WALEMAVU WALIOPATA FURSA WAMEJISAHAU SANA-Peter Sarungi

Peter Sarungi (kushoto), Spika wa Bunge ndugu Ndugai pamoja na viongozi wengine wa siasa,
Peter Sarungi (kushoto), Spika wa Bunge ndugu Ndugai pamoja na viongozi wengine wa siasa,

Kuna msemo wa wahenga unasema ALIYESHIBA HAMKUMBUKI MWENYE NJA. Haya maneno nilidhani yanatumika kwa watu nisio wajua tu kumbe hata watu ninao wajua na ambao tena wapo kwenye jamii nyonge ya watu wenye ulemavu. Watu wenye ulemavu sasa wamefikia Milion 4, jamii hii bado imeendelea kukumbwa na umaskini mkubwa unao sababishwa na ugumu wa mazingira wanayokutana nayo katika kutafuta maisha bora. Watu wenye ulemavu wamelia sana kuhusu changamoti zao lakini sauti zao bado hazisikiki katika vyombo vya maamuzi na mipango ya nchi, hii inatokana na uchache wa watu wenye ulemavu waliopata fursa kushindwa kutumia fursa zao katika kutetea na kushawishi vyombo vya maamuzi na vyombo vinavyotunga sera, sheria na mipango kukumbuka uwepo wa wa watu wenye ulemavu ili kusaidia utekelezaji wa sera na sheria zinazo toa fursa kwa watu wenye ulemavu. Ukweli ni kwamba ni walemavu wachache sana walioweza kupata fursa za uchumi, fursa za siasa na hata fursa za kijamii, Lakini hawa wenzetu wengi wamekuwa mabalozi wasiojali maslahi ya kundi hili na hata kufikia kujiondoa kiroho katika kundi hili ingawa ki mwili bado wana hesabika ni watu wenye ulemavu.fb_img_1480102785902

Kwa bahati mbaya jamii imetumia ulemavu wetu kama alama ya utambulisho (public figure) kiasi kwamba jamii inakutambua kwa ulemavu wako na si vingine kisha sifa zingine zinafuata na mara nyingi sifa mbaya za watu wenye ulemavu zimekuwa zikivuma kuliko sifa nzuri za jamii hii. Hili ni tatizo linalozaa utengano kwa jamii ya watu wenye ulemavu maana hawa wanaopata fursa kwa mgongo wa kundi hili wamejisahau na kujikuta wanapigania maslahi yao na matumbo yao bila kujali uwepo wa jamii ambayo imesababisha wao kupata fursa. Wenzetu badala ya kutuunganisha katika fursa, wao wameendelea kula dili na wasio husika. Badala ya kupaza sauti ya ushawishi na utetezi, wao wameendelea kukaa kimya na kuridhika kwa vinono wanavyopata. Badala ya kuanzisha miradi ya kuwezesha jamii hii wao wana anzisha miradi ya kitapeli katika jamii, wameshindwa kushawishi utekelezaji wa sera za walemavu ingawaje kila siku wapo angani kwenda mataifa ya wenzetu waliopiga hatua juu ya utekelezaji wa sheria na sera za watu wenye ulemavu, Wameshindwa kushawishi kuanzishwa kwa jumuiya ya walemavu katika vyama vyao vya siasa ingawa wao wamepata fursa kupitia jumuiya ya wanawake, wameshindwa kushawishi utekelezaji wa sheria no.9 ingawaje wamepewa utawala katika sheria na wizara ndani ya ofisi ya waziri mkuu, wamegeuza dhamana kuwa msaada, wamegeuza msaada kuwa mtaji na wametumia mtaji wa unyonge wa walemavu kuwa fursa kwao na familia zao

Peter Sarungi (Next Speaker-Baba Pilato)
Peter Sarungi (Next Speaker-Baba Pilato)

#Mytake
Wewe uliyepata fursa za uchumi, siasa na utawala kupitia walemavu, jiulize, Umeifanyia nini kundi hili linaloteseka na kunyanyasika kila siku wakati linakutegemea wewe kushawishi na kutetea mabadiliko yao? Ujue Mungu anakuona vizuri sana. Usijisahau ukadhani unaishi bila ulemavu na hata ukaukataa kwa maneno na matendo, bado utaendelea kuwa kwenye kundi hili maana hakunaga uponyaji kwa uumbaji wa Mungu labda kwa usanii na maigizo.fb_img_1480102909327

UKIMYA WA HAWA NDUGU ZETU UNAUMIZA NA KUKERA KULIKO HATA KELELE ZA WAPINZANI WETU. Badilikeni..

Asanteni

**Baadhi ya maoni ya watu**screenshot_2016-11-25-13-40-52-1-1 screenshot_2016-11-25-13-40-33-1 screenshot_2016-11-25-13-41-16-1

Leave a Reply