Category Archives: Elimu juu ya maisha

Mc.Pilipili: HUU NI UKICHAA WA MAPENZI

Regranned from @mcpilipili - HUU NI UKICHAA WA MAPENZI. ?Kushika mimba ukadhani ni mtego ili uolewe.
? Kutafuta mkamilifu wakati tabia zako tunakuvumilia tu.
? Kutafuta msichana mrembo wakati huna pesa.
? Kutafuta mke mwema kanisani wakati we unaenda kanisani wakati wa maombi ya Christmas tu.
? Kusema wanawake wote sawa.
? Kuendelea kuchagua wanaume wakati unajua waoaji siku hizi wachache.
? Kuishi na mpenzi wako kabla ya ndoa, unamfulia, unampikia na unampa penzi wakati unajua hujulikani kwao, ukiachwa unatafuta ushauri mitandaoni.
?Kusema umeokoka lakini unazini na mchumba kama kawaida kwa kisingizio kwamba soon mtakuwa mke na mume!
?Kuogopa kuongozana na msichana au mvulana eti mtaingia majaribuni, unajua kutamani tu ni uzinzi?
? Kufikiri kwamba utampata mtu mwenye sifa mia nane unazozitaka labda umuumbe mwenyewe!
?Kujifanya unapendwa wakati moyoni unajua wazi mtu kakuchoka, na amekwambia kabisa anatafuta mtu mwingine!
? Kumhonga mwanaume ili akuoe!
? Kudhani kwamba kutoolewa ni laana, hii ni bangi mbaya!
? Kumtongoza mchumba au mke wa rafiki yako!
? Kuoa wakati huna kazi /chanzo cha kipato!
? Kufikiri eti wanaume wa kiafrika wanaweza kufanya mambo ya kwenye tamthiliya za kifilipino.
? Kumsomesha mtu ili uje umuoe!
? Kumng'ang'ania mtu asiyekupenda, utazimia ukialikwa harusini!
?Kuwaeleza mashosti zako 'utam' anaokupa mtu wako!
? Kumwambia bebi wako anunue gari wakati amepanga chumba kimoja……..

Diamond: Ili ufanikiwe ni lazma Udharirike kwanza

@Regranned from @diamondplatnumz - lli ufanikiwe ni lazma Udharirike kwanza...  Yaani lazima uwaonyeshe watu kuwa kitu fulani mie nakiweza........na katika kuwaonyesha huko kunawengine watakudharau, watakubeza, na kukucheka.........ila kuna wengine watakipenda, watathamini, kukikubali na kukupanafasi........ Maisha ndio yako hivyo........ Kadri unavyozidi kuogopa na kuona "watanichukuliaje" ndio unazidi kuchelewa kufikia ndoto zako...........Amka sasa Ukawaonyeshe! - #regrann

Mc PiliPili: ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele

@Regranned from @mcpilipili – *JE UNAJUA KWA NINI HUFANIKIWI?* Una mizigo mingi isiyo ya lazima wala faida ambayo umeibeba:- 

1. Umejipa jukumu la kuwa “mpelelezi” wa maisha ya wengine na umesahau maisha yako.

2. Umebeba vinyongo na visasi moyoni vinavyokufanya uwafikirie waliokuumiza zaidi kuliko kufikiria furaha na maendeleo yako.

3. Una marafiki wengi ambao ni kama kupe, wapo kukutumia tu na hawachangii lolote katika maendeleo zaidi ya kujifanya ndio watu wako karibu lakini kumbe wapo kwa maslahi yao!

4. Umeweka mbele zaidi “watu watanichukuliaje” kuliko kuangalia maisha yako.Watu ndio wanakuchagulia aina ya maisha unayoishi na unajilazimisha kuishi kama wao hata kama huna uwezo huo.

