TAFAKURI YA LEO JUU YA WABUNGE WA CCM.- Peter Sarungi

Peter Sarungi (The next Speaker)

Tabia ya wana siasa kabla ya kuwa watawala ni kama tabia za wachumba ambao bado hawajafunga ndoa. Tabia yao kuu ni kuhaidiana mazuri, kusifiana, kuelekezana kwa lugha ya kuvutia, kutiana moyo, kuoneshaana upendo wa agape lakini pia kuna tabia moja mbaya ya walioyo nayo ya kuficha udhaifu wao na mabaya yao.

Kila inapoitwa leo, napata fursa ya kujua tabia za mkuu wa nchi kupitia kauli zake na matendo yake. Niliwahi kukiri hapo mwanzo kwa kusema kuwa Mkuu wa kaya anasimamia vizuri kauli na matendo yake wakati wa kampeni nikidhani ataendelea kutawala kupitia kauli zake za kusisitiza umoja wa nchi. Nahisi ni mihemuko ya muda iliyo niathiri.

Pamoja na changamoto hizo bado maisha na siasa zitaendelea na ni lazima tuendelee kuwaoma wabunge hasa wa CCM ambao ni 75% kusimamia kwa kuikosoa, kuisema na hata kuipongeza serikali wanapo kuwa bungeni maana hiyo ndiyo kazi tuliyo watuma. Pamoja na mtikisiko huu ulio wapata wabunge kutoka kwa Mkuu wa kaya kama ilivyo ripotiwa na gazeti la mwananchi bado mtaendelea kuwa wabunge mlio pewa dhamana na wananchi ya kuwa wakilisha bungeni katika kuisimamia serikali.

Tusijenge Taifa la chuki na uadui unao tokana na siasa, tuki ruhusu hilo basi hatutokuwa salama maana ukweli ni kwamba chuki na uadui havina mipaka, nikikuchukia kwenye siasa usidhani nitakupenda uraiani. Hiyo ni mbegu mbaya itakayo tafuna jamii yetu.

Tujitahidi kujenga jamii ya kuvumiliana, kushauriana, inayo heshimu fikra tofauti na inayoweza kuwa karibu hata kama watakubali kutokukubaliana.

Mungu tubariki huko tuendako.

Leave a Reply