Pumzika kwa amani Mh. Celina Kombani!

kombaniKwa makasikitiko makubwa sana, naomba nitowe salama za pole kwa familia ya marehemu  Waziri Celina Kombani na Watanzania wote walioguswa na msiba huu. Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa rehema apate kuwatia nguvu na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu.

Kwa walio wengi ulijulikana kama mwanasiasa  wa chama cha Mapinduzi, na mfanyakazi wa Umma lakini kwa familia ya Otieno Igogo wewe ulikuwa sehemu ya familia. Japo mimi binasfi (Alpha) sikuwahi kujaliwa kukuona uso kwa uso lakini upendo wako na ukarimu wako kwa familia yetu ulikuwa mkubwa sana kiasi cha kujihisi kuwa tulishawahi kuonana. You were our Shero! Daima utadumu ndani ya myoyo yetu.

Utakumbukwa sana na rafiki yako kipenzi ambaye alifanya familia nzima ikujuwe (Mr. O.O Igogo) na kwaniaba yake na familia yake yote kwa pamoja tunasema mpaka siku ile ya hasubuhi ya fahari itakapo fika; pumzika kwa amani mama yetu. Poleni wanafamilia wote.

“Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda;  baada ya hayo nimewekewa taji ya haki, ambayo Bwana, mhukumu mwenye haki, atanipa siku ile; wala si mimi tu, bali na watu wote pia waliopenda kufunuliwa kwake.” 2 Timothy 4: 7-8

One thought on “Pumzika kwa amani Mh. Celina Kombani!”

Leave a Reply