All posts by Alpha Igogo

A word of wisdom

FB_IMG_1451174733834

Family time-the Igogos

FB_IMG_1451933181067Ha ha ha! Leo nakupeleka kijijini kwetu Utegi, wilayani ya Rorya. Hapa kuna baba yangu mdogo, mama zangu, dada zangu, na bibi zangu. Yani wamenikumbusha kwetu! Kwenu ni kwenu hata kama nyumba za manyasi ati! Kheri ya mwaka mpya ndugu zangu, mbarikiwe sana

Happy New Year: The Bereges

FB_IMG_1451759173501Hawa naona wao walikula  Christmas na New Year kwa jirani zetu huko Zambia. JB (Jimmy Berege)  far right, ni my college mate at CBE, huyo kati ni kijana wake anaitwa Thomas, na huyo mwingine ni cousin-brother. Haya mbarikiwe sana wapendwa.

Family time-the Kakoschkes

FB_IMG_1451933171491The Kakoschkes wakimalizia  vacation yao huko Bangkok. Pendeza sana and Happy New Year

Sister sister! The Sarungis

FB_IMG_1451942742755Hahaha! jamani hawa dada zangu hawa msiwaone hivi! Hawa walikuwa “Homa ya jiji” hapo Dar es salaam na Mwanza yote! Yani watu ambao walikuwa wanakula bata la kueleweka miaka ya 80 mpaka late 90 wanawajua hawa watoto wa marehemu mzee Robert Sarungi! FB_IMG_1451942703804Ndio maana nasema ni muhimu mtu kujitambua. Unaona hawa sikuhizi wamejikalia zao na familia zao mambo ya bata wamewaachia vijana lol! Happy New Year my sisters mbarikiwe sana.

Jipu la leo!

FB_IMG_1451922931019??????????

Sister sister!

FB_IMG_1451919755194Don’t play with wadada kutoka “kanda ya ziwa Victoria” ni warembo kupita kiasi. Just look at them! Hapa walikua wakitalii ndani ya jiji la Oakland Huko LA. Si utani lazima uwe “unajitambua” kuwa na wadada kama hawa! Hey, Yes you! Stop! Wake za watu hawa usilete maswali mengi ?? Mbarikiwe sana dada zangu!

Happy New Year-Tengas

FB_IMG_1451865213988Naona wa kwa Tenga nao walikusanyika kusherekea mwaka mpya pamoja. Nawatakieni Mwaka Mpya mwema, mbarikiwe sana wapendwa.

Mother and daughter moment

FB_IMG_1451792569254Picha yetu ya kwanza kabisa katika kipengele Chetu cha “mother and daughter moment” kwa mwaka huu 2016 inatoka huko Mbagala kwa binamu yangu kipenzi Tabu Obago na binti zake Julieth na Jacqueline.  Hapa walikuwa wakisherekea mwaka mpya. Mbarikiwe sana wapendwa.

Happy New Year: The Sarungis

FB_IMG_1451617820140-1Hivi ndivyo familia ya mzee Prof. Sarungi walivyo funga na kufunga mwaka. Wamependeza sanaaaaaa FB_IMG_1451617820140-1-1Safi sana. Happy 2016 wapendwa.

Happy New Year -mama Pendo na timu yake

FB_IMG_1451865621099Salamu za mwaka mpya toka kwa timu ya mama Pendo. Kwakweli leo ndo nimeona madhara ya watoto wakike  kubadilisha last name zao ?? yani nimeshindwa kabisa kukumbuka ubini  (last name) ya hii familia japo ni watu tunao fahamiana sana kwa zaidi ya miaka 20! Nimejaribu kupekua wapi!! Watoto wakike waliolewa na kubadili majina mwe! Na wengine wanatumia majina bandia,  basi imekuwa ngumu sana kukumbuka ndio maana nimeandika “mama Pendo” kwani n Pendo ndiyo first born wa familia hii. Mama Pendo nihuyo mwenye shortpants  ya pink amemuegemea “barafu” ya roho yake (baba Pendo) FB_IMG_1451865650334pia naomba niseme Happy belated birthday to mama Pendo. Naona watu  wengi wamefungua mwaka na birthday zao pamoja. Ok. Mbarikiwe sana wapendwa.

Happy belated birthday mtani

FB_IMG_1451923126990Happy belated birthday mtani wangu. Natumaini ulikuwa na siku njema na uliuwanza mwaka vyema. FB_IMG_1451923119203Hahahahaha! halafu Wahaya mnavituko yani wewe picha zako zote umepiga ofisini?! Ndo tujuwe kuwa una ofisini au uneajiriwa ??? Nitakomaje sasa kwenye Facebook ??? ole wako unichambe “nitampiga chini” mdogo wako ?? siunajua my future “Denzel Washington” anatoka Bukoba ????  Happy birthday mtani wangu.  Be blessed.

Jipu la jana

FB_IMG_1451764596636???? Wambie hao “vidudu” mtu ???  Jamani hii nimetoa kwa dada Joan yeye ni mtangazaji wa Bahari Fm Radio Zanzibar. Anasema mwaka huu anatatumbua “majipu” na hivi ndivyo alivyo anza ?? siku ya 1/1/2016!  Basi usiwe nahofu mie nitakuletea kila jibu atakalo litumbua ??? FB_IMG_1451922978578

Birthday Boy katika pozi!

IMG-20160102-WA0010-1He he he! Naona mtu kanunuliwa suti mpya na tai, sijui ndio wanajaribu kumwambia “muda wa kuowa” umefika ?? mwe! Huyu mdogo wangu ni mpenda starehe huyu ngoja avute vute muda kidogo ???? tatizo wadada wa “mujini” wamemganda kama ‘ruba’ vile ??? IMG-20160102-WA0005hapa naona yupo na mdogo wake. Wote wamezaliwa December. Soma hapa au hapa kusoma birthday wishes zao IMG-20160102-WA0002-1Haya kaka naona suti zimekukaa kweli kweli ?? lakini yani wewe hata wifi wabandia hukumpata upigenaye picha ?? IMG-20160102-WA0004Blessing sijui alikuwa ametoka kuamka? Maana kanuna lol! Haya nawatakieni Mwaka Mpya mwema. Hope to see you soon maana nimewa miss kichizi ?

Namshukuru Mungu

IMG-20160101-WA0000Namshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kumponya mama yangu. Mama alikuwa anaumwa, huwa anasumbuliwa na Allergies pamoja na Asthma huwa anapata tabu sana especially majira ya joto kali.  Hivyo for the past two weeks hali yake aikuwa nzuri sana lakini sasa anaendelea vizuri. Hapo ni siku ya Ijumaa  Mrs Zou Fu Qiang alienda kumtembelea. Yeye ni family friend wetu.  Tushukuru na kuwaombea marafiki wanao chukua muda wao kuja kutujulia hali. Mbarikiwe sana wapendwa. Love you mama!

Hello there!

Happy New Year wapendwa wasomaji wangu! Naomba mnisamehe sana leo nimeshindwa kuleta picha za familia kama ilivyo kawaida yetu. Lakini Nahaidi nitazileta kesho, kwa sasa nimebanwa kidogo. Natumaini mmeanza mwaka vyema.  Asanteni sana.

FB_IMG_1451841713620#TBS#Home,02/2010 Nilikuwa likizo Bongoland na hapo nilikuwa nakwenda kula “bata” Hiyo nguo bado ninayo ila sijawahi ivaa tena sina uwakika kama bado inanitosha ? I love that color is one of my favorite colors. Haya Muwe na siku njema.

Nawatakieni Mwaka Mpya mwema!

Screenshot_2015-12-07-19-41-52-1Wapendwa wasomaji wangu, ndugu, jamaa na marafiki. Napenda kuwatakieni kheri ya kuufunga mwaka 2015 na kufungua mwaka 2016. Nasema asanteni sana kwa kutembelea hii blog bila kuchoka, sina cha kuwalipa zaidi ya asante. Naomba mnisamehe wale wote niliyo wakwaza kwa namna moja ama nyingine. Sidhani kama nilikusudia kumuumiza mtu na sina huwakika kama nimemuumiza mtu yoyote! Lakini kama binadamu huwezi jua hivyo najishusha kwa kusema I am sorry! Tuzidi kupendana, tuombeane, na tutakiane mema siku zote! ……………….Mdogo wangu ? Blessing naye anawatakieni mwaka mpya mwema. Anasema yeye ni mpenzi wa hii blog hivyo siku zote anatembelea na kuwasoma hapa kwa kutumia mtandao wenye mawasiliano na Internet ya kuaminika. #Halotel ndiyo habari ya mujini na vijijini!

Nawaacheni na huu wimbo. Nimoja ya nyimbo ninazo zipenda sana sana. Yani huwa nausikiliza kwenye gari karibia kila siku!

Happy New Year wapendwa. Tukutane 2016 ???

Wimbo nilio upenda zaidi mwaka huu 2015 #Utanipenda?

Screenshot_2015-12-19-18-45-35-1-1Nimeusikiliza huu wimbo zaidi ya mara 20, believe me! wimbo huu una ujumbe mzito sana ambao mtu yeyote yule anayekaa chini na kutafakari vitu haswa watu walio kuzunguka lazima utakuliza! Very touchy song with a Billion $$ question #Utanipenda? Nakuletea behind the scene za wimbo huu na wimbo wenyewe angalia na tafakari sana tunapo malizia mwaka huu na ufanye maamuzi sahii! Je hao watu iwe ni rafiki, jamaa,  wapenzi, n.k waliokuzunguka je ungekuwa hauna hivyo vinavyo wavutia sasa je wangekubali kusimama nawe? Je vipi vikiondoka ghafla wataendelea kuwepo au nao wataondoka? #Utanipenda? Screenshot_2015-12-31-13-36-19-1

#TBT# Mahojiano yangu yamwisho kwa mwaka 2015: Bin Zubeiry

FB_IMG_1437541501275
Najua mimi na wewe tunafamiana toka tukiwa wadogo lakini kwa faida ya wasomaji naomba ujitambulishe maji
na yako halisi:  Asante, mimi ninaitwa Mahmoud Ramadhan Zubeiry,   walizoea kuniita Mudi
Unaweza ukatuelezea kidogo kuhusu elimu yako?  Shule ya msingi nilisoma pale Mgulani, baadaye nikaenada Rutabio sekondari kabla ya kufanya kozi mbili za awali za Uandishi wa Habari MAMET (Maarifa Media Trust), chuo ambacho kilikuwa kinamilikiwa na akina Jenerali Ulimwengu. Baada ya hapo, mwaka 2008 nilipata Stashahada ya Uandishi wa Habari ya LSJ (London School of Journalism) ambayo nilifanya online
FB_IMG_1437541539371
Ilikuwaje mpaka ukaanzisha blog yako na kwanini uliiita binzubeiry?
Baada ya kufanya kazi za kuajiriwa kwa muda mrefu tangu mwaka 1999, katika magazeti ya Dimba, Mtanzania, Rai, Bingwa, The African na baadaye Tanzania Daima na Sayari hapa nyumbani nikaona sasa inatosha. Lazima nisimame kama mimi kutafuta mafanikio binafsi. Ndipo nikaamua kuanzisha blog, ambayo sasa imekuwa tovuti kamili ya michezo, www.binzubeiry.co.tz
FB_IMG_1437541634585
Yalikuwa maamuzi magumu, ambayo mpinzani wa kwanza alikuwa mke wangu, pale nilipomuambia ghafla ninaacha kazi mwaka Mei mwaka 2012. Kama unavyojua mishahara ya kwenye vyombo vya habari hapa nyumbani haitoshelezi kukidhi mahitaji- hivyo niliacha kazi sina chochote. Sikuwa hata na kiwanja. Nilianza blog katika mazingira magumu sana, sina vifaa, nahangaika kusaka habari mitaani. Nilijituma hivyo hivyo hadi blog ikaanza kuvuma hatimaye nikaanza kupata watangazaji, taratibu nikaanza kununua vifaa vya kazi. Alhamdulillah sasa nina vifaa ambavyo ninafurahia kufanyia kazi, kuanzia kamera, MacBook na zagazaga zote. Nipo full, ila tu ofisi bado popote.
FB_IMG_1437544009848
 Hali ikoje leo? Alhamdulillah ninamshukuru Mungu, watoto wangu wane kati ya watano wote wanasoma shule za kulipia, wawili kati wao sekondari kidato cha kwanza (Nurat na Precious). Wawili wapo shule ya msingi darasa la kwanza (Prince Akbar) darasa la pili (Princess Asia). Mungu akijaalia mwakani Sheikh Yussuf (miaka miwili) ataanza chekechekea. Nina shamba la embe ekari mbili eneo la Kigamboni. Nina nyumba Kigamboni huko huko na kiwanja ambacho hakijajengwa bado cha ukubwa wa 40-40. 
FB_IMG_1437543931792Unamagari mangapi? Yapo matatu tu, Passo anayotumia mke wangu, Range Rover na BMW ambazo natumia mwenyewe
Inaelekea unapenda sana michezo, je ulisomea uwandishi wa habari upande wa michezo au ni kipaji tuu ulizaliwa nacho?
FB_IMG_1437544757337
Kama utakumbuka napenda michezo tangu nipo mdogo, nimecheza mpira mwenyewe pale KJ, lakini sikubahatika kufika mbali. Wakati nipo shule ya msingi Mgulani nilichaguliwa na Mwalimu Chale kama unamkumbuka katika kikundi cha Chipukizi, ambao ndiyo tulikuwa Ball Boys wa Uwanja wa Taifa enzi hizo mpira wa Tanzania uko juu sana. Kwa hivyo tangu hapo nikawa mpenzi sana wa michezo. Kwa kupenda kusoma magazeti, nikapenda sana na mimi siku moja niandike. Nilikuwa navutiwa wana na uandikaji wa watu kama Johnson Mbwambo na Francis Chirwa. Nilitamani siku moja niwe kama wao. Nashukuru walikuwa mabosi wangu, walinifundisha kazi katika gazeti la Dimba kwa upendo kabisa. Kama ninasifiwa leo ni Mwandishi mzuri wa michezo, basi kwa sababu nilipitia kwa walimu wazuri hao na wengine wengi kweli. Eric Anthony alikuwa Mhariri wangu wa kwanza pale Dimba. Huyu jamaa alinipiga msasa sana.
FB_IMG_1437544685611Ulipata wapi ujasiri wa kuanzisha blog yako mwenyewe?haswa ukitazama hapo nyuma watanzania walio wengi walikuwa wanafikiri kuanzisha blog ni lazima uwe mtu maharufu au mtu ambaye umetoka kwa familia yenye pesa? Kama nilivyokuambia, niliamua tu kujilipua kwa kuacha kazi na kwenda kujiajiri mwenyewe. Nilijikabidhi kwa Mungu na leo ninamhsukuru sana Mungu kwa kweli. Amenisamamia na anaendelea kunisimamia. BIN ZUBEIRY ndiyo habari mjini
Hii blog unaitumia kama sehemu tuu ya vitu unavyo vipenda au pia ni sehemu ya kujiingizia kipato? Mama hii ofisi, inafanya niishi kupitia malipo ninayopata kutokana na vijitangazo hivyo. Ukiondoa hii tovuti, mimi mkulima na nina mpango kuanza mradi wa ufugaji nitakapohamia kwenye nyuma yangu Januari Mungu akipenda.
FB_IMG_1437541894205
Najua watu wengi hawajui historia ya ulipo tokea ila kwa sisi tulio kufahamu tunaona ni ukuu wa miujiza ya Mungu. Je wewe ulisha wahi kuwaza wakati wa utoto wako kuwa ipo siku moja utaishi maisha haya unayo ishi sasa hivi? Labda udokeze kidogo maisha ulio kulia: Kuna wakati huwa nalia mwenyewe ninapokumbuka nilipotoka, misukosuko na shida za maisha nilizopitia. Lakini mwisho wa siku ninamshukuru Mungu tu, kwani yeye ndiye mpangaji wa yote. Niseme nini Alpha, mimi nimetokea familia ya kimasikini pale Keko wewe mwenyewe unajua. Tulikuwa na maisha duni kupita duni zote. Kuna wakati nilikuwa nakwenda kwenye jalala la soko dogo pale Keko kuokota vilivyotupwa na kutafuta vyenye nafuu ili twende nyumbani kupika kupata chakula. Nilianza kufanya deiwaka hata kabla sijaanza darasa la kwanza, napimisha watu uzito kwa mzani si unakumbuka? Na ni ule mzani ulinosomesha mimi, ilikuwa kila nikitoka shule naenda kusanya, Napata fedha za mahitaji ya shule. Nilikuwa nakwenda kubeba mizigo Kitumbini. Nimepiga debe, nimeuza mitumba minadani. Manyanyaso, chuki na masimango hivyo ni vya kawaida.
2Wewe ni mtu au mwandishi wa habari pekee ulie bahatika kuona gari la kifahari (ambalo ni custom made) la kijana wa Bhakresa; ulijisikiaje ulipo pata fursa hiyo? Kwanza mlifahamiana wapi au ulimjuaje?
6
Yussuf ni rafiki yangu. Tumejuana kutokana na kazi, wao wanamiliki timu ile ya Azam FC. Alipenda ninavyoandika habari za timu yao, akawa rafiki yangu, tumeshibana hadi tumeaminiana kiasi hicho.
5
Na Yussuf pamoja na Zacharia Hans Poppe ni watu wenye mchango mkubwa katika maisha yangu. Hawa ni wafadhili wakuu wawww.binzubeiry.co.tz
8
Ni nini umejifunza zaidi au faida kubwa umepata kutokana na mitandao? Je unafikiri watanzania wanatumia vizuri mitandao?
Nimejifunza mengi sana, nilisahau kukuambia, nilisoma kozi moja fupi pia ya namna ya kuendesha blog mwaka 2012 ilidhaminiwa na SBL (Serengeti Breweries). Kuhusu matumizi, si Watanzania, watu dunia nzima wapo wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii. Na vigumu kuwabadilisha. Hizo ni hulka. Mtu anayejishimu hawezi kuposti picha za ngono. Hawezi kutumia mtandao kumtukana mtu.
FB_IMG_1437541501275Nini ujumbe wako kwa Watanzania wenzako? Ujumbe wangu kwa Watanzania na vijana wenzangu. Wamtegemee Mungu, waache ushirikina. Mafanikio yanakuja baada ya kujituma. Lazima tufanye kazi, tuache majungu. Tanzania itaendelea zaidi, iwapo vijana watafanya kazi kwa bidii.

Continue reading #TBT# Mahojiano yangu yamwisho kwa mwaka 2015: Bin Zubeiry

A word of wisdom

Dr. Ben Carson (Retired world renowned neurosurgeon, and Republican Presidential Aspirant) wrote this beautiful piece. Read and be blessed……… FB_IMG_1451232210742

“Sometimes you are unsatisfied with your life, while many people in this world are dreaming of living your life.

A child on a farm sees a plane fly overhead and dreams of flying. But, a pilot on the plane sees the farmhouse and dreams of returning home. That’s life!! Enjoy yours.

If wealth is the secret to happiness, then the rich should be dancing on the streets. But only poor kids do that.

If power ensures security, then officials should walk unguarded. But those who live simply, sleep soundly.

If beauty and fame bring ideal relationships, then celebrities should have the best marriages. But those who live simply, walk humbly and love genuinely!

All good will come back to you!!!

Man asks, “Where was God when Myles Munroe, wife and his associates were killed in a crash? He answers, “The same place I sat when John the Baptist my servant was beheaded. When Stephen my servant was stoned to death. When Paul my servant was murdered in Rome. The same place I sat when my only Son was brutally crucified, wounded, bruised and killed. I have not moved from my position.” I am the same. It is not the means of exit from earth that matters but the destination. Live simply. It’s all about God!!”