Joyce Kiria: 09/04/2018 ni siku ya kihistoria ya kutua mzigo huo mkubwa mno wa kulea familia peke yetu

Regrann from @joycekiriasuperwoman – Nipo na Kamanda wa Vita! Shujaa acha kabisa! Mpambanaji wa ukweli @paulmakonda • Ni fursa kubwa kwetu Wanawake wa Taifa hili tunaoteseka kutunza familia peke yetu, 09/04/2018 ni siku ya kihistoria ya kutua mzigo huo mkubwa mno wa kulea familia peke yetu, hatimae tumepewa fursa ya kupaza sauti zetu kwa Serikali yetu.

Binafsi naamini Hii ndo siku ya kusababisha mabadiliko makubwa ya sheria inayosimamia malezi ya watoto kuanza rasmi mchakato wa mabadiliko, na kuweza kuleta sheria kali kama za nchi za marekani.

Tatizo la baadhi ya wababa kukimbia majukumu ni kubwa mnooo ninahitaji viongozi wenye ushawishi kama hawa watusemee! •

Kwa kweli Asante zangu nyingi kwa shujaaa wetu mpambanaji sana Mkuu wetu wa mkoa @paulmakonda kwa kutuona wanawake wa Taifa hili tunavyoteseka na mzigo wa kulea familia peke yetu ilihali wababa wapo ???? TUMECHOKAAAAAAAAA • – #regrann

Leave a Reply