5. Unaongea zaidi ya kasuku lakini vitendo hakuna.Unatamani mafanikio tu moyoni lakini huna mipango ya kuyafikia.

6. Maisha yako yote umeyaweka kwenye mitandao ya kijamii.Huna siri hata moja!Hivyo unalazimika kuishi aina ya maisha ambayo yataendelea kufanana na yale uliyoyaweka kwenye mitandao ya jamii kwa sababu ukibadilika tu watasema “umefulia”

7. Kila aliefanikiwa ni rafiki yako au utasema ni mtu wako wa karibu na unaishia kuwasifia tu na kupiga nao picha lakini hujifunzi kutokana na mafanikio yao na wala hutumii fursa hiyo ya kujuana nao.

8. Upo sahihi kila siku(you are always right). Huambiliki, hushauriki na kila wazo atakalotoa mwenzako basi si zuri ila la kwako ndio sahihi na utataka litekelezwe hilo hilo. Mwisho wa siku kila mtu anakukimbia hakuna wa kukuambia “hapa umekosea” kwa sababu ya ujuaji wako.

9. Hujifunzi maarifa mapya.Mara ya mwisho kusoma kitabu ilikuwa ni “Ngoswe, penzi kitovu cha uzembe” Tena ni kwa sababu ilikuwa ni kwa ajili ya kujibia mtihani. Hujifunzi “life skills” wala ujuzi mwingine.

10. Unazurura mno mitandaoni bila faida. Kwako wewe intaneti ni kwa ajili ya kuchati tu na kufuatilia habari za mjini ambazo tangu umeanza kuzifuatilia hujawahi kuingiza hata shilingi moja, zaidi unateketeza tu hela yako ya vocha.

ISHUSHE hiyo mizigo kama kweli inahitaji kusonga mbele

Chuki, ubaguzi, na upendo mtoto ufundishwa na wazazi wake!

Chuki na ubaguzi mtoto ufunzwa na wazazi wake kama ilivyo upendo! Mtoto anazaliwa na kichwa che ubongo mtupu na safi! Sasa wazazi na walezi wa hawa watoto ndio inategemea watajaza huo ubongo wa huyo mtoto na vitu gani! ........Nisawa na elimu kuhusu Mungu, mtoto hawezi jua umuhimu wa kuabudu na kumcha Mungu kama wazazi na walezi wake hawakumfundisha na kumuonyesha kwa vitendo kuwa kuna Mungu anaye stahili kuheshimiwa na kuabudiwa! Au utakuta Mzazi anamwambia mtoto wake hiyo nguo mbaya mpe fulani (ana taja jina la mtoto mwingine) hivyo mtoto anakua akijua kuwa kama kitu kibaya au kimezeeka ndio unagawa kwa wengine! Ambapo ni makosa makubwa sana! Mzazi mfunze mtoto wako kupenda watu wote wa rangi zote bila kujali kipato chao cha kiuchumi!

Tamera amenifanya nijisikie kuolewa na mzungu ??? I’m curious to see how my baby will look like ??

Hakuna ubaya kumkumbusha mtu kitu au kumpa mtu tahadhari. Tatizo ni jinsi unavyo sema na mahala unapo semea ndiyo huleta shida!

Kwanini unamkatisha mwenzio tamaa? Wewe Kama haukubaliani na ndoto za mtu mwingine, basi pale anapo amua ku share na wewe badala ya kumkatisha tamaa ni vyema ukanyamaza’  If you don’t have any positive thing to say to someone just “shut your front door!” Tujifunze kupenda kubariki wengine  nasi tutabarikiwa tena zaidi. Mtu anapo share na wewe  mawazo  yake au  mipango yake inamaana amekuamini, kama upendi aendelee kukuamini basi nyamaza! Hivyo itakuwa umetumia busara zaidi kuliko kuanza kumtolea maneno ya kukatisha tamaa kama vile; “sidhani kama utafanikiwa”, au “mh! Jitahidi mwanzo  mugumu.”

