“Naamini bado nina nafasi kwenye moyo wako please usiniangushe”!

Umeshawi kumpenda mtu asiyekupenda? Well, naamini wengi tu imeshawatokea. Pengine utakuta kama ni mwanamke basi anakubali hata kuwekwa kimada miaka nenda rudi basi tu mlimradi naye aseme nipo kwenye “relationship” au “married” ?? hiyo yote nikupenda asiye kupenda. Nawengine ndio wanakuwa na ujasiri zaidi kama huyu mrembo Teddy!  Jamani hii siyo hadithi ya kutunga, ni kitu cha kweli kabisa. Teddy Lacoste ni binti mzuri sana, na mchakarikaji. Kwakweli ametokea kumpenda kijana Tuma. Kwa bahati mbaya Tuma anampenda Teddy kama rafiki tu / kama dada. Lakini Teddy anaona kuwa yeye na Tuma ni “soul mate” match made from Heaven! Hivyo amekuwa akimbembeleza Tuma wawe pamoja naikiwezekana waoane wawe mke na mume wazae watoto! Ameshakuwa akimbembeleza Tuma kwa zaidi ya miaka 2 sasa kwa kutumia lugha zote za mapenzi, in private lakini ikashindikana. Sasa akaamua kuja public kwa social media. Yani ni anapost picha na status za kumuomba Tuma amkubali #Live lakini Tuma kagoma!!   Tuma ni kama mdogo wangu, age mate na wadogo zangu, amekuwa nikimuona pale mtaani kwetu KJ. Hivyo amenizoea ananiita dada. Sasa, mwaka jana mie nikaona Relationship status ya Teddy kwa Facebook kuwa “engaged to Tuma” na picha ya pete. Halafu na Tuma aka “Like” hiyo status. Basi mie nisifurahi  nikaja ipost humu (somahapa) si ndio Tuma anakuja niambia kuwa it’s not true haja mu-engaged ni vituko vya Teddy ?? mbona yalinishuka, nami nikagoma kuiondoa kwani yeye Tuma huwa ana “LIKE” hizo status za Teddy!  Sasa jana nikamwambia Tuma kuwa leo nakuja kuanika hii story yao kwa blog ili watu wengine watoe ushauri wao. Kwani mie hiyo kesi ilinishinda pale Teddy alipoileta kwangu mwaka jana. Nilimwambia mapenzi ya kutongozewa au kulazimisha mtu hayanaga mema mengi! Nimeona wengi huwa hawana furaha ya kweli. Ni shida. Hivyo yeye mwenyewe ndo itabidi aendelee kum #Seduce Tuma mpaka aukubali wimbo ?? Though moyoni natamani kama wangekuwa pamoja. I love both of them ?? ……. Haya wewe una ushauri gani kwa Teddy na Tuma?

Leave a Reply