Category Archives: Beauty and fashion

Malia Obama ndani ya “hot topics”!

Ule usemi uliotumika sana na  wahenga wetu kuwa “mtoto umleavyo ndivyo ukuavyo” unaweza usilete maana sana katika kulewa watoto wa karne hii ya 21! Hivi karibuni kama wiki na siku kadhaa zilizopita binti wa Mstahafu Rais Baraka Obama, ajulikanae kama Malia Obama alikutwa akibusiana na mwanaume ambaye aliaminika kuwa ni boyfriend wake katika viwanja vya chuo kikuu cha Harvard university na pia alionekana akivuta sigara. Tazama kwenye hii video kuanzia dakika ya 22.50 kama inavyoelezewa na gwiji wa “hot topics” Wendy Williams  ?

Sipati picha Michelle Obama alikasirikaje, unaweza zimia bila “kizimio” ?? Halafu sasa kutokana na sheria za huku Malia Obama anatambulika kama mtu mzima ambaye anaweza fanya maamuzi yake binafsi na wazazi wanatakiwa kuyaheshimu! Najua hata Africa ukishafika 18+ unatambulika wewe ni mtu mzima kwenye karatasi za serikali lakini kiuhalisia wazazi wetu wengi bado wanakuwa na mamlaka juu yetu na kutufanyia maamuzi mengi juu yetu. Ni mfumo wa tamaduni zetu ambao unafanya watu wengi kutokuwa na mawazo huru na kufanya maamuzi ambayo yanampendeza yeye na kwafaida yake kwanza. Funguo za furaha zetu zipo mikononi mwa watu kama wazazi, marafiki, na jamii na ndio maana wengi ni wanafiki na waongo kupita kiasi!  Lakini vile vile lazima tukubaliane kuwa kila familia lazima iwe na identity yake! Kila mtu anazaliwa tofauti lakini kama familia lazima muwe na kitu kimoja ambacho watu watajua na kuwatambua nacho. Hivyo sishangai kwanini Michelle na Baraka wamekasirishwa na kitendo hicho. ……..Mungu atusaidie sisi ambao tunataka kuzaa na wale ambao wanalea katika karne hii ya 21 kwani changamoto ni nyingi mno!

Mama na wanawe! …..The Mashimi!

Mama na wanawe, the Mashimis’ katika ubora wao. Honestly nilikuwa napenda sana kupost family moments kama hizi because I strongly believe in family institution. Lakini wapika majungu na kamati ya ufitina wakaanza kupika majungu nakuwajaza watu hofu kiasi kwamba watu wakawa hawataki kuweka picha zao kwa hii blog. Hivyo siku hizi naweka only picha za watu ambao najua hawatakuja kusema “toa picha zangu kwenye blog yako”! Unless wewe mwenyewe uniruhusu, sito weka picha za watu humu. Ni za familia yangu na watu ambao najua they won’t bring drama to me!! Sitaki drama mimi I am too old for that crap!…….Anyway, nimependa hii picha, ni the Mashimis’ from Atlanta, Georgia. Wamependeza sana na ninawapenda ?❤

JNM: Where there’s passion, perseverance and dedication there’s always a reward. Keep going!

“Where there’s passion,perseverance and dedication there’s always a reward. Keep going!” ———-JNM

Cookie Moses Iyobo nionee huruma mwenzio!

Jamani Cookie binti wa Moses Iyobo na aunty Ezekiel ni nini unanifanyia mwenzio! Embu nionee huruma my darling, wewe hujasikia wenzio ndoa zinavunjika hawataki kuzaa kwa uchumi huu wa Babu yako Trump na Dr. Magufuli ?? maisha magumu  mwanetu ??.   

Tatizo ni jinsi wewe ulivyo mzuri yani mpaka unanitia katika vishawishi  mwanangu wee! Nitakuwa mgeni wa nani mie maisha yenyewe haya ya paycheck to paycheck, Niki miss paycheck moja tu nakuwa homeless  ????????‍♂️ You are beautiful and photogenic fulani amazing kweli kweli! Mungu akulinde, ukuhepushe na manyang’au ya hii dunia! Amazing! BTW, happy belated birthday mama Cookie, Ubarikiwe sana.