Okay, mtu kufuata  ndoto zake sio lazima afanikiwe kama wewe unavyotaka au unavyo fikiria kwani kitendo cha mtu kujaribu teyari ni mafanikio tosha! na wewe ni nani haswa mpaka ujue what the future holds of your fella?  Unajua aliye tengeneza bulb alijaribu mara ngapi kabla ya kufanikiwa? Bill Gate alishawahi kusema kuwa yeye huwa haajiri mtu ambaye hajawahi ku fail! Na hawa ni watu ambao leo hii dunia inawatazama kama baadhi ya watu ambao ni the most achievers in the world!  “Mmh! Mwanzo mugumu” oh! well, who doesn’t know that?! Nani asiejua kua katika kujaribu kufanya kitu chochote kile unaweza usifanikiwe? Why uone umuhimu wa kumguna mtu ili umwambie mwanzo mugumu? Au Wenzetu wanasema “talking / saying with attitude” hivi unajua Billoner Mr. Trump amewahi ku file bankruptcies mara ngapi? na ni nani asiye jua kuwa Rome haikujengwa ndani ya masaa 24?!

Hakuna ubaya kumkumbusha mtu kitu au kumpa mtu tahadhari. Tatizo ni jinsi unavyo sema na mahala unapo semea ndiyo huleta shida! Pia tabia ya kurudia rudia kitu kimoja kila wakati it becomes annoying! Namwishoe mtu anaanza kulichukulia hilo neno in a negative way hata kama ulilisema kwa nia nzuri. Kwanza nimegundua  ukiona mtu anakukatisha tamaa kwenye juhudi zako jua huyo mtu anatamani sana kuwa wewe ila hawezi! Hivyo kupooza maumivu  anaona akuvunje wewe nguvu ya kusonga mbele! Siku zote jaribu kuwa mbaraka kwa mwingine hata kama mambo yako unaona hayapo sawa. Kwa kufanya hivyo utajenga tabia ya kupenda maendelo ya wengine nahapo ndipo utakapo barikiwa nawewe. Be a blessing! Kataa kuwa na roho ya kichawi!

Zamaradi Mketema: Kumbuka details ndio zinazotengeneza PACKAGE, na package ya ukweli unayoifahamu ni wewe

@Regranned from @zamaradimketema – Ukiona MAAMUZI yako yanaangalia sana watu ujue una hatihati ya kuharibu maisha yako, kuna watu wanategemea sana ushauri na APPROVAL za ndugu, jamaa wa karibu na marafiki katika kila kitu bila kuchuja mengine aone ni ya kwake na yanamuhusu yeye tu, tusichofahamu linapokuja swala la hisia na mahusiano hakuna ubaya wa kusikiliza lakini fata kulingana na moyo wako, wengi wanaokushauri watakushauri kulingana na interest zao juu ya huyo mtu au vile wanavyomuona nje, lakini kumbuka wewe ndio unaishi nae na ndio mwenye moyo. Na zaidi kuna vingi unavyovijua ambavyo wao hata wawe karibu kiasi gani hawatakaa wavione, na hata kama mnahadithiana mara nyingi mnaongelea matukio na sio DETAILS, na kumbuka details ndio zinazotengeneza PACKAGE, na package ya ukweli unayoifahamu ni wewe, ila kwa kutaka kuridhisha watu unaweza jikuta unaacha kufanya maamuzi sahihi kwakuwa fulani kakwambia sio sawa tena kwa kuangalia tu kile ULICHOMUAMINISHA NACHO ama kumwambia, mwisho wa siku athari za UKWELI unabaki nazo wewe. Kumbuka tu Washauri ni wengi kwenye maisha lakini hawana msaada wowote na wewe pale linapokukuta, watu wapo kila siku lakini hupaswi kuwazingatia kiasi mpaka ukasahau lenye umuhimu na wewe kwa kuwapendezesha wao, wao wanafanya ya kwao bila kujali utawahukumu vipi na ya kwako yatakapoharibika utakaekaa ndani kulia ni wewe peke yako, na zaidi hawatakuwepo muda wote kwa ajili yako. – #regrann

LeMutuz: Nilichojifunza Bongo ni hakuna anayetaka kukubali kuwa tunalo tatizo na hakuna anayetaka kuongelea solutions so we are creating a TIME BOMB.

