Shukuru kwa ulicho nacho sasa ndipo utabarikiwa zaidi!

db2a5e2578ab6f5d636489ad43de6824FB_IMG_1472436063790Jifunze kushukuru kwa ulicho nacho kwanza ndipo utabarikiwa zaidi! Sasa kuna watu ambao hata kile kidogo walicho nacho hawalidhiki kutwa kujenga chuki na wengine bila sababu za msingi! Hawa watu wasio ridhika ndio unakuta hata awe na pesa na mali kiasi gani lakini HANA AMANI NDANI YA ROHO YAKE!! Yani akikuta hata watu wasio na uwezo kifedha na mali (masikini) wanajichekea na kufurahia maisha kwake ni tatizo kubwa! Kwani anaumia na kuchukizwa kuona masiki anafurahia maisha kana kwamba ni mtu tajiri sana!! Siri ni moja tu……….!! Huyo masiki unaye muona ni masikini wa pesa na mali tu lakini Mungu kampa amani tele moyoni kwa kuwa kashukuru kuwa ni sawa kutokuwa na vyote. Hivyo kama ni mtu wa kujishughulisha na kupigania maisha bora zaidi ya aliyokuwa nayo sasa basi ipo siku Mungu atamwona na kumbariki zaidi! Haina aja ya kuchukia mtu kwasababu anafuraha moyoni mwake! Hakuna sababu ya kumchukia mtu Kwasababu ana wazazi wake ambao wanampenda, hakuna haja ya kuchukoa mtu Kwasababu kajaliwa watoto na wewe hauna! E t c ………… Shukuru kwa ulicho nacho sasa ndipo utabarikiwa zaidi!

Leave a Reply