ASANTE MH. JPM KWA UKWELI NA UWAZI-Peter Sarungi

Maisha ya binadamu ni mafupi sana ukilinganisha na mipango yake, hivyo kuishi kwa binadamu kunahitaji tyming kwa kila jambo. Hivyo Ukweli na Uwazi ni nguzo kuu ya maisha yetu ya kila siku.c1Kumekuwa na gumzo kubwa katika mitandao ya jamii kuhusu kauli ya Mh. JPM juu ya kutambua wake wa Marehemu Dr. Massaburi, wengine wakimshangaa na kumlaumu JPM na wengine wakimsifu kwa kusema ukweli uliofichwa na msemaji wa familia.

Binafsi nampongeza sana Mh. JPM kwa kuondoa huo Ukakasi katika jamii nyingi za watanzania, nimemuelewa sana JPM na kauli yake ya Ukweli itasaidia wajane na watoto wa viongozi wanaokuwa wanatangulia mbele za haki kama Massaburic5Ukweli ni kwamba Massaburi alikuwa ni kiongozi wa kitaifa lakini pia alikuwa ni mtu anayetokea katika jamii ya kabila la LUO. kabila lenye tamaduni na desturi mbalimbali ikiwemo ya kuwa na wake zaidi ya mmoja. Kwetu Ujaluoni kuna sababu za kuwa na wake wengi, moja ya sababu ni kuendeleza Ukoo. Naamini Dr.Masaburi alikuwa na ndoto ya kuendeleza na kupanua Ukoo wake utakao beba jina Massaburi, na hili amefanikiwa ila sijui amefanikiwa kwa kiwango gani alichokuwa anataka. Na amefanikiwa kwa sababu ya kuwa na wake wengi, maana huwezi kuwa na watoto 20 kwa mke mmoja ukiwa na miaka 56 hadi mauti yanapo kufika. Na kama ukilazimisha watoto 20 watoke kwa mama mke mmoja tena kwa kipindi cha miaka 30 ya ndoa basi huo utakuwa ni Unyanyasaji wa wanawake ambao WALUO wengi hatupendi unyanyasaji huo. Sisi WALUO tunajua Marehemu alikuwa na wake watano ambao alifanikiwa kupata nao watoto na wote wanatambulika kwa mila na desturi zetu. c2Nadhani msemaji wa Familia alikengeuka kutoka na haya mambo ya protocal za serikali na chama pamoja na kuiga tamaduni za magharibi. Asingekuwa ni kiongozi wa kitaifa basi WALUO tungefuata taratibu zetu zote za LUO katika Mazishi yetu, tumeheshimu serikali na chama.

#Mytake tusipende kuiga kila mtindo wa maisha kutoka Magharibi hata na sisi tuna mitindo ya maisha iliyotulea toka enzi na enzi za mababu zetu na inatufaa kulingana na mazingira yetu ya kiafrika. Afrika nayo ina imani, desturi na mila zetu tusipotezwe na itifaki za serikali na vyama tukajikuta tinasema Uongo na kuficha Ukweli.

Peter Sarungi akiweka signature kwenye msiba wa Dr. Didas Massaburi
Peter Sarungi akiweka signature kwenye msiba wa Dr. Didas Massaburi

Asanteni sana.

fb_img_1472436063790Asante kaka yangu kwa kuongea ukweli…… Hapa Mh. JPM aliongea kama rafiki wa karibu wa marehemu. Pia kutokana na mambo ambayo yaliyo jitokeza ambapo kama Rais asingetumia sauti yake (his power) kusema hadharani basi kuna uwezekano mkubwa wa baadhi ya wake na watoto kunyimwa haki yao ya mirathi haswa mke mkubwa ambaye she has been the wheel ya maendeleo ya Dr. Massaburi kiuchumi!! Asante Rais kwa kusema ukweli?

Leave a Reply