LIVE STRAIGHT TALK:- The Art Our Lost Culture  

Sasasahivi in our Society tunatengeneza Vijana wengi Lesbians na Mashoga na hakuna anayejaribu hata kuliongelea kwa mapana au chanzo cha hili tatizo ni tatizo kwa sababu we are creating a Society of confused Youths ambao ndio Taifa la kesho! Nilichojifunza Bongo ni hakuna anayetaka kukubali kuwa tunalo tatizo na hakuna anayetaka kuongelea solutions so we are creating a TIME BOMB. Siku moja litakuja kulipuka vijana wetu kuanza kudai ndoa za Jinsia Moja tutaanza kutafutana kurundikana Rumande na Jela kumbe tuna wakati wa kutosha kulirekebisha hili tatizo now!……… As a Society tunatokea kwenye Mila na Desturi ambazo sasa hivi zinapitia a big test of kama ni kweli zilikuwa strong enough from the West Culture ambayo imekuja na sera za Wawekezaji na hasa the Television Culture ambayo Baba wa Taifa aliikataa sana. Sometimes ninajiuliza sana je kwanini Mwalimu alikuwa muoga sana na the Western Culture? Je alikuwa na wasi wasi na how fragile our Culture is?!  Maana ukienda Zanzibar hata wao wana Television pia lakini Mila na Desturi kwao hazijaharibiwa na Western Culture kama sisi huku Bara it is a FACT! ndio maana hapa mjini mitaa yetu imejaa watoto wasiokuwa na wazazi as opposed na Visiwani, wenzetu hawana hilo tatizo ……….Tanzania tumefanikiwa sana ku maintain Swahili as our Language na ni by the Fact that tulishituka mapema na kuunda Baraza la Kiswahili now nashangaa kwanini hatukuunda mapema chombo cha kusimamia Maadili na Utamaduni wetu au huenda tunavyo lakini they are toothless!………Vijana wetu wa sasa hawawezi kubeba na kuyakubali Maumivu ya Maisha ambalo ni tatizo namba moja la The West. So kule kuna Chama cha wamiliki wa Bunduki kinaitwa NRA ambacho agenda yake ni kubwa sana Dunia nzima kwa kushirkiana na NGO za Mashoga na Lesbians kule Holywood kama ulikuwa hujui wao ndio wamiliki wakubwa wa the Culture of Television ambayo unamuachia mtoto wako mdogo huku Bongo kuangalia siku nzima ………. Usichokijua kipindi cha TV cha Dakika 15 to 30 kinalazimishwa kutoa maswali na majibu ya maisha kwa matatizo ya vijana ndipo hao NRA huingiza agenda ya kutumia Bastola au kubadili jinsia kama the Kardeshians! TUKATAE HUO UTAMADUNI! – le Mutuz –

Kama wewe ni mpangaji usimdharau mmiliki wa nyumba ya udongo!

Kama wewe unaishi kwenye nyumba ya kupanga usimdharau yule anayemiliki nyumba ya udongo! Hauna haki ya kufanya hivyo! Kwani wewe unayeishi nyumba ya kupanga hauna uwezo au nguvu ya kutosha kumiliki hata ardhi ya kujenga nyumba ya udongo. Nasiku ikatokea hauna kazi au ajali ya ulemavu ikakukuta ukashindwa kufanya shughuli za kuzalisha pesa inamaana utashindwa kulipa kodi ya pango na mwenye nyumba yake atakufukuza! Lakini yule mwenye nyumba ya udongo maisha yataendelea tu! Nyumba ya udongo inaweza isiwe na mvuto sana kwenye macho ya watu lakini inatoa matumizi sawa na nyumba ya matofali! Wakiitwa majina ya watu na mali zao mwenye nyumba ya udongo jina lake litakuwepo lakini jina la yule anaeishi nyumba ya kupanga itakuwa shida kwake! Usimdharau mwenye chake! Kama wewe ni mpangaji usimdharau mmiliki wa nyumba ya udongo!……..Anyway, hayo ni mawazo yangu asubuhi hii siku ya JumaTatu! Nawatakieni wiki njema na uzalishaji mwema!

Dina Marios: Kuna watu tutakutana nao kama baraka kwetu na wengine ni mafunzo kwetu.

Kuna watu tutakutana nao kama baraka kwetu na wengine ni mafunzo kwetu. Hata wale unaohisi ni wabaya kutokana na yale waliyokufanyia au wanayokufanyia sasa wapo hapo kwa sababu. Wapo kwa ajili ya kukupa funzo fulani…….wapo hapo kukufanya uwe imara na mkomavu.
Dina Marios

Dr. Shika kutambulishwa usikuwa wa 900 itapendeza!

Mara paa! Dr. Shika kwa celebrity! Jamani, it’s never too late to be you and achieve your dreams! Huwezi jua ni lini na kwa njia gani Mungu atakufungulia mlango wa kufikia malengo yako! Wewe fanya kazi zako kwa uwaminifu na kwa bidii mengine Mungu atakutimizia. Pia safari moja huwanzisha nyingine. Unaona hapa Dr. Shika alikwenda kwenye mnada wa kununua nyumba of his own dream japo mfukoni alikuwa “kachacha” lakini alithubutu. Mwenda bure si mkaa bure! Watanzania wangapi walikuwa wanamjua Dr. Shika lakini leo hii ndio the talk of the country! Katika umri huu kwa mazingira ya Africa haswa Tanzania sidhani kama hata yeye aliwahi kuwaza kua sentence yake moja tu “900 itapendeza”  itaweza badilisha maisha yake na kumuweka kuwa wa level nyingine kabisa! Leo hii ana mkurugenzi na kualikwa sehemu mbali mbali kuelezea maisha yake. Nani alijua kuwa maisha ya mtu kama Dr. Shika yanaweza yakawa kivutio na yahamasa kwa Watanzani?!  Somo hapa nikuwa wavumilivu katika safari za kufikia ndoto zetu kwani Mungu ndiye mpangaji na mtoaji wa vyote! Acha tamaa ya kutaka vitu kwa haraka! #900Itapendeza

Embu tucheke kidogo! Eti wewe waonaje kwa hili?

Juzi kati niliweka tangazo la msiba wa ndugu yangu  kwa hii blog , nikaambatanisha na picha ambazo tulipiga akiwa hai ambapo ilikuwa mara ya mwisho kuonana naye Tazama hapa ??  (Tanzia). Sasa kuna mtu ameweka comment akishangazwa na picha niliyotumia kwani tulikuwa tuna tabasamu. Anasema tunatangazaje kifo kwa furaha hivyo? Soma ??  Nimecheka kwani kwangu imekuwa kichekesho,nikahisi huyu dada lazima atakuwa Muhaya maana Wahaya akili zao wanazijua wenyewe, na hilo pozi wala uulizi katoka mkoa gani ?? …… Hivi kuna kanuni ya picha ipi itumike kutangaza msiba? Ukishaweka picha ya marehemu akiwa mwenyewe zile zingine sizinakua ni kumbukumbu mlizopiga!! Jamani, mimi ni Msabato na Mjaluo vile vile hivyo kuna vitu vingine haswa kwenye swala la misiba mtanisamehe. Kwani kuomboleza kupo tu lakini huwezi kuomboleza kama mpagani! Halafu, tujenge tamaduni za kuonyesha upendo wa dhati kwa wale ambao wanagusa maisha yetu wakati bado wako hai! Mambo ya kumlilia mtu na maneno mazuri akisha kufa ni upuuzi mtupu! Yani mimi kama umeshindwa kunipenda nikiwa hai, hata salamu hutujuliani gafla nikisha kufa eti wewe ndo unakuja na makelele yako kunililia?! No! Sitaki! Kaa kwako nitashukuru zaidi, kuliko kuja kunililia kinafiki! Kwanza kuliliwa na wanafiki inaweza ikawa kikwazo cha kuingia Mbinguni ?? just saying! Sipendi wanafiki haswa nikisha kufa nawaomba msije! Nionyeshe unanipenda na kunijali nikiwa hai! Nami nitafanya vivyo hivyo!

