Kesha la asubuhi: Kujua yasiyo julikana

*KESHA LA ASUBUHI*

*JUMAPILI 8/4/2018*

*KUJUA YASIYO JULIKANA*

  *_ Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. 1 Wakorintho 2:11._*

?Ufunuo sio uumbaji au ugunduzi wa kitu kipya, bali dhihirisho la kile kilichokuwepo, ambacho hadi kilipofunuliwa, hakikuwa kikifahamika kwa wanadamu. Ukweli ulio mkuu na wa milele uliomo kwenye injili hufunuliwa kwa njia ya bidii katika kuchunguza na kujinyenyekeza wenyewe mbele za Mungu. Mwalimu wa mbinguni huwa anaongoza akili ya mtafutaji wa ukweli aliye mnyenyekevu; na kwa uongozi wa Roho Mtakatifu, ukweli wa Neno hujulikana kwake. Tena, hapawezi kuwa na njia iliyo wazi na stadi zaidi ya ujuzi kuliko ya kuongozwa kwa namna hiyo. Ahadi ya Mwokozi ilikuwa, “Lakini yeye atakapokuja, huyo Roho wa kweli, atawaongoza awatie kwenye kweli yote” (Yohana 16:13). Ni kwa njia ya namna Roho Mtakatifu anavyopasha habari ndivyo tunavyowezeshwa kulielewa Neno la Mungu.

?Mtunga zaburi anaandika, Jinsi gani kijana aisafishe njia yake? Kwa kutii, akilifuata neno lako. “Kwa moyo wangu wote nimekutafuta, usiniache nipotee mbali na maagizo yako….Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako” (Zaburi 119:9-18).

?Tunaaswa kuutafuta ukweli kama kutafuta hazina iliyofichwa. Bwana huwa anafungua ufahamu wa mtafutaji wa dhati wa ukweli; naye Roho Mtakatifu anamwezesha kuelewa ukweli wa ufunuo. Hiki ndicho mtunga zaburi anachomaanisha anapoomba macho yake yafunguliwe apate kuona maajabu kutoka kwenye ile sheria. Nafsi inapoonea shauku ubora wa Yesu Kristo, moyo unawezeshwa kushika utukufu wa dunia iliyo bora. Tunaweza tu kuelewa ukweli wa Neno la Mungu kutokana na msaada wa Mwalimu wa mbinguni. Kwenye shule ya Kristo, huwa tunajifunza kuwa wapole na wanyenyekevu kwa sababu tumepewa ufahamu wa siri za utauwa.

? Yeye aliyelivuvia Neno ndiye mfafanuzi wa kweli wa Neno. Kristo alionesha kielelezo cha mafundisho yake kwa kuvutia usikivu wa wasikilizaji wake kuelekea kwenye kanuni za viumbe asili na kwenye vitu vinavyofahamika ambavyo waliviona kila siku na kuvishughulikia. Kwa namna hiyo aliongoza mioyo yao kutoka kwenye vile vilivyo vya asili kwenda kwa vile vya kiroho. – Sabbath School Worker, Dec. 1, 1909.

*MUNGU AKUBARIKI NA UWE NA SIKU NJEMA*

Leave a Reply