Category Archives: Baptism

Ubatizo wa mzee O.O Igogo.

Jumapili ya tarehe 06/18/2023, mida ya 12:30 asubuhi (masaa ya AfricaMashariki). Mchungaji Aketch wa kanisa la Menonite lililopo Dar es salaam, Tanzania,  jimbo la Segerea; alifanya ubatizo wa kuzaliwa upya kwa njia ya maji mengi kwenye bwawa la Golden Tulip hotel, Oysterbay. Miongoni mwa  waumini wapya hao katika Bwana, alikuwemo Mzee Otieno Olung’a Igogo ambaye ni baba yangu mzazi.


Wahitimu wa darasa la ubatizo wakielekea kwenye bwawa kwa furahq teyari kuzaliwa upya.

Juu ni Mzee O.O Igogo akibatwizwa kwa maji mengi. Hongera sana kwake, Mwenyezi Mungu azidi tembea naye kwenye safari hii ya kiroho.

Mchungaji Aketch pamoja na mama Mchungaji (mwenye nguo nyekundu) wakiwa na mtoto aliyezaliwa upya siku ya leo mzee O.O Igogo na mama Igogo.

Baadhi ya wanafamilia ya mzee O.O Igogo kutoka Segerea siku ya jana jioni waliungana na wanafamilia ya mzee O.O Igogo ya Kibada, wakapata chakula cha jioni pamoja, wakapumzika, na leo asubuhi waliamka mapema sana kwaajili ya kumsindikiza baba /Babu yao kipenzi kwenye safari yake mpya ya kiroho ambapo atabatizwa kwa maji mengi. …. Sifa na utukufu vyote twamrudishia yeye aliye umba Mbingu na nchi. Amen.

Eli baptism

Waacheni watoto wote waje kwangu kwakuwa ufalme wa Mbinguni ni wao; hayo ni maneno yake Mungu mwenyewe alitusihi tuwapeleke watoto kwake kwani ndipo wanapostahili kuwepo kwa usalama zaidi! Basi siku ya jana mtoto Eli alipelekwa mbele za Mbingu na kupokea upako mtakatifu wa kumkabidhi maisha yake kwa Yesu!  Eli ni mtoto wa my brother Kevin and Laura from Wichita, KS. Huyu ni mtoto wao wa pili. Mungu awakuzie, awalinde, na kuwabariki watoto wenu na familia yenu kwa ujumla! Kevin akiwa amembeba mtoto Eli!.....Kwafaida ya wasomaji wangu, huyu kaka yangu Kevin a.k.a KB (Kevin Bwahama)  ndio alikuwa my very first neighbor hapa Marekani, in Wichita, Kansas. Nyumba zetu zilikuwa zinatizamana, alikuwa ananijali as his little sister tumeishi kwa upendo sana. Namshukuru sana Mungu kwa kunipa some few good friends ambao hata mida ambayo nakuwa sina imani na Wabongo  nikiwaona watu  kama akina brother Kevin napata a little bit of hope to try to trust again! Asante sana kaka yangu for being there for me. Mungu azidi kukubariki sana. I'm sure your wife got the best man, such humble caring man! Japo kishingo upande lakini inanibidi niseme Yes! Is another good Muhaya ?? ......Btw, kwa wale mnajua story ya Notorius BTK leader miaka kama mitatu hivi baada ya kuhama Wichita aligundulika kuwa alikuwa anakaa mtaa wa pili toka kwenye nyumba zetu ??? Scary! Nafikiri ulikuwa inaitwa Hydraulic / Douglas       Mbarikiwe sana wapendwa! Ngoja nifurahie baby Eli na huu wimbo