Sir. O.O Igogo: Uwaminifu na huruma ni nguzo kuu ya maisha, zingatia.

Leo nimepewa somo na Sir O.O Igogo kuwa uwaminifu na huruma ni nguzo kuu ya maisha, hivyo nizingatie! Aliyasema hayo baada ya kunitumia picha ya aliyekuwa mke wa mmoja wa fundi wetu marehemu Tyson.

Mke wa marehemu fundi Tyson na mtoto wa marehemu

Mke wa Tyson alitokwa na machozi baada ya kukabidhiwa fedha ambazo ziligundulika kuwa zilikuwa hazijamaliziwa kulipwa katika kazi ya ujenzi wa ukuta wa nyumbani kwetu ambayo marehemu mumewe aliifanya mwaka 2014. Jamani msiwe wadhurumaji kwani hauto kaa ubarikiwe kamwe! Wengi wanashindwa kuelewa kwanini mafanikio yao huwa yanakuwa ya muda mfupi wakati wengine maisha yanawanyookea mika nenda miaka rudi! Acha dhuruma  Mungu hapendi!! Machozi ya watu yanalaana sana! Btw, wangapi huwa mnaweka rekodi ya kila risiti na gharama za ujenzi wa nyumba zenu? Hii huwa naona sana kwetu kila jengo huwa nakitabu chake kila kitu kinarekodiwa na risiti zote zinatunzwa. Ujenzi ukikamilika basi kitabu kinakaguliwa na kufungwa na kuwekwa kwenye kumbu kumbu za kudumu. Sasa kama kuna mtu hakulipwa pesa zake kama marehemu Tyson au kuna kitu kilisahaulika kufatiliwaa basi kitafanyiwa kazi wakati huo. ………Anyway, poleni sana wafiwa. R.I.P Tyson!

Zamaradi Mketema: Asieheshimu muda wako haheshimu maisha yako.

Asieheshimu muda wako haheshimu maisha yako.
MUDA NI MAISHA, na ndiomana tunaishi kwa ratiba na deadlines hata kwenye maofisi, na hata kwenye maisha ya masomo kikawaida kuna ratiba ya kuanza na kumaliza kutokana na umri, ingekuwa kila kitu kinafanyika kwa muda mtu anaojitakia vitu vingi visingekuwa vilivyo, hivyo heshimu sana muda wako na wa wengine pia, na usiruhusu mtu autumie ndivyosivyo ama anavyotaka yeye sababu anaecheza na MUDA WAKO anacheza na MAISHA YAKO.

Zamaradi Mketema: Kama unaweza kupokea machungu yangu bila kunihukumu kwanini ushindwe kuibeba furaha yangu bila kunituhumu

Dunia ya sasa ni dunia ambayo watu hawataki wala kufurahia kuona unasherehekea mazuri yako, na unapofurahia inatafsiriwa kwa namna tofauti na kila mtu atakuangalia kwa jicho lake. Wanachoona sawa ni post za malalamiko na kutamani kila siku upost huzuni zako wakupe pole kitu ambacho sidhani kama ni sawa. Tusichofahamu kila mtu ana kitu kinachompa raha ama satisfaction, tupeane nafasi na uhuru wa kufurahia bila kuhukumiana vile vinavyotupa furaha kwenye maisha. 

Kama unaweza kupokea machungu yangu bila kunihukumu kwanini ushindwe kuibeba furaha yangu bila kunituhumu, maana tunatakiwa kufurahia kila hatua hata kama ni ndogo kiasi gani