Zarinah Hassan: We have been created so different, the type of humans who can multi task

“There is so much in a woman that most people don’t know. We have been created so different, the type of humans who can multi task. A man can watch a game and not hear what one said while a woman can watch a movie and still hear, still know the stove is on, and so on (the list is endless). So here is to all the multi tasking women juggling through life as mothers, wives, momprenuers aka business women, caregivers and many more. You are appreciated! It’s all about knowing what comes 1st #prioritize. Salute? help me tag one woman who inspires you. @lukambaofficial ?” ——-Zarinah Hassan

Mr and Mrs Mkandamizaji

“About last night with my 1 and ONLY Monica. Ni katika harusi mtu mfupi ya JOT!! Shukran KAMILI Kwa Dada Yangu wa ukweli @isariaclothingboutique @isariaclothingboutique Kumnogesha Msukuma wangu?? #JamaniMsukumaRutubaImemkubaliiiMweeeeeh?????????# #HiiInaitwaMboleaYaKukuzia#” ~~~~~ Masanja

Masanja mkandamizaji na Monica wake! Wamependeza sana! Hongereni kwa hiyo zawadi aliyobeba Monica tumboni mwake. Mungu awajalie ajifungue salama na mtoto mwenye afya njema!…..sijui nitabiri ?? natabiri mtoto wa Kiume ??

 

RARE Magazine yatumia page mbili kuandika ‘Bio’ ya LB!

Kwakutumia social media accounts zake Linda Bezuidenhout alielezea furaha yake na kumshukuru Mungu kwa mibaraka hiyo kama unavyosomekahapa chini ? “Wow! Please zoom to read my bio and all the achievements Thanks to God Alhamdulilah ??. My bio keeps growing we now need 2 pages to complete all the awards and achievements WOW! The RARE Magazine based in NY used 2 pages just for my bio and other pages for my designs….. please if you haven’t seen the cover of the magazine with an LB dress go to @linda_bezuidenhout_couture …soon we will add the resent events on our website which are among the major events we participated (LB COUTURE ) My Accolade Media Award and to showcase for 50 Shades Of Pink.
One more Amazing event to come for this year InshaAllah ?? God Willing. Listen ? everybody Listen!! THANKS FOR YOUR LOVE AND SUPPORT. MashaAllah Bio yangu na matukio makubwa niliofanya ni mengi mpaka ina chukua kurasa mbili kwenye gazeti. Hilo kwenye gazeti kubwa sana la NY. Tukuio na tunzo niliopata za juzi juzi hatujaweka bado kwenye website … InshaAllah kuna tukio lingine kubwa moja kwa mwaka huu limebaki ??. NAWASHUKURU KWA MAPENZI YENU NA SUPPORT YENU ??” LB  Nami napenda kumpongeza sana Linda kwa mafanikio haya. Kweli Mungu si Athumani, nani alijua kuwa “Fundi cherehani” anaweza kutumia page mbili kuandikiwa Bio! Very inspiring! Ubarikiwe sanaaaaaa! ??

The C.E.O herself! #Molocaho

Nani Kama Jacqueline!! The C.E.O of Molocaho furniture katika ubora wake!  Nampendaje sasa!! Mzuri wa sura, shepu, mpaka roho! Kuna wanawake wengine japo ni wazuri wanavutia lakini usiombe ukae nao karibu utajuta!! Wana roho mbaya mfano hakuna, hawapendi kuona wengine wanafuraha kwani maisha yao ni vilio kila siku!! Halafu maendelo ya wengine ni chungu kwao kumeza kama mwarobaini!! ……Ubarikiwe sana Mrs Billionaire ?? 

Mr and Mrs Kimesera katika ubora wao!

Awiiiihh! Wamenoga eeh!! Wow! Super cute, couple yangu ya ukweli hii! Yani wanavutia na kuwapa moyo wengine kuwa True Love still exists ?? Kama wewe ni mgeni basi naomba ujua kuwa hi couple ndio ilikwa my 2016 Hottest And Best Couple Of The Year (SomaHapa). Nawapenda sana ??………Baadaye kuna post inakuja ya kuipongeza LB kwa award waliyo pata. Sasa hivi nipo busy kidogo hivyo naishia hapa!

Winny Edwin Kihore: Living in love

                                      LIVING IN LOVE
 I once heard about a husband and wife who were so upset after a big argument that they refused to speak to each other. That night, not wanting to be first to break the awkward silence, the man left a note on his wife's side of the bed that read, "wake me up at 6 o'clock in the morning ". The next morning, by the time the husband woke up, it was already 8 o'clock. Furious, he roared, "where is she?" and was about to chew out his wife when he found a note on his side of the bed : "lt's six o'clock; wake up." If we're going to live in love, we have to learn to forgive one another. The Bible says, "Do not let the sun go down on your anger, but instead, forgive. And above all things, put on love. " EPHESIANS 3:17- That we would be "rooted and established in love so that we would have power together with all the saints " when we choose to walk in love, we have the power of God in our lives, as well as healthier relationships. We should always look for the best in each other. That's one of the things l love my husband Edwin Kihore. I used to think that he didn't see the things that l did wrong. Then l realized: it's not that he doesn't see them ; he choose not to focus on them. Let 's learn to walk in love and see the best in everyone. A house divided will fall. That's why it's so important to keep peace in your home. Be the first to apologize. Be quick to forgive. You need to remind yourself that God has put that person in your life, and He's got good things in store. If you will do your part by being kind, respecting one another, treating each other the way you want to be treated, God will do his part, and you can live in love!

