Category Archives: Elimu juu ya maisha

“Ukiniuliza Mimi nitakuambia huyo asiyekua lolote wala chochote Leo ndio mzuri….”~~~Rose Shaboka

Nguo unayoinunua dukani ikiwa READY MADE wakati mwingine sio rahisi kuirekebisha iwe exactly unavyotaka. Lakini nguo unayoenda kushona kwa Fundi kuanzia mwanzo ni rahisi sana kuitengeneza ikawa exactly kile unachotaka. Msichana unayetaka na kuomba mwanaume ambaye tayari ana kila kitu (ready made) hujui unachokiomba. Sio vibaya ukipata mtu ambaye ana kila kitu tayari lakini nakuambia usimkatae wala kumdharau huyo ambaye hana kitu Leo. Ukiniuliza Mimi nitakuambia huyo asiyekua lolote wala chochote Leo ndio mzuri na ukishirikiana na Mungu vizuri unaweza kumtengeneza akawa unavyotaka na anachotakiwa kuwa kirahisi sana kuliko yule ambaye ameshatengenezwa usivyotaka. Mimi kama Fundi ukiniletea hicho kitambaa ambacho hakijashonwa ni rahisi kutengeneza unachotaka kuliko ukiniletea nguo ambayo ilishashonwa kitu kingine niitengeneze iwe kitu kingine. Huyo mwanaume asiye na chochote Leo ni kitambaa kipeleke kwa Fundi anaitwa Yesu akutolee style moja matata itakayokutosha katika hali zote ambayo macho hayajawahi kuona, masikio hayajawahi kusikia wala akili za mwanadamu hazijawahi kufikiria Yale mambo Bwana amewaandalia wampendao.

#mchungaji anapokua Fundi cherehani hata kwenye vitambaa vya kushona anapata mafunuo#
#kila jambo lina majira, hata kukosa kuna mwisho hatakua maskini milele, usimdharau#
#pastors new day church, power house#
#victoria petrol station#

“ASANTE MUNGU” Maana yatupasa kushukuru kwa kila jambo

Kuna tajiri mmoja aliamka asubuhi akachungulia dirishani na kumkuta Maskini mmoja akiponda kokoto, alitema mate chini kisha akasema ee mwenyezi Mungu wewe ni mkuu mno nakushukuru sana Maana Mimi si kama huyu Maskini anayeponda kokoto hapa.Akisha kusema hivyo alimkejeri yule Maskini huku akimwambia we choko lazima ufe mapema. Lakini yule Maskini alimuangalia kwa uchungu kisha akasema, yeye anayenifanya niwe hai mpaka muda huu ndiye aujuaye hata mwisho wangu.

Mwanafunzi mmoja alifaulu peke yake darasani huku wenzake wote wakifeli lakini hakujisifu kwamba ana akili sana bali alipiga magoti akamshukuru Mungu akisema asante Mungu maana hii ni neema tu na wala si ujanja wangu.

Askari mwingine alinusurika vitani baada ya wenzake wote kuteketezwa, yeye hakujigamba kwamba ni mpambanaji sana bali alinyenyekea mbele za Mungu akasema asante Mungu maana wewe ndiye unayenipigania.

Mama mmoja alifiwa na mumewe akisha kulia sana alijifuta machozi yake huku akisema asante Mungu kwa yote haya yanayonipata Maana wewe ni mume wa wajane utanifariji.

Dada mwingine alisalitiwa na mpenzi wake lakini wala hakujiua bali alimshukuru Mungu huku akisema asante Mungu maana najua utanipa mume mwema.

Kaka mmoja alikataliwa na mpenzi wake na kukanwa hadharani lakini hakufa moyo bali alisema asante Mungu maana ndiwe utakaye nipatia mke mwema.

Mtu mwingine alikuwa msibani akiomboleza na kulia sana huku akisema asante Mungu maana najua unanipa wewe neema hii ya kuishi na siyo kwa nguvu zangu.
Picha credit: unknown
Kuna yatima walitengwa na ndugu zao na kudhurumiwa haki zao lakini hawakujikatia tamaa Maana walimshukuru Mungu wakisema asante Mungu maana tunakufahamu yakuwa wewe ni baba wa yatima utatutetea..

==>Hata wewe uliyeusoma ujumbe huu sema "ASANTE MUNGU" Maana yatupasa kushukuru kwa kila jambo, kumbuka hata huu uhai tulio nao tunapewa bure na wala hatuulipii.

*** Source unknown. Copy and paste  from Facebook ***

Nilifundishwa…………..!

Soma Comments kwa Masomo Mengi zaidi......

Continue reading Nilifundishwa…………..!

“watu wema wengi huishia kuwa na sifa ya UBAYA vinywani mwa watu lakini kwa kuwa MUNGU NDIE ANAELIPA!!”>>>> Zamaradi Mketema

Tenda wema unavyotenda, kuwa mwema unavyokuwa, mpende binaadamu unavyoweza, muoneshe kumjali kupitiliza, niamini kitu kidogo kitamsahaulisha yote makubwa tena hakuna ajabu kukuta kinachomfanya akuone mbaya ni haki yako, hakuna anaefanya jema kwa mtu ili alipwe, ila kuna ile hali ya KUONA na kuthamini juhudi anazofanya mtu ambapo hiyo inapokosekana ndio unakuta mtu unakuwa dissapointed kwa namna fulani, maana mara nyingine mtu unatoka hadi nje ya njia zako kumridhisha mtu ama hata kujinyima mara nyingine ili wengine wafurahi hata kama ni kwa kidogo, huenda ndio uwezo wako ulipoishia, lakini hakuna hisia mbaya na zinazoumiza kama kujihisi HUTOSHI ama huna unachofanya hasa kwa mtu ambae deep down unajua unafanya nini na unajali kiasi gani. Nilichogundua ukiwa mwema sana unaowafanyia mara nyingi wanakuonea, watakugandamiza, wata-take advantage of you na zaidi watavuka hadi mipaka yako mara nyingine hata kwa vile vitu vya kutumia tu akili, kiufupi watafanya hadi yale ambayo kihalali wasingeweza kuvumilia kufanyiwa na watu wengine na ukiongea ni KOSA, unakuwa mbaya, tena mara nyingine unaweza hata ukanuniwa, wanataka hata wanapokugandamiza unyamanze UKAE KIMYA hata kama ni haki yako kuongea. Ikikutokea usiumie na wala usiache kutenda pale inapostahili, watu wema wengi huishia kuwa na sifa ya UBAYA vinywani mwa watu lakini kwa kuwa MUNGU NDIE ANAELIPA!! Usiache kujitoa, uzuri yupo na ANAONA!!

Kuwa muungwana kwa maisha yako ya baadaye na sio maisha yaliopita!

  Nimekutana na hii topic huko Instagram nikaona ni share nanyi! Inasema kuwa acha kujaribu / usije jaribu kufanya biashara na mtu ambaye mmeachana (ex)  au hata kujaribu kuwa marafiki kwani ndio maana kuna mke/ mume tafuta wako ufanye naye biashara! Kuwa muungwana/ mkarimu kwa maisha yako ya baadaye na sio maisha yaliyopita! Let bygone be who she / he is! Tafuta mwenza wako ndo mfanye naye biashara! Kuna wengine inatokea wakaachana na bado wakaendelea kufanya biashara pamoja. Lakini kundi la watu hao ni wachache sana! Hata Beyonce alimfukuza baba yake u-Manager baada ya kuachana na mama yake Beyonce sasa sembuse wewe?! ……………”Stop trying to do business and be friends with your ex.  There’s a spouse for that. Get one! >>>>> Be loyal to your future not your past!”>>>>>> AskcheyB

Je! nawewe ni kama mimi?

What's up with my hair ???Nauliza kama kuna mtu mwenye mtazamo kama wangu! Mimi picha is all about memory / memories captured! Its more about the "moment" than the look! Yani naweza piga picha katika hali yoyote ile; niwe nimevaa vizuri au la! Niwe nimepaka makeup au la! Ilimradi kuna kumbukumbu itakayotokana na hiyo picha kupigwa mie huwa sijali! And I can share it! Because I'm a real person comfortable in who I'm! Mimi napenda sana memories za picha. 
Sisi tulizaliwa kwenye familia ambayo by then haikuwa na uwezo sana lakini Camera was around our home! Baba yetu anapenda sanaaaaaa picha yani sasa hivi ni uzee na majukumu mengi ndio yamemfanya a-slow down! Nafikiri mimi nimeiga hako katabia ??? .........

Sisterhood
 Trust me, sijui ninesha mtumia "Muhaya" picha ngapi but I normally don't care how I look mpaka siku hizi kanizoea (I guess) ??? au ndio mambo ya "kunyapia nyapia" makaratasi ya Ujaluoni hivyo hana budi ?? Haki vile umeshawahi ona wale watu haswa wakina dada /wanawake ambao hawawezi weka picha zao kwa social media mpaka ziwe "perfectly fine"? Yani hata kama ni ndugu yake amevaa siyo kulingana na hadhi atakayo yeye basi hiyo picha au hizo picha hamta kaa mzione kwa social media! 
Hawa ndio wale watu ambao ndugu zao wote ni wenye pesa, wasiopitwa na fashion ya nguo yoyote, wenye kupaka makeup 24/7 yani those kinda diva-ish behavior kama Mariah Carey! Na, hizo tabia zina wa-cost sana! Unaona jinsi Mariah Carey pamoja na uzuri wake na pesa alizonazo bado Nick alimuacha? Akasema I can't take it anymore! Haya juzi juzi tu hapa akampata kijana Bilionea akamvisha na pete ya uchumba naye baada ya mwaka mmoja kamwaga manyanga ?? (tazama video hapo ??) .....sasahivi kaishia kum-date back dance wake ????

Personally, I'm allergic to "Divas"! Kuna tofauti ya mtu kuwa classy na mtu kuwa Diva! Kwamfano, Zari is very classy but she ain't a Diva! Ndio maana unamkuta anaweza kwenda kokote na ku-cop na watu wa aina yote! Hili hata kwa Wema Sepetu pia, she's  not a diva! But Wema lacks CLASS au naweza sema ameshindwa kuelewa where / how to apply it though she's  down to earth. 

Anyway, wenyewe wanasema hivi "Fake people have an image to maintain and protect. Real people just don't care"! ?? #BeReal

“Usiache kumsifu kwa UKUU na UTUKUFU wake pale unapobarikiwa.” -Zamaradi Mketema

Kuna kipindi unasali sana KUOMBA, halafu kuna kipindi unasali sana KUSHUKURU, katika maana maombi yanakuwa machache na shukran zinakuwa nyingi zaidi, na hapo ndipo unapogundua MUNGU ametenda kitu kwako. kama uko kwenye position ya kushukuru endelea na usiache wala kupunguza speed, kama ulivyokazana kwa machozi mbele za MUNGU kuomba akutendee basi lia kwa machozi ya furaha na shukurani mbele zake kwa miujiza aliokuonesha, muombe MUNGU alinde hizo BARAKA zinazokufanya ushukuru, usiache kumsifu kwa UKUU na UTUKUFU wake pale unapobarikiwa.

“Unajilalisha macho na njaa kujenga ukifa watoto wanauza wanagawana na kula batazzz”–Lemutuz

Live at my MBWENI Plot...hahaha...huku tumemaliza Ukuta U know ...Mwanaume kujenga nyumba ni muhimu sana ila lazima kujipanga kwanza sio kujikosesha maisha kisa kujenga ....hahaaha...unajilalisha macho na njaa kujenga ukifa watoto wanauza wanagawana na kula batazzz ...jipange inawezekana kujenga huku unakula Maisha like me ...hamna haraka ....ok guys vipi MAJIRANI MPO? KAMA NI JIRANI YANGU HAPA MBWENI Karibu na Shule ya Komba check me out TIFAHAMIANE U KNOW!....hahahahaa ...I lov it! - le Mutuz Nation

“Mambo ya kuishi kwenye lijumba halijaisha na Friji limejaa maji HAPANA! not for me!” – le Mutuz Nation

EXTRA LIVE STRAIGHT TALK:- Nimesikia maneno mengi sana ya kujaribu kubadilisha Hoja yangu ya Msingi kuhusu kujenga nyumba ninasema tena kujenga nyumba ni jambo Muhimu sana na Bora sana ila kujenga Nyumba kama Elimu huwa sio la kila mtu kuna wanaotakiwa kulifanya lakini sio wote na inatokana na MIPANGO KWANZA .........Kwa bahati mbaya sana Wabongo tumeliweka hili la kujenga mbele sana mpaka tunaishia kushindwa kuishi Maisha yetu mpaka tunashindwa ku enjoy our lives kisa kujenga tu that I am against ...

Kama ni mfanyakazi ili ujenge nyumba unatakiwa upate mkopo na ni lazima uwe na kazi nzuri yaani umesoma vizuri so unaweza kuutumia ujira wako kwa maisha na kubakisha akiba ya kujenga smoothly sio kukosa maisha watoto wako wanateseka kisa kujenga nyumba HAPANA! ...na ndio hizo nyumba sasa hivi zinauzwa kila kona tena kwa bei poa kisa wenye majumba walikuwa wapiga dili Makazini sasa toka Magufuli awe Rais hamna madili tena mshahara hautoshi unaanza kurudi tena ulikotoka na ambako ndiko you belong kupanga kitu ambacho ulitakiwa kutumia akili mapema sana ukaenda na maisha pole pole ...

Kwa mfano mimi nilijenga nyumba nikiwa Majuu baadaye nilipokuja kupata akili ile pesa ningeweza kununua nyumba Majuu nikaiuza kwa pesa ndefu sana wakati nimeamua kurudi bongo ningeweza kujenga nyumba hata Tatu kwa pesa ile ile ambayo sasa hivi imekaa tu pale Kinyerezi for nothing ...now kuna Elimu yako na ya Watoto ambayo n muhimu sana kuliko hata Nyumba si mnawaona watoto wa wenye nyumba mlizopanga hela za kodi hazitoshi kwa mwenye nyumba kuishi vizuri na familia yake wanaishia kukimbizana na Wapangaji kuongeza kodi kila siku .... Again ninasema kila mtu na maisha yake ila mimi binafsi nitaendelea kukaa nyumba ya kupanga hapa Downtown huku nikiendelea kuwekeza na kujenga Nyumba mpya Mbweni na nitaachana na ya Kinyerezi lakini siwezi kujinyima maisha yangu kisa kujenga nyumba Mbweni HAPANA! no way ...nitapigana na maisha kupata mapato ya kutosha kuishi vizuri sasa hivi as I do and then nitaangalia kama zinatosha akiba ya kujenga pole pole lakini cha msingi ni kwanza kuishi maisha mazuri sasa hivi mambo ya kuishi kwenye lijumba halijaisha na Friji limejaa maji HAPANA! not for me! - le Mutuz Nation