Category Archives: Best family moment of the year

Ubatizo wa mzee O.O Igogo.

Jumapili ya tarehe 06/18/2023, mida ya 12:30 asubuhi (masaa ya AfricaMashariki). Mchungaji Aketch wa kanisa la Menonite lililopo Dar es salaam, Tanzania,  jimbo la Segerea; alifanya ubatizo wa kuzaliwa upya kwa njia ya maji mengi kwenye bwawa la Golden Tulip hotel, Oysterbay. Miongoni mwa  waumini wapya hao katika Bwana, alikuwemo Mzee Otieno Olung’a Igogo ambaye ni baba yangu mzazi.


Wahitimu wa darasa la ubatizo wakielekea kwenye bwawa kwa furahq teyari kuzaliwa upya.

Juu ni Mzee O.O Igogo akibatwizwa kwa maji mengi. Hongera sana kwake, Mwenyezi Mungu azidi tembea naye kwenye safari hii ya kiroho.

Mchungaji Aketch pamoja na mama Mchungaji (mwenye nguo nyekundu) wakiwa na mtoto aliyezaliwa upya siku ya leo mzee O.O Igogo na mama Igogo.

Baadhi ya wanafamilia ya mzee O.O Igogo kutoka Segerea siku ya jana jioni waliungana na wanafamilia ya mzee O.O Igogo ya Kibada, wakapata chakula cha jioni pamoja, wakapumzika, na leo asubuhi waliamka mapema sana kwaajili ya kumsindikiza baba /Babu yao kipenzi kwenye safari yake mpya ya kiroho ambapo atabatizwa kwa maji mengi. …. Sifa na utukufu vyote twamrudishia yeye aliye umba Mbingu na nchi. Amen.

My 2017 best family moment: The LB family

Huko nyuma  nilishawahi kusema kuwa hii picha imekosha moyo wangu, soma ?? (HiziPichaZimenikosha) na mpaka sasa bado zinanikosha. One of the best family moment of the year kwa hii blog! Ukweli hata kama familia mnapendana kiasi gani lakini kama hamshirikiani katika maswala ya kujiinua kiuchumi, maendeleo, na kiroho basi upendo wenu ni BATILI! Yani ni upendo wa "kichina" kwakweli! Hii family ni mfano mzuri sana katika kitu kinaitwa family unite and family love! Sijasema ni PERFECT! Nope! Hakuna hapa duniani familia ambayo imekamilika! Kila familia ina matatizo yake, lakini kama kuna upendo wa kweli basi kila kitu kitaonekana sahii!  Basi, kwa maana hiyo familia ya mwanamitindo wa kimataifa Linda Bezuidenhout nasema imeshinda nafasi hii is 2017 best family moment! Hapa ilikuwa ni ufunguzi wa duka la nguo za LB! Yani kama vile mbavyo mnaonaga LV, Zara, Nine West n.k wana maduka yao maalum basi ndivyo ilivyo kwa brand ya nguo za LB!