USISAHAU MALIPO NI HAPAHAPA!!Hivi unanini wewe? umeolewa kama wanawake wengine, umemkuta mumeo anawatoto unaanza kuwa adui kwao na kuwatenganisha na baba yao. Au umeolewa baada ya mumeo kuachana na mke wa awali sasa umeanza kumwambia mumeo kila mabaya ya hao watoto wake na mazuri ya hao wakwako. Kiu yako ni kumweka mbali na wanae na kumfanya awapende wakwako. Kibaya zaidi unawashawishi wanao wawachukie hao watoto wa mumeo, eti unawaambia kuwa wao wanashea baba ila mama ni tofauti na kwamba wajiepushe nao sio watu wazuri. Hivi nia yako hasa ninini? Haujui kwamba kila ulipandalo utalivuna? Hujui kwamba “what goes around comes around?”. Usijefikiria ndio umefika, hujui hata kwanini mwenzako alitoka, nawewe unaweza kutoka vilevile – Chris Mauki
Category Archives: Inspirational stories
“We should all be feminists”!
Ni aibu sana kuona kuwa tupo 21st century na bado haya mambo yanatendeka! Kwamba wanawake hawatakiwi kuwa na ndoto za kufanya vitu vikubwa kisa hato olewa??!! Really! Asipo olewa anakuwa si mwanamke kamili!! Akiolewa hajazaa basi ndoa yake batili!! Akiolewa , kazaa watoto wa kike tupu bado anaonekana hajazaa!! ……….Akifanya mambo makubwa eti huyo uhuni ndo umemsaidia!! Kwakweli sauti ya mwanamke wa Kiafrica bado haina nguvu kabisa siyo tu katika jamii bali hata ndani ya familia nyingi!! Na hili swala halitaisha kama bado familia hazijatambua na kuona thamani ya mtoto wakike kuwa ni sawa na ya mtoto wa kiume! Haya matatizo yote yanayo husiana na mambo ya jamii huwanzia ndani ya nyumba na tiba yake huanzia nyumbani! Pia vile vile ni ngumu sana kukabiliana na hizi changamoto kama bado tunawachagua viongozi wakiume kusimamia mambo ya wanawake!!………Tafakari, fanya mabadiliko!
Strong walls shake but never collapse!
Hakuna kitu au jambo jipya hapa duniani! Vitu vingi tunavyo viona au mafundisho mengi tunayoyasikia huwa yanakua yalishawahi tokea na kusemwa huko nyuma na watu fulani! Tofauti inakuwepo kwenye namna ya usemaji au style ya maneno yanayo tumika kufikisha huo ujumbe mpaka kuonekana kama kitu kipya au kugusa hisia za watu……. Hivyo nimependa sana ujumbe hapo juu ? hasa sehemu hiyo ya mwishoni “strong walls shake but never collapse”!! Ni ujumbe ambao nimekuwa nikiusikia katika maneno tofauti tofauti lakini haya ya leo yamenigusa zaidi!……….. anyway, duniani kuna mambo mengi na watu waaina tofauti tofauti. Wengine wabaya, wengine wapo sawa kiasi, na wengine ni watu makatili wenye roho za Farao! Katika hao watu wapo watakao kupa furaha, wapo watakao kupa huzuni, na wapo watakao taka kukuangamiza kabisa kwasababu tu ya udhaifu wao na chuki walizo nazo juu ya nafsi zao lakini kwakuwa hawawezi jibadilisha hivyo wanaona kuumiza wengine ndio njia pekee ya wao kupata faraja! Katika hayo yote mema, mazuri, na mabaya tambua tu kuwa wewe ni ukuta imara ambao kamwe hauto anguka! Unaweza yumba kwa mtikisiko lakini hauto anguka kamwe!
Kutoka Facebook
#FBF #Mahojiano na Linda Bezuidenhount
Leo nimeamua ku “Flash Back” videos za interview ambazo nilifanya na mwanamitindo wa kimataifa Ms. Linda Bezuidenhout mnamo mwezi wa Pili mwaka jana 2015!
Hapo juu ?nisehemu ya kwanza ya mahojiano. Na hapa chini ? nisehemu ya pili au ya mwisho ya mahojiano yetu.
Haya yalikuwa ni mahojiano yangu ya kwanza kabisa kufanya huku nikirekodiwa. Nilipewa hii nafasi ghafla, yani nilijua nataka kufanya mahojiano na Linda lakini sikujua lini yatafanyika. Mara ilikuwa siku ya juma Tatu napigiwa simu na kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog nakuambiwa kuwa Linda ametukaribisha kwake siku ya Juma Mosi na yupo teyari kufanya mahojiano nami! Nilisita, lakini kaka yangu akasema nitaweza nisiogope! Basi hivyo ndivyo ilivyokuwa. Kama hujawahi yaona basi nakuomba uyatazame na niruhusa kutoa maoni yako! ……….Kwakweli siku zote nitamshukuru sana Linda kwa nafasi hii aliyonipa na pia sito choka kuwashukuru kaka yangu Dj Luke wa Vijimambo blog pamoja na mtani wangu Mubelwa Bandio wa Kwanza Production kwa kunisaidia kufanikisha hii ndoto. Sina chakuwalipa bali nawaombea baraka siku zote! ??
Hot Pic of the day: Mmiliki wa Facebook akila ugali na Samaki!
“Schoolbag lighting up homes”
What a brain! Congratulations to all the brain behind “Mobile Library”. Your faith and determination is what will change the lives of many underprivileged students in Tanzania. You are an inspiration to many! Congratulations!
Source: CITIZEN
Picha katika 50th wedding anniversary ya Mr and Mrs Mkapa
Wajukuu wakiwa na nyuso za furaha wakisubiria kushudia historia ya maisha ya ndoa ya bibi na babu.
Familia ya mzee Mkapa ikiwa katika ibada takatifu ya shukrani kwa Mungu katika kuwawezesha wazazi wao kudumu katika angano takatifu kwa miaka 50!
Mr and Mrs Mkapa wakiingia kanisani huku wakisindikizwa na watoto wao, in-laws, na wajukuu wao!
Wakiombewa na kuvalishana pete ya nadhiri ya miaka 50
Wow! Walipokea cheti maalum toka kwa Papa huko Vatican! What an inspirational event! God bless them abundantly
Mambo ya kumbu kumbu
“kodaki” moments kutoka kwa wanafamilia
Wakisalimiana na ndugu, jamaa, na marafiki kutoka pande zote. Na hapa namuona mstaafu Major General G. Waitara na mkewe
Viongozi mbali mbali wa serikali na dini walikuwepo
Mzee Mkapa akiongea na wageni waalikwa
Watoto, in-laws, na wajukuu waki share cake ya kheri ya miaka 50 ya ndoa
Rais aliyestaafu hivi karibuni Mr Kikwete na mkewe nao walikuwepo
Wana familia
Watu walipendeza sana
Safi sana!……… Tunawaombea na kuwatakia kheri siku zote ili tuje tushuhudie their ‘Diamond’ anniversary! ………….. Btw, Happy 13th Wedding Anniversary to you Foster and your darling! 37 more years to go to celebrate that “golden” moment! All the best!
“Through that loss it’s also possible to find yourself” -Iyanla Vanzat
Ujumbe mfupi lakini ni mzito sana! “In this journey called life, it is possible to lose everything. Through that loss it’s also possible to find yourself”!!…………. Watu wengi (including myself) tunapoteza muda mwingi kuwaza kwanini hiki kinatokea kwangu? au kwanini hawa watu wananitenda hivi? Badala ya kufikiria ni nini natakiwa nijifunze katika hili lililo nikuta?? ………. Wiki iliyopita kuna rafiki yangu wa muda mrefu sana. Tunaheshimiana sana na huwa I considered him as a “brother figure” to me, baada ya jitihada nyingi za kunitafuta alifanikiwa kunipata wiki iliyopita na tukaongea kwa simu. Moja ya swali alioniuliza ni mbona nime keep a distance from him! Nikamwambia nimesikia mara nyingi kutoka kwa wahenga kuwa ukitaka kuwa imara basi jifunze kusimama mwenyewe!! Nikamwambia nahitaji kuwa imara ili niweze kusonga mbele na kufikia kile ninacho kiamini kuwa ni ndoto zangu! Akanishangaa!!…… Anyway, ninachotaka kusema ni kwamba; katika safari hii ya kutaka kufanikisha ndoto zangu nimekutana na vikwazo vingi sana toka kwa ndugu wa karibu pamoja na wale niliyo amini kuwa ni marafiki zangu! Nime kuwa betrayed multiple times na watu ambao hata sikuweza wafikiria kuwa wangeweza fanya hivyo! Katika safari hii ya kutaka kutimiza ndoto zangu nimepoteza marafiki wengi sana!! Nimetumia muda mwingi sana tena sana KULIA NA KUJITIA! Kutwa nilikuwa najiuliza kwanini? And why me?! Lakini namshukuru sana Mungu kwani katika kulia huko na hali ya kukata tamaa akanipatia nguvu za kusonga mbele. Katika hali hiyo hiyo ya kulia na kuhuzunika I found my own strength!!! Kitu ambacho hapo mwanzo sikudhania kuwa ninacho! Nilikuwa nategemea sana tena sana emotional support ya familia, ndugu, na marafiki kama my strength!! Bila kujua kuwa hata familia yako wakati mwingine inaweza isisimame nawe vitani!!! Bila kuwaza kuwa hata ndugu zako wanaweza kuwa maadui zako!! Bila kufahamu yakuwa watu wengi tumezungwa na maadui wengi waliopo karibu yetu chini ya mwanvuli ujulikanao kama “close friends”!!……….. Katika changamoto hizi ambazo nimepitia I found myself!! Nimejifunza kuwa ni kweli you don’t need a crowd of people to be happy!! “In this journey called life, it’s possible to lose everything. Through that loss it’s also possible to find yourself”!!…….. Vipi wewe mwenzangu, have you found yourself au bado unaangaika na the feeling yakutaka kuwa accepted na watu ambao wana ku- betray na kukuzibia mibaraka yako ambayo Mungu anataka kukubariki nayo?!! Tafakari!!
Happy birthday Francisca and Faith!
Nimependa huo ?ujumbe toka kwa Foster kwenda kwa ndugu zake katika siku yao muhimu! Kilicho nivutia zaidi kwenye ujumbe huo ni namna ya uhusiano wao jinsi ulivyo kama ndugu!………. Unajua kuishi nje ya Tanzania kume minifumbua macho kwenye mambo mengi sana haswa katika maswala ya familia na undugu! Nyumbani Tanzania watu wengi wanaishi maisha ya “kinafiki” sana pale inapokuja swala la kuwa mkweli na hisia zako haswa kwa watu wako wakaribu! Yani kumwambia au kusema ukweli kwa watu wako mara nyingi inachukuliwa kuwa ni “chuki”!! Wakati wenzetu wanaamini kuwa if you truly love and care for someone lazima utataka ajue ukweli!! And family is not family if one can not be honest to his / her feelings without the fear of rejection!!……… Nimependa alivyosema wamezinguana sana lakini usije jaribu kumchokoza mmoja wao ?? ………..Anyway, hakuna familia iliyo kamilika hapa dunia kila moja inamapungufu yake! Na kugombana kwa wanafamilia sio mwisho wa undugu au kuondokewa kwa upendo miongoni mwao!! Kumbuka damu ni nzito kuliko maji…………….!!
Happy birthday Francisca Wandiba na Faith Kalanje. Mungu awape uhai mrefu na afya njema!!
Amani! Amani! Amani! Ndiyo nguzo ya Tanzania!
Watu walio starabika utawajua tu kwa matendo yao! Yana ng’aa hata gizani!! Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni!! Kwakweli mzee Lowassa na mke wake ni watu wastarabu sanaaaaaa! Hawa ni watu ambao hawajazoea “drama” hata kidogo! Ni watu wa kujishusha. Haya mambo mengine ni watu tu wanataka kuwalazimisha lakini sio asili yao! Unajua kuna watu ni wastarabu wa mavazi tu! Yani ukiwaona utafikiri tabia na roho zao zinaendana na mavazi yao ya kitanashati!! Kumbe ovyo kabisa!! ……….anyway I love this picture a lot! Siasa sio uwadui na wala sio chuki zisizokuwa na kichwa wala mguu!! Tunataka democracy ndani ya Tanzania lakini hatuwezi kuvunja nguzo yetu kuu (amani) halafu mkafikiri tutakua salama baada ya hapo!! Nope! Pindi tutakapo jaribu vunja amani ya nchi yetu basi tuhesabu maumivu! Haitokaa irudi tena! Niambie nchi gani ambayo imechezea amani ya nchi yao nawakaweza irudisha???!! Amani! Amani! Amani! Ndiyo nguzo na msingi wa Tanzania!!
“Tulaani kila mtu atamkae mwita albino Zeruzeru”- TAS Temeke

Katika pita pita yangu huko Facebook nikakutana na huo ?ujumbe/ angalizo!……… Nimuhimu sana watu kujifunza kuwa kila kiumbe chenye uhai kina hisia na kinafaa kuheshimiwa!! Katika jamii yoyote ile iliyo staarabika, wenye watu wenye kujitambua na yenye busara huwezi kuta hata siku moja wakiita binadamu kulinganga na ulemavu wao, rangi zao, au mapungufu yoyote yale walionayo! Hata Adam na Hawa baada ya kukaidi amri ya Mwemyezi Mungu hakuwaita majina tofauti na yale walio nayo! Sasa sisi kwanini tunapenda ku label watu? Tena watu wengi sana in Bongoland wanfikiria its OK to label people as the society has “legalized” it!!! ………………..
Hili angalizo linanikumbusha my childhood life!……… Nilipokuwa mdogo nilipata matatizo ya meno ikabidi nitolewe meno yote ya juu na baadhi ya chini. Kwabahati mbaya meno yangu yalichelewa kuota mpaka nakaribia darasa la pili (Std 2). Sasa basi yani harassment that I used to get at home was huge compared to what other students teased me at school!! Yani nilikuwa hata nashindwa kuongea na ndugu zangu saa zote nikitaka kufungua mdomo niseme kitu utasikia mtu ananicheka na kuniita “mapengo”!! Yani hata saa nyingine mtu badala ya kukuita jina lako utasikia anakuita “wee mapengo”!! Halafu kana kwamba hiyo ilikuwa haitoshi nikawa nafananishwa na bibi yetu fulani (sasa hivi ni marehemu) huko kijijini Utegi ambaye alikuwa na matatizo ya meno hivyo meno yake yote yaling’oka (hakuwa na meno). Napia alisadikika kuwa na sura mbaya!!! Hivyo badala ya kuniita jina langu wakawa wananiita jina la huyo bibi pale walipo ona nimekosea kitu au wakitaka kuniudhi or just to make funny of me kwani walikuwa wakisema I look exactly like her!!! Trust me, hivi vitu vinauma sana tena sana especially when you are just trying to enjoy your childhood like other children and all you can think is someone watching my mouth? So am I really ugly as they say it?!!………
Honestly these type of abuses need to end!! It’s not cool, not funny, it is wrong in all levels!! It kills people’s self esteem!! ……….. kitu ambacho sijakielewa kwanini TAS waone nisawa kuitwa “albino” ? Lakini si “zeruzeru”? Kwani kiswahili cha “albino” ni nini au mie ndo sielewi?!……………. Anyway, regardless, we have to respect and honor their wishes!! The name is offensive to them then people need to stop using it whether unaelewa kwa nini au la! Jukumu lako nikuacha kulitumia na si kujua kwanini!! Na ujifunze kuwa na UTU wa kuwaita watu kwa majina yao halisi na sio kutokana na ulemavu wao!!
“If she’s worth it, you won’t give up “!
“Every woman is born a princess. Yet not every woman grows to become a queen”!
GOD IS RAISING AN ARMY OF WOMEN
Every woman is born a princess. Yet not every woman becomes a queen. Being a queen requires growth, change, evolving, maturing; and learning to value, respect, and care for yourself and serve others. Esther was selfless and willing to even die as she went before the king and plead with him to stop the death of the Jews. Back then you could be killed if you approach the King when he had not called for you , so this involves being more selfless than you are selfish, and more loving than you are defensive.
A queen is a woman who knows who created her and the purpose for which she was created. After Esther became a Queen it didn’t end there. She would pray and fast to fulfill the reason why she had been made Queen which was saving the Jews. A queen is a woman who never stops growing into who she ought to be, a wise woman who is rarely in the midst of gossip, and who partakes not in drama and childish things. Esther knew the dangers of what could have happened to her but she didn’t stop or give excuses. A queen is a woman who is strong-minded, intelligent yet humble, soft spoken, and doesn’t justify her weaknesses, but daily focuses on improving. A queen is everything a princess has potential to become. Until a woman grows into the queen she is created to be, she will remain a lost princess.”
Like Esther, discover your purpose of living and your God-given path which leads you to the palace. Your purpose will open doors for you as proverbs 18:16 tells us. Don’t get too comfortable being an idle queen but keep forwarding ahead. Be a woman of prayer, fasting and daily meditation of the word of God. God is raising women like Esther to arise from being a lost princess to becoming a Queen.
By: inspired with T_sha
Don’t hasitate be original that’s how change happens-Maria Sarungi Tsehai
Ubarikiwe sana kaka Tumaini Kajo!
Naomba niamini kuwa haya uyasemayo yanatoka ndani ya roho yako na ndivyo ulivyo! Na kama nikweli basi ubarikiwe sana! ……….. Siyo kwamba sikuamini bali kwa experience ambayo nimepitia na kuona, nimegundua kuwa watu wengi wanaojaribu kuweka a “positive” image kwenye public si wakweli na wala hiyo “image” haiendani na huwasilia wao! Na wengi haswa wanaume wanatafuta the weakest woman ambaye ata cover na ku protect their image ya kuwa ni mtu mwema kumbe sivyo! Sorry, I’ve seen a lot of abusive men and this has nothing to do with you! Naongea in general!………. Otherwise, ubarikiwe sana! Mabadiliko yanaanza na wewe!
Je, wamfahamu John Stephen Akwari?!
Binafsi nilikuwa sijawahi msikia John Akwari mpaka juzi kati nilipokutana na hiyo ?post hapo juu. Labda nianze kwa kusema kuwa kwenye maswala ya michezo ukitoa netball, basketball, tennis, na swimming kwakweli mie si mpenzi sana wa michezo. Hivyo huwa siifatilii sana! Kwasababu hiyo ni utetezi tosha wa kwanini simfahamu John Akwari. Au pia niseme taifa letu limeshindwa kuwaenzi watu kama John Akwari na ndio sababu watu wengi hatumfahamu!…………..Lakini hiyo haikuwa sababu ya mimi kumuweka hapa. Sababu kuu nikutaka watu waguswe na habari ya huyu shujaa wetu ambaye sisi tumeshindwa jivunia wakati mataifa mengine wanajivunia na kuguswa kwa ushujaa wake!………… Najua maisha yana changamoto nyingi ambazo wengi wetu tunapitia. Na saa nyingine mateso na maumivu yanakuwa makali sana kiasi cha kutaka kukata tamaa ya kutimiza ndoto zako au kuendelea na maisha. Trust me, I’ve been there multiple times! I truly understand and know the feeling! Basi usife moyo, kuwa mshindi si kuwa wakwanza kufika bali the spirit of not giving up is the real victory! …….. Embu tazama hii video
Nilijaribu kutafuta habari yake na nikakutana na haya ?mahojiano ambayo amefanya na Issa Michuzi soma hapa ? Michuzi …….. Acha kifo ndio kiamue kuwa ndoto zako zimefika ukingoni lakini wewe kazana tu! Kama unahitaji kupumzika basi fanya hivyo! Vuta pumzi ukipata nafuu endelea na safari. Wengi tunaonekana tunatembea kiushujaa kabisa japo miyoyo yetu ina ‘chechemea’ kama matone ya drip kutoka na mambo ambayo tumepitia au tunapitia.
“Mungu huweza kuinua mtu usiyemdhania kukubariki” J.J Idd
Habari ya mama aliyeuguliwa ghafla na mtoto wake majira ya SAA 2 usiku, mtoto alibanwa na kifua(asthma), hali ilikuwa mbaya na mama akaenda kuomba msaada kwa jirani yake aliyekuwa na gari, akamjibu gari haina mafuta, akaenda kwa mchungaji ili amsaidie, akamjibu nina wachungaji toka USA, hivyo sitaweza kuwaacha peke yao, mama hakuwa na jinsi aliamua kumbeba mtoto ili amuwahishe hospitali akiwa na hofu asije kufa kama baba yake aliyefariki miaka michache kwa ugonjwa huo. Huyo mama alikuwa na tatizo la mguu na mtoto alikuwa mzito, mama alianguka Mara kadhaa na akainuka kuendelea na safari. Njiani alikutana na watu waliotoka kazini aliomba wamsaidie walimpuuza na alijaribu kusimamisha magari hayakusimama. Kichaa mmoja mchafu aliyekuwa akizungukazunguka mitaani na jalalani alipomuona yule mama anavyohangaika na mtoto akamwendea na kumchukua mtoto, kisha akamweka begani, mama hakuwa na la kusema ila kumwelekeza Hospitali, yule kichaa alielewa akaenda haraka hadi Hospitali. Ma doctor walipomuona yule kichaa na mtoto wakajua kuna dharura, wakamchukua mtoto na kumhudumia haraka, baada ya dk.10, mama wa mtoto akawasili, kisha ma doctor wakatoa taarifa kuwa, mtoto angecheleweshwa dk 5 angekufa. Mungu alimtumia yule kichaa mchafu kuokoa maisha ya mtoto. Hivyo usimteegemee Mch, jirani, wenye magari, matajiri nk. Mungu huweza kuinua MTU usiyemdhania kukubariki. Mwamini Mungu atakubariki. Usitumainie wanadamu hakuna baraka kwao. Mungu huinua vinyonge ili kuangusha vyenye nguvu.
Hot pic of the day:….21!! And Pilot?!!
Wow! Wow! The youngest Commercial Pilot in the WORLD!!! And he is from Zambia, Africa!! Congratulations to 21 years old Kalenga Kamwendo the Youngest Commercial Pilot in the world!……….But I’m sorry to say this, I’m not sure if I will trust a young person with my life ?? I can barely trust my daughter when on the wheel?? “mama you can move to the back seat” often she tells me that lol!………… Congratulations young man, you truly made us proud!