
Huwezi kumzuia ADUI…….
kukutisha, kujitapa, kukukejeli na kukudhihaki, kujiona yeye ndio bora kuliko wewe………kubwa Simama kwenye nafasi yako. Ukikaa kwenye nafasi yako wote waliokukataa, waliokususa, waliokudhihaki, waliokutusi na waliokuona si lolote si chochote ipo siku watakuunga mkono. Waliokuona hufai kuwa kwenye maisha yao…………………..hao hao watasimulia mambo makuu kuhusu wewe, watakutamani na watakuheshimu. Hata wasipokiri kwa vinywa vyao mioyo yao itakiri na kuthibitisha wewe sio wa kawaida. Kumbuka Ulivyo leo sivyo utakavyokuwa kesho. Nakukumbusha tena Kaa kwenye nafasi yako, ndani yako unayo mambo makubwa ambayo bado hujafanya hata Robo.

Wewe sio wa kawaida…….mtag na umwambie na mshikaji/shost wako wewe sio wa kawaida…Usilale wewe ndio kwanza kumekucha. Simama kwenye nafasi yako. Je nafasi yako unaijua?????
Nimependa sana hizi picha za rafiki yangu wa miaka mingi sana toka tupo shule pale Kowak Girls Secondary school iliyopo wilaya ya Rorya, mkowa wa Mara. Hapo ndipo tulikutana na mpaka leo hii zaidi ya miaka 20 bado tu marafiki sana. Yeye anaishi Geita………..ha! ha! ha! Ngoja niwape story moja hivi ya huyu rafiki yangu ??? kwa mara ya kwanza kusikia mvua inapiga kelele kwenye bati ilikuwa shuleni Kowak! Aliliaje sasa, alikuwa anatetemeka kama mtu mwenye mapepo! Tulikuwa wageni kabisa shule tupo form one akasema hakuwahi kusikia mvua ikifanya hivyo , tukawa tunamshangaa lol! Kumbe toka azaliwe amekulia kwenye nyumba za ghorofa ??marehemu baba yake alikuwa General Manager wa Mwatex hivyo siku zote ameishi kwenye nyumba za shirika. Halafu shule alisoma Nyakaoja, Mwanza ambapo nazo ni ghorofa. Maisha ya watu na experience ni tofauti sana, kile ambacho wewe unaweza kufikiria kuwa ni kitu cha kawaida “normal /simple thing” kumbe kwa mwingine ni miujiza! Lakini bado wote ni binadamu na thamani yetu wote ni sawa kabisa…………Kuna binamu yangu yeye alikuwa anasema anaomba Mungu amjalie apate elimu nzuri na pesa ya kuweza kumjengea mama yake nyumba yenye paa ya “mabati” eti naye aweze sikia sauti ya mvua ikinyesha kama wengine ?? kwani akiwa ndani ya nyumba ya “majani” hasikii wala hajui mvua kama inanyesha mpaka atoke nje!! Lakini Mungu si Athumani, her wishes came true! Nasasa hivi ni judge mwenye PhD naalipo anza kazi kitu cha kwanza alimjengea mama yake nyumba ya “mabati”!
Prisca umependeza sana. Mbarikiwe wewe na familia yako. Much love ❤❤
Mh. ShyRose Bhanji akiwa ndani ya Bunge la EALA. Napenda sana kumuangalia huyu dada yangu kwani ni mwanamke shujaa sana. Nimekuwa nikimfatilia safari yake katika maswala ya siasa kwa muda mrefu sana. Kwakweli nimejifunza mengi sana toka kwake kama mwanamke. Hakati tamaa, na haogopi kujaribu. Nimfano mzuri sana kwa watu haswa wanawake ambao wanafikiria kupata “shot cut” kwa kuigawa “miili” yao kwaajili ya kufanikisha malengo yao.
Well, mtu anaweza sema wapo wanawake waliofanikiwa kwa kuigawa miili yao! Sasa ngoja nikwambie hao wanawake ni kama jipu linalovuja usaa halafu wao wakalipangusa kwa nje na kufunga vizuri na bandage bila kutoa “kiini” cha jipu! HAKUNA MAFANIKIO bali ni wamejiweka au kujijengea daraja la utumwa kwa wanaume! Yani siku zote hawatokuwa na amani wala furaha moyoni mwamgu kwani wanajua wako “powerless” hawawezi simama wenyewe bila kutoa miili yao. Na huwa hawafiki mbAli kabisa. Hii ni hata kwa wale wanao pata maendeleo kwa kutumia njia isiyo halali, huwa hawana amani, wala furaha, hata kama anapesa kiasi gani. Hivyo ni bora uangaike kwa jasho lako hata kama ni kwa tabu lakini matunda yake ni matamu sana. Hongera sana dada yangu Mh. ShyRose Bhanji kwa kuwa mfano mzuri kwa jamii yetu. Ubarikiwe sana. (Pichani ni Mh. ShyRose Bhanji, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje Dr. Susan Kolimba, na mwingine ni Mbunge wa EALA).

Hii leo ndio picha yetu ya moto moto! Baba yangu, kaka yangu mkubwa, wifi yangu mkubwa na my nephew Gabriel. Wifi yangu yeye anafanya kazi Utegi Technical Enterprises Ltd, hivyo baba yetu ni “top boss” wake. Kwahiyo hapo kuna undugu wa kidamu na ki-business ??
Mambo yakuchangia gari na mumewe (kaka yangu) basi siku nyingine kaka yangu huwa anabanwa na kazi zake hivyo inabidi wifi yangu apande daladala ?? hiyo haikumpendeza boss wake (baba yetu) jana akaamua kum-surprise na “kausafiri” wake ambao hautumii mafuta sana na hivyo nirahisi kwake kumudu mizunguko ya mujini…………..”Amen. It was always painfull to me seeing my own daughter in law jumpimg on daladalas, While I could afford her a vehicle. So yesterday I suprised her with that small gift. She was Amazed!” ? hayo nimaneno yake babamkwe wa ukweli ??
Ha! Ha! Ha! Nimependaje hii picha! Huyu ni kaka yangu anaitwa Martin Sarungi hapa yupo na binti yake. Nimecheka kwanza kwasababu ya hiyo peace symbol (✌) aliyo weka mtoto wake. Huyu kaka yangu yeye ni Chadema / UKAWA damu damu. Naona kamridhisha na binti yake? ubarikiwe sana kaka yangu na familia yako yote.
Sister Penny doing what she does best! Kufundisha watu nikipaji cha pekee sana haswa kufundisha watoto wadogo. Sio wote wanaoweza kusoma na kushika pen au chaki wanafaa kuwa walimu / wakufunzi! Ni talanta waliojaliwa nayo watu wachache sanaaaaaa kama huyu dada yangu.
Hapa ni siku ya Sabato (Juma Mosi iliyopita) akiwafundisha watoto maneno ya Biblia kuhusu uumbaji wa Mungu. Penny yeye si mwalimu, ila anahicho kipaji cha kuelekeza / kufundisha watu kwani hata sehemu kubwa ya kazi yake ni kuelekeza watu……Kama nilivyo sema kipaji cha kufundisha watu ni kipaji cha pekee sana, kwakweli mimi sikujaliwa nacho ?? mimi na panick haraka sana na huwa nakuwa confused kama mtu anielewi! Hata mwanangu anajua hilo yupo radhi afundishwe na mtu mwingine lakini siyo mimi ??? nilimfundisha kuendesha gari mbona ilikuwa ni patashika?! Lakini hakuwa na ujanja alielewa tuu mpaka akapata driving license yake. Hakuna ubaya wowote kusema your weakness (es) ni njia moja wapo yakuonyesha kuwa umekomaa kifikra na unajitambua!Hivyo mimi huwa nipo muwazi sana sioni shida kusema my weakness as a normal human being!
Naomba nimpongeze dada yangu Peninah Tenga kwa kipaji ambacho Mungu amemjalia nacho na anakitumia kama kinavyo stahili, zaidi kwa kumtukuza Mungu. Ubarikiwe sana dada yangu na Mungu awaongoze watoto wetu washikemafundisho yake, Amen!
My dad, Mr O.O Igogo, enjoying himself somewhere in China last week. We thank God for His traveling mercies, he’s safely back home.
Nimevutiwa na gukuswa sana na maneno ya #KichunaWaKizaramo hapo juu ☝ ……….Hongera sana Maryam, Mungu akuongoze, akubariki sana, usiishie hapo tuu bali ukawe the next Christian Amanpour!
Wow! Mama akiwa beneti kabisa na binti yake, kwa support na upendo wa mzazi. Hongera sana Linda kwa kuwa mama mwema.
Wapendwa wasomaji wangu, nawaombeni tum-support mtoto wetu. Maryam pia yeye amejaliwa kipaji cha ushonaji, na amesha onyesha dalili za kwenda mbali zaidi basi tumuunge mkono wapendwa. Yeye anabuni nguo za midoli. Unaweza kuona kazi zake na mambo anayofanya kwa kum-follow kwenye IG yake kwa jina la #Fashionadoz. Mbarikiwe sana mnapo fanya hivyo.
Once again, Congratulations Maryam and your whole group, wishing you the best of all.
Mama na binti zake. Wamependeza sana. Mwenye dera la blue hapo kati ni my friend and schoolmate wangu toka Kowak Girls Secondary school iliyopo wilaya ya Rorya, mkowa wa Mara. Yeye anaitwa Maimuna, mwenye dark-blue ni dada yake mkubwa, na mwenye green ni mama yao mzazi. Asanteni sana wapendwa, mbarikiwe mno.
Binadamu yangu Wakili wa kujitegemea Richard Opiyo (Katikati) akiwa na marafiki zake ndani ya Ngorongo Crater, Arusha. Mbarikiwe sana
Nimependa sana hii picha ya Hawa, from the ‘Queens land’ kapendeza sana na lemba lake. Simple and beautiful!


I truly love the New Yorkers family, beautiful people with beautiful soul!
Guys, you know how to partyy, one day gonna join you ? not like I’m jealous no-no-no! Just want to have fun with ya! ??
Awhh! Look at that msosi, so yummy!
Halafu wee mtani mmh! Unapenda kurusha watu roho kha! And who is that ? yes him!! “Wivu sina lakini roho inauma” ?? Haya bwana, lemme zip it oops! Am typing!
Brothers looking shap! ?
Siyo siri umetisha mtani wangu! To cute ??
Mr and Mrs Mali Kimesera. Naipendaje sasa hii couple ?? Wamependeza sana. Hapa ni jana wakiwa katika charity event huko Atlanta, Georgia a.k.a “Hotlanta” Georgia. Safi sana LB na Manager wake mnafanya kazi nzuri mno. Great example to many couples. Mbarikiwe sana.
Huyu #KichunaWaKizaramo unajua ni level nyingine kabisa! Hiyo nguo aliyovaa Missy LB ni kashona mwenyewe designer wetu waukweli ? soma hayo maneno aliyo andika basi kama uwamini………
Nahivi ndivyo ionekanavyo kwa nyuma. Hongera sana #KichunaWaKizaramo Mungu akujalie ufike mbali zaidi. Pia hongera kwa shemeji yetu kwa kuwa Manager mzuri. Mbarikiwe mno ?



Marehemu baba wa taifa na Rais Dr. Magufuli. Maneno kwa vitendo ????

Lovely pics of Mr. Madebe. I love the kitinge, very colorful. Be blessed Mr. 
Pendeza sana binti wa mzee Otto! Nimepitiwa na ulivyo vaa na mpangilio wa rangi za mavazi yako ni mzuri sana. Ubarikiwe sana.
Simply beautiful!