Tuwapende na kuwaheshimu walimu wetu

FB_IMG_1441688921784Kila mtu hapa dunia amejifunza  kitu fulani kwa maana ya kuwa hakuna aliyezaliwa akijua kituchochote bali ni kwakujifunza. Mfumo ya kujifunza ipo ya aina mbili formal  (mfumo rasmi) na informal  (mfumo usio rasmi). Haijalishi ni mfumo gani umetumia kujifunza kwani yote lengo lake ni kutoa elimu. Na wale watu wanao tumika kutoa elimu wanaitwa walimu kwasababu wanakuelimisha. FB_IMG_1442328100723-1

Labda nifafanue kidogo kwa wale ambao watajiuliza tofauti ya mfumo rasmi na mfumo usio rasmi. Mfumo rasmi wa kujifunza ni kujifunza kitu au kupata elimu ya kitu fulani kupitia mlolongo wa ngazi na njia tofauti ambazo zimeainishwa kulingana na mfumo wa elimu husika kutoka katika mamlaka ya elimu husika.  Na elimu ya mfumo usio rasmi ni kujifunza vitu au kupata elimu kwa njia ambayo aitambuliwi kulingana na mamlaka husika. Kwa mfano mtu anaweza kua mpishi mzuri kwa utundu wake au kufundishwa na bibi yake, mtu wa hivi atakuwa ameelimika katika mapishi lakini sikuwa amekwenda shule ya mapishi. Mtu kama huyu anaweza akafundisha watu mapishi yake lakini hawezi kufundisha watu juu ya chakula bora kwani kuna elimu furani kuhusu vyakula ambayo hana japo anajua kupika. FB_IMG_1442328082221

Turudi kwenye mada yetu. Jamii haswa za Kiafrika zimekuwa na tabia ya kutokuheshimu walimu bila kujua kuwa walimu ni moja ya nguzo muhimu sana katika jamii. Binafsi nafikiri walimu ni nguzo ya pili ukitoa familia  (wazazi) ambayo nafikiri ni nguzo ya kwanza muhimu katika jamii yoyote ile. Walimu wanachukua nafasi ya wazazi wetu pale tunapokuwa mashuleni kwani hawa hutufunza maadili na maarifa muhimu ya jinsi ya kukabiliana na maisha. Walimu si tuu wanatufunza kuandika bali tabia zao na mienendo yao inachangia sana katika ukuwaji wa tabia zetu na maendeleo ya nchi.

Pichani ni mimi na mdogo wangu pamoja na Assistant Director wa Kowak Girls Secondary school. Hapo ni 2013 tulienda kutembelea walimu wetu. Mimi na mdogo wangu wote tuliaoma Kowak kwa wakati tofauti.
Pichani ni mimi na mdogo wangu pamoja na Assistant Director wa Kowak Girls Secondary school. Hapo ni 2013 tulienda kutembelea walimu wetu. Mimi na mdogo wangu wote tulisoma Kowak kwa wakati tofauti.

Yatupasa kuwapenda na  kuwaheshimu  sana walimu wetu. Tuwaonyeshe umuhimu wao na thamani yao kwa faida ya maendeleo ya taifa letu.

Hapa ni sisi pamoja na Director / Headmistress wa shule. Huyu ni tofauti na Headmistress wa wakati wetu. Sisi tulikuwa na Sister Magdalena toka U.S.A
Hapa ni sisi pamoja na Director / Headmistress wa shule. Huyu ni tofauti na Headmistress wa wakati wetu. Sisi tulikuwa na Sister Magdalena toka U.S.A
Hapa tupo na baadhi ya walimu wa Kowak. Mdogo wangu aliye vaa top nyeusi yeye hakusoma Kowak bali alitusindikiza.
Hapa tupo na baadhi ya walimu wa Kowak. Mdogo wangu aliyevaa top nyeusi yeye hakusoma Kowak bali alitusindikiza.

Tupatapo nafasi si vibaya kuwajulia hali zao na kuwashukuru kwa mchango katika maisha yetu binafsi.

Hapa ni mdogo wangu na mwalimu wa Chemistry wa Kowak. Amesha funds have hapo kwa zaidi ya miaka 20. Ni mmoja ya walimu wa kwanza kabisa waliofundisha hapo tangu siku ya kwanza. An aitwa Mr. Mwita.
Hapa ni mdogo wangu na mwalimu wa Chemistry wa Kowak. Ameshafundisha hapo kwa zaidi ya miaka 20. Ni mmoja ya walimu wa kwanza kabisa waliofundisha hapo tangu siku ya kwanza. Anaitwa Mr. Mwita.

Kufundisha ni karama si kila mtu amezaliwa nayo. Japo siku hizi techology inafanya kila mtu aweze kufundisha kwa njia moja ama nyingine.  Kwani unaweza jifunza kwa kusoma status ya mtu au kwa kuangalia maisha ya watu fulani au familia kwa kutumia television au social media. FB_IMG_1441688921784Napenda kumpongeza sana schoolmate wangu toka Kowak Girls kwa kuamua kutoa mchango wake katika maendeleo ya taifa letu kwa njia ya elimu. Wanasema uwalimu ni wito, kwani ni kazi ngumu sana kumuelimisha mtu haswa watoto. Uvumilivu na busara ya hali ya juu inahitajika sana. Ubarikiwe sana Furaha.

Leave a Reply