Mother and daughter moment!

Mama Gabby na Gabby wake! Beautiful pic

Quote for today: You’re the most beautiful thing I keep inside my heart!

Okay!! Major General, what is real going on?!

First of all, I love your conservative-modesty look! Umependeza sana but nywele not feeling it lol!……… Secondly, what is really going on Major General!?! So many rumors are going on, from “it might be over” to ” DNA has proven the baby boy is not his”!! As your fans we really deserve to know the truth, only from your mouth! And some of us don’t do “snapchat” thus better be an interview or. Live Instagram video ?? Please, we need to hear from you!

Jacqueline Mengi: Apendwae akajua haachi kujishauwa!

If the only prayer you said in your whole life was “thank you” that would suffice. Meister Eckhart

Nimekwenda kwenye Instagram page ya Jacqueline Mengi nikakuta ame post msemo huu “Apendwae akajua haachi kujishaua”!………… Kwakweli hata mimi nakubaliana na huo msemo! Raha sana kupendwa na mtu anayekupenda kwa right reasons and in a right way!! Kuna watu wanaweza kukupenda in a wrong way kama Bobby  Brown na Whitney Houston! Bobby Brown alikiri kuwa alimpenda Whitney Houston but he didn’t love her in a right way!! Sikiliza sehemu ya hiyo interview hapa ??

Hapo ni vile mtu anakupenda lakini anashindwa kukukataza au kukuzuia kwenda kwenye njia mbaya badala yake na yeye ana support njia zako mbovu in the name of “LOVE” halafau wote mnaangamia. Sasa kwa hawa aliye salimika ni Bobby peke yake Whitney na binti ya ke BobbiChristina wakafariki kwa drugs….. Mtu anyekupenda katika njia sahihi na kwa sababu zilizo sahii siku zote ata wish to see the best of you! Mtu huyo atapigana mchana na usiku kuwakikisha hauingii gizani na kupotea. ………Hivyo ukimpata mtu wa namna hiyo huna budi kushukuru Mungu na kama binadamu basi kujishaua lazima!…….. Wewe jishaue tu Mrs Billionaire, acha wenye wivu wajinyonge tu ??? kama hawana kamba tutawanunulia waseme tu ???

“good things come to those who hustle” ~~~~~ Major General

 “Last thursday of the month, not sure what motivation is needed but I know i gotta put the past behind me and focus on the future…. good things come to those who hustle #WorkMode”~~~~Zari. a.k.a  Major General

Mmesikia? “Mke mzuri halindwi”!!

Wahenga waliyaona na kushuhudia kuwa ni ukweli haiwezekani, ndio maana wakatoa “angalizo” au muongozo ili vijana wanaokuja wajifunze bila kufanya makosa!……….Sasa Wahenga walitoa angalizo kuwa “mke mzuri halindwi”!! Mke nzuri anahitaji MATUNZO NA HESHIMA basi wala huangaiki naye anatulia ndani ya nyumba anapendeza kama waridi!! Sasa wewe unadai unamke mzuri halafu amani rohoni hauna umekuwa FBI wa penzi lako mwenyewe? Inahusu!?! Mke nzuri muwekee mazingira mazuri ya kuishi kama haya ya Jacqueline, kiyoyozi masaa 24, maji safi ya kunywa na kuoga unafikiri atatoka? Aende wapi?! Sasa wewe mke mzuri halafu unampangia chumba uwanja wa fisi karibu na “corner bar” utafikiri alikwambia yeye Bar Maid ??? halafu wewe ndio mkali mtu asipite karibu yenu ??  Jamani mke anahitaji matunzo nyie wanaume! Mke anahitaji heshima, sio kumchanganyia wanawake kila asubuhi!! Yani hata heshima kwa wanawake wenzake hapati kwasababu ya mumewe!! Embu muige mfano hapa!! Hata kama hauna hela ya kumjengea nyumba kama hii jaribu kumuonyesha thamani yake kwa kumuwekea mazingira fulani mazuri! Kha!……( tuache matani Jacqueline mzuri eeh)  That Foyer is one to die for kwakweli! Your house is beautiful! Safi sana!——–‘ Btw! Jacqueline, kwanini usinunue Miss Tanzania? Naamini wewe unaweza ukayapeleka na kuyapa hadhi yanayostahili kwani uwezo wa kupata sponsors wa uwakika unao! Embu tafakari Miss wetu! Ongea na Dr. Mwakyembe na Lundenga uyachukue mpendwa! ??

The Queen herself!…….. Ujumaa njema/ weekend njema wapendwa!

@aminadesign @laviemakeup…. Was great working with you, awaiting this project

Nawatakieni Ijumaa njema na weekend mjema. Embu tufunge wiki na hizi picha za Queen, the one and only one BossLady! Pendeza sana ❤❤…………Sorround yourself with love, wenye roho za kwanini kaeni nao mbali lakini msiwasahau kuwaombea!  Continue reading The Queen herself!…….. Ujumaa njema/ weekend njema wapendwa!

Martin Tiho ashirikiana na Jokate kuanzisha “Sauti Ya Watu Wenye Ulemavu”!

Mr. Martin Tiho na Jokate Mwegelo

“Nikiwa na rafiki yangu Martin Tiho niliyekutana nae kwa mara ya kwanza miezi miwili nilipofanya ziara katika ofisi za New Habari Sinza jijini Dar es Salaam, alikuwa anasambaza CD za filamu aliyoigiza na kutengeneza mwenyewe. Tukabadilishana mawasiliano baada ya kununua CD yake na kuahidi kushirikiana nae. Ameanzisha kampeni yake ya “Sauti Ya Watu Wenye Ulemavu.” Na hivi karibuni tutawaletea tshirt kama njia moja wapo ya wewe kuchangia katika project yake. Nilimwalika aje tupige picha za pamoja. Picha hizi zitakuwa kwenye tshirt zake. Karibuni. Usengwile.” Jokate Mwegelo

Yessss! Jojo is back!

Proudly made in Bongo Land @mac_couture ?❤️. I love the clarity of this pic shot by the kid @m.a.k.u.n.g.u and of course the flawless hair and make up by Dada Deee @americannailstz
Miss Jojo. Dress By @mac_couture Image Shot By @m.a.k.u.n.g.u ?❤️??
I missed y’all walahy. So I’m happy I’m kinda back, ??‍♀️. That billion ? smile shot by the baddest @m.a.k.u.n.g.u
Huwa napenda ku-support vipaji vipya kwenye tasnia hii ya ubunifu wa mitindo Tanzania. Leo nawaletea huyu @mac_couture nguo anashona mwenyewe. Beautifully and wonderfully made in Tanzania ?????‍♂️

I’m super happy my beautiful, smart, elegant, kind, loving, and “environmental friendly” babysister is back just like the way I wished!! ?? Yes! Such an environmental friendly lady; wanawake wengine ni hatari kwa mazingira yetu tunayo ishi!! Maongezi yao yamejaa chuki na uchochezi tuuu! Kazi yao is to pollute hali ya hewa ili kila mtu awe miserable kama wao! Wanawake kama Jojo ni wanawake adimu sana siku hizi! Woman with class!…….so happy! Welcome back baby girl you look AMAZING! Gorgeous is understatement kwakweli……….. We love you Jojo!?? ??

 

Womanhood!

It doesn’t matter how bad your day is, BE NICE to everyone, you never know what type of help God is sending your way . #happysundayeveryone ? #millenmagese⭐️??

Vazi la Michelle Obama laleta tafran’ kwa Facebook!

Mtoto wa aliyekuwa Rais wa Marekani kabla ya Donald Trump, Malia Obama asubuhi ya leo alipost picha ya mama yake akiwa vacation kwenye visiwa fulani huku akiwa amevalia vazi la ufukweni. Mama Obama alionekana kama alikuwa anapanda kwenye boat ambapo upepo ulipuliza na kuacha sehemu kubwa ya mapaja yake wazi. Kuna watu ambao hawakupendezwa na hiyo picha kuonyeshwa kwenye public, kuna wengine hawakupendezwa kwa jinsi alivyo vaa mbele ya macho ya watu wengi wameona kama hastahili kuvaa hivyo kwani ni mtu ambaye anaheshimika sana na alikuwa First Lady wa Marekani. Mmmh! Embu wee tizama picha halafu useme jinsi uonavyo; mimi sijaona ubaya wa hiyo picha kwani vazi lilikuwa sahihi na alipokuwa. Nilisha sema huko nyuma (SomaHapa) picha kama hiyo kuwekwa kwa public ni maamuzi binafsi na ujasiri wake. …… Maoni ya watu yapo kwa lugha ya English kama uwelewi basi tafuta mtu akutafsirie!

Baadhi ya maoni: