halotel ? lakini lazima ni keep ahadi yangu mpaka mwezi wa tano……..Basi ngoja ni kukumbushe kuwa Halotel bado ndiyo habari ya mujini na vijijini! Nunua Halotel kwa mawasiliano yako yote kwani wana network nzuri, Internet ya uwakika kabisa, na HaloPesa kwa huduma za kifedha za haraka!

Hot shot of the day

FB_IMG_1460124700563-1Gorgeous! Kitu uzuri wa asili ‘no chemical added’, organic from Kanda ya ziwa ?? pendeza sana mrembo. Tafadhali, huyu ni mke wa mtu hivyo tazama hii picha kwa heshima zote! Ubarikiwe sana Anna.

“You will never walk alone”

You Will Never Walk Alone!

When you walk through a storm, hold your head up high

 And don’t be afraid of the dark

At the end of the storm, there’s a golden sky

And the sweet, silver song of a lark

Walk on through the wind 

Walk on through the rain

Though your dreams be tossed and blown

Walk on, walk on

With hope in your heart

And you’ll never walk alone

You’ll never walk alone

Walk on, walk on

With hope in your heart

And you’ll never walk alone

You’ll never walk alone

 

Source: one of Facebook friends

#TBT

2016-04-07 09.31.35Me, myself,  and I #TBT  #1996  #TemekeSDA

Kwenye maisha hakuna hali ya kudumu -Dina Marios

Nimejifunza kwenye haya maisha hakuna hali ya kudumu.Kufumba na kufumbua mambo yanaweza kubadilika. Kufumba na kufumbua uelekeo wako wa maisha unaweza kubadilika kwa uamuzi utakaoufanya. Uelekeo utakaochukua unaweza kukupa neema au kukupa majuto baadae. Hayo ndio maisha full of surprises.

Watu tusiowatarajia wanaweza kutokea na kututengeneza kuwa kile tunachotamani kuwa au kile tunachotaka kuwa. Hayo ndio maisha full of suprises.

Kufumba na kufumbua unaweza kujikuta kwenye hali mbaya sana kama binadamu. Kuna kaka nilikutana nae kama mara mbili hivi mara ya tatu naambiwa yule kaka amepata matatizo ya akili amechanganyikiwa ni kufumba na kufumbua.

Kufumba na kufumbua watu uliokuwa unahisi unawajua sanaa kutokana na ukaribu mliokuwa nao utagundua kumbe ulikuwa huwajui hata chembe… ndio maisha full of surprises.

Hayo ndio maisha kufumba na kufumbua kila kitu kinaweza kubadilika hali kuwa nzuri au mbaya…… good morning! FB_IMG_1460010305974

Nani anastahili kula matunda?

Nataka wewe leo uwe hakimu (Judge), tena si wa mahakama ndogo. Hapa, wewe leo ni jaji wa mahakama ya rufaa. Na unatakiwa kufanya maamuzi juu ya kesi hii na maamuzi yako ni ya mwisho hakuna wakupinga. Nakuletea hawa watu wawili ambao wote wanataka haki itendeke bila kumuonea mtu yoyote kwani “mnyonge mnyongeni haki yake mpeni”!  c870acd11ac7f72e26d3e44fe6221a1e17fe5673e3e9db547ed6ee9a777e8d5b_1Mtu wa kwanza tutampa jina la Sikudhani. Na mtu wa pili tutampa jina la Sikujua. Sasa Sikudhani na Sikujua wao wenyewe kwa hiyari yao wakaamua kununua shamba pamoja. Wote walitoa kiasi sawa cha fedha kilichohitajika kununua shamba. Wakagawana katika ili kila mtu alime sawa bila ‘kumyonya’ mwenzake. Sikujua hakuwa na pesa za ziada hivyo alitegemea wangesaidiana na rafiki yake ili waweze kutafuta pesa pamoja kwa kuuza mazao watakayo lima. Sasa katika harakati za kuanza kuandaa shamba ili wapande mazao ilikuwa kama ifuatavyo -:

SIKUDHANI: Sikudhani yeye hakudhania kuwa lile shamba lina ubora na virutubisho vyoyote ambavyo vingewezesha kuzaa matunda au mazao. Hakuona kama kuna umuhimu wa kutumia nguvu na pesa zake kuwekeza kwenye hilo shamba kwani halina thamani hiyo. Hakudhania kuwa kuchukua pesa zake na kutafuta watu wa kulimaa na kuongeza mbole kwenye hilo shamba ni wazo la busara. Hivyo aliachana na hilo shamba bila kujali chochote. Hata pale Sikujua alipo msihi kuwa jaribu hata mara moja kabla ya kusema haifai, lakini Sikudhani alikataa kata kata tena kwa dharau na dhihaka nyingi; “shamba lenyewe lipo sehemu kavu. Hakuna hata maji pamekauka kama jangwani nitapata nini hapo! Angalia lipo kwenye muinuko mvua ikija mazao yote yatachukuliwa na mvua. Sina shida nao, hela ya kununua vyakula ninayo mpaka siku nakufa.”!

SIKUJUA: Yeye alikuwa na imani kuwa anaweza kupata kitu katika shamba lile japo hakujua ni kwa kiasi gani. Alijua kuwa linadhamani yakutosha kuwekeza nguvu zake hapo kwani ametumia pesa yake kulinunua. Sikujua yeye alikuwa mtu mwenye hali duni hivyo shamba ndiyo ilikuwa tuamini lake!

Basi, Sikujua alianza kuandaa shamba kwa jembe lake dogo la mkono. Kila siku anaamka hasubuhi na mapema, anaandaa chakula na maji ya kunywa anaenda shambani kuanzia saa kumi na moja (5am) asubuhi mpaka saa kumi na moja (5pm) jioni. Akatoa magugu yote, upande wake na upande wa Sikudhani. Kwasababu alikuwa hana pesa, hivyo akamwambia Sikudhani kuwa; nimetoa magugu na nyasi zote shambani  naomba unisaidie hela kidogo ya kununua mbegu ili nipande mazao. Nitapanda hata upande wako. Kwa kuzuiya mmonyoko ningependa kuanza kwa kupanda miti ya maembe pembezoni mwa shamba kwanza. Sikudhani akamjibu kwa dhiaka; “nipishe huko wewe mjinga, sina pesa za kupoteza mimi.”! Sikujua kwa upole na unyonge mwingi akaondoka huku akisema “asante Sikudhani.” mangosmtree2-1Sikujua akatafuta pesa za kununua mbegu kutoka kwa mama yake mzazi akampatia. Japo mama yake alikuwa na shida nyingi lakini hakuweza kumtupa mwanae kwani naye kama ilivyo kuwa kwa Sikujua aliamini kuwa mwanaye atapata kitu kwenye lile shamba na hato hitajika kumsaidia tena. Sikujua alimshukuru sana mama yake si tu kwa msaada wa pesa aliyompatia bali kwa kumsaidia kujihifadhi pamoja na wanawe kwenye kibanda alichokuwa anaishi.

unnamedSikujua akapanda mbegu 20 za mti wa maembe kuzunguka eneo lake tu. Hakupanda hata mbegu moja kwenye eneo la Sikudhani! Kwasababu pale ni pakavu sana basi ilimbidi aende mbali kuchota maji ya kumwagilia ili mbegu zake zisikauke. Sikujua alitembea peku peku kwani alikuwa hana uwezo wa kununua viatu. Pesa alizokuanazo kidogo alinunua mbolea akamwagia kwenye mbegu. Mvua ikaanza kunyesha.

Kwakuwa mvua ilikuwa inanyesha kubwa akahofia mbegu zake kuchukuliwa na maji kwani pale kulikuwa na mteremko. Basi akaamua kwenda kusomba mawe ili aweke pembezoni mwa shamba kuzuiya madhara ya mvua kwa mbegu zake. wakati anarudi kutoka kutafuta mawe akiwa njiani mvua ikaanza kunyesha. Pale hapakuwa na sehemu ya kujihifadhi hivyo ilimbidi aendelee na safari. Aliloana sana.

Akafika shambani na kuweka mawe huku mvua ikiendelea kunyesha lakini hakuacha kwani mbegu zile zilikuwa muhimu sana kwake kuliko kuloana na mvua haswa akikumbuka kuwa pesa alizo nunulia mbegu amepewa na mama yake mzazi ambaye ni mzee na masikini kama yeye! Mvua ilikuwa ni kubwa sana, mbegu 19 kati ya ishirini zilisombwa na maji. Ikabakia moja tu ambayo ilikuwa katikati ambapo ndipo panagawa mpaka wa eneo lake na eneo la Sikudhani. Sikujua hakukata tamaa. Akalinda mbegu hiyo moja. Mti ukawa mkubwa. Sikudhani alipo ona mti unakuwa mkubwa kama ilivyo kawaida yake na dharau nyingi. Akawa anasema “huo wala hauto toa maembe. Huo mti ni tasa hauzai unajisumbua tu!”  

Screenshot_2016-03-31-00-57-12-1Baada ya muda kidogo, mti ule ukaanza kuota maembe. Ukatoa maembe makubwa sana tena maembe “dodo”! Maembe yalikuwa mengi sana na matawi yalikuwa marefu hivyo yalipo anguka chini mengine yaliangukia upande wa Sikudhani! Sikujua akayakusanya maembe akapeleka sokoni akauza akapata pesa za kujikimu.  Mti unaendelea kutoa maembe na Sikujua anafurahia faida anayo pata kutokanana jasho lake. Ameweza kununua ng’ombe anapata mbolea na kuuza maziwa pia anatumia ng’ombe kulimia. Sikujua sasa amejenga na nyumba anaishi na wanawe! IMG_20160406_155652Bahati mbaya mama yake mzazi Sikujua aliugua na kufariki kabla ya mti kuanza kutoa matunda. Alibahatika kuuona ulivyo kuwa mkubwa lakini hakuona matunda yalivyo toka. Hii inamsikitisha sana Sikujua na baadhi ya ndugu zake kwani wanatamani sana mama yao angeona na kuonja matunda angalau kidogo. Mungu si Athumani, Sikujua amebahatika kupata wajukuu. Nao wanapenda sana maembe. Wanafurahiya kunywa maji ya maembe kila siku!  Screenshot_2016-04-06-15-44-08-1Chakushangaza, Sikudhani sasa naye ananyemelea maembe ya Sikujua! Anasema yale yanayo angukia upande wake ni yakwake! Sikujua hataki hata kusikia habari hiyo! Sasa hivi Sikudhani anaumwa anahitaji hela za matibabu matokeo yake anataka achukuwe maembe aende kuuza ili apate pesa za matibabu. Lakini Sikujua hataki kusikia habari hiyo kwani bado anakumbuka matusi, dharau, na dhihaka alizo mfanyia!  Gold+Mangoes+4.JPG-1Siku moja, Sikudhani akamwambia Sikujua kwa sauti ya ukali kuwa; hata kama hilo shamba tuligawana katikati kwaajili ya kulima, lakini hati miliki ya shamba inaonyesha wote wawili ni wamiliki wa hilo shamba. Hivyo nayeye anastahili kupata maembe yaliyopo shambani hapo! Sikujua amekataa na sasa amekimbilia mahakamani kupata haki yake!Screenshot_2016-03-29-08-25-27-1Ni nani haswa anastahili kula matunda kati ya Sikudhani na Sikujua? Na kuna ubaya wowote Sikujua kumkatalia Sikudhani kuchukua maembe? Tafakari kwa kina toa hukumu ya haki na sahii!

Tafadhali: picha zilizo tumika hazina huusiano wa moja kwa moja na hadithi hii.

 

Hot shot of the day

FB_IMG_1459874496611Mr and Mrs Baraka Kissa ndani ya Rock city! Nafikiri hapa ni Tilapia Hotel kama sijakosea. Enjoy your vacation wapendwa ❤❤❤ FB_IMG_1459874517218

Kutoka Facebook

FB_IMG_1459973264324-1Nimependa sana hii picha ya Mwajuma na wanawe. Hawa wanaishi kwa Malkia Elizabeth. Mbarikiwe sana wapendwa

“Live as you before you live as we”-Devon Franklin

Here are some of the experiences that are worth sampling while you practicing #TheWait – what would you add? FB_IMG_1459908764778

Autism is not a disease, it’s a condition!

FB_IMG_1459863091911Kwanza naomba nianze kwa kumpongeza sana wifi yangu Veneranda Obure na binamu yangu Dr. Joseph Obure pamoja na wazazi wote wenye watoto wanao sumbuliwa na Autism inchini Tanzania kwa ujasiri wao wa kuweza kutoka mbele ya public na kueleza dunia kuwa watoto wao wanasumbuliwa na ugonjwa ujulikana kama Autism. Sio wazazi wengi wanaweza kujitokeza hadharani namna hii kwasababu ya kuogopa kauli za watu na stigma zao zilizo jaa ufinyu wa fikra!! Hongereni sana.

Nakumbuka mara ya mwisho nilipokuwa nyumbani. Rafiki / jirani yetu wa zamani alinisihi sana kuwa nisiondoke bila kumuona. Basi nami nilifanikiwa kwenda kuwasalimia. Katika kuongea ndipo akaamua ku-share nasi (nilikuwa na mdogo wangu Magreth) kuwa kwa muda mrefu ameangaika na mwanae na alipo mpeleka Nairobi kwa uchunguzi zaidi, doctor akamwambia kuwa mtoto wako ni autistic! Yani kwa Africa huu ugonjwa ndiyo sasa hivi wanaanza kuelewa tofauti na nchi zilizo endelea. Hivyo doctor akikwambia kitu kama hicho kwakweli kwa mzazi inakuwa ngumu sana kuelewa na hujui jinsi gani uchukulie. Hivyo nikitu ambacho rafiki yangu huyu kimemuadhiri sana. Na matatizo yanaongezeka zaidi haswa pale mzazi mmoja anapo kuwa hatoi ushirikiano katika kumuangalia mtoto.

Naomba Mungu ampe nguvu huyu rafiki yangu ili siku moja naye awe jasiri zaidi ya alivyo sasa, aweze kutoka mbele za watu na kushiriki na wazazi wenzie ambao wana watoto wanao sumbuliwa na Autism.                                            FB_IMG_1459863073585What is Autism!

FB_IMG_1459863122667Kuna huyu mwana mama ajulikanaye kama Holly Robinson Peete yeye ni mmoja wa wamama ambao watoto wao wana  sumbuliwa na Autism. Kwakweli napenda sana jinsi wanavyo handle hii situation ampaka imemsaidia sana ukuwaji wa mtoto wao tofauti kabisa na doctors walivyo sema. Na kitu cha kwanza wanasema ni wazazi kukubaliana na hali halisi. Halafu kuweza kuwa wazi kwa mtoto toka akiwa mdogo. (Tazama baadhi ya video ?)  

FB_IMG_1459863103016Mungu akinijalia uzima mwakani nitashiriki nanyi katika movement hii. I will walk for my darling nephew, mtoto wa rafiki yangu, na kwaajili ya watoto wengine wote wanao sumbuliwa na Autism hapa duniani. Mungu awape mwangaza doctors wanaofanya uchunguzi juu ya ugonjwa huu waweze kupata tiba haraka ?

Hot shot of the day

Screenshot_2016-04-05-11-47-37-1

Natural Hair Movement

Screenshot_2016-04-05-10-45-51-1June 2015, Bethel and I in Kalamazoo, Michigan. Bethel is rocking her own natural hair ? Screenshot_2016-04-05-10-16-49-1I am very proud of you all young ladies! Keep up the good work, and let us all embrace the all authentic us!! #NaturalHairMovement

Nunua nguo kwa bei nafuu!

Screenshot_2016-04-05-09-04-09-1Wapendwa, naomba mtembelee Facebook na Instagram ya Zawadi Kakoschke upate kujichagulia nguo nzuri sana kwa bei nafuu. Ni nguo ambazo ni zake mwenyewe lakini zipo kwenye hali nzuri kabisa kwani hazijavaliwa sana. Muungishe mkono kwani 50% ya mauzo I nakwenda kwenye kutoa msaada ?   Screenshot_2016-04-05-09-03-56-1

Get your ticket!

IT’S OFFICIAL THE MOST ELECTRIFYING SHOW TO HIT THE EAST COAST FEAT. AFRICA’S ARTIST OF THE YEAR -DIAMOND PLATNUMZ LIVE CONCERT IN WASHINGTON DC THIS MEMORIAL WEEKEND SUNDAY MAY 29 @ COCO CABANA CLUB ……… THIS IS THE BIGGEST SHOW TO EVER HIT THE DMV, TICKET LEVELS OUT NOW ? WWW.DIAMONDDC.EVENTBRITE.COM

#AfricasArtistOfTheYear #MTVAwardWinner#BETNominee #AfrimmaWinner #AEAU.S.AWinner#ChannelOWinner #KilimanjaroAwardsWinner #ThisIsIt

FB_IMG_1459824532292

Birthday girl night-out with her friends

2016-04-04 17.47.14Someone was feelin’ #22! Get together and had fun with her friends, Kalamazoo, Michigan………Enjoy the pictures IMG-20160404-WA00152016-04-04 17.49.22IMG-20160404-WA0012IMG-20160404-WA0011IMG-20160404-WA0010IMG-20160404-WA0009IMG-20160404-WA0009-1IMG-20160404-WA0008IMG-20160404-WA0008IMG-20160404-WA0007IMG-20160404-WA0006IMG-20160404-WA0005IMG-20160404-WA0004IMG-20160404-WA0003IMG-20160404-WA0002

Cyber crime law!

Screenshot_2016-04-04-10-55-42-1FB_IMG_1459785347759

Are you a magician?

Screenshot_2016-04-04-11-00-41-1Huu ujumbe toka kwa Mombobied umenichekesha sana nikaona ni share nanyi ?? kuna kitu cha kujifunza!……… swali are you a magician? ??? Lakini watu wengi ambao tuna hela ya ‘kuunga unga’ ndio huwa tuna matatizo kama haya!! Haya sasa tujifunze na tubadilike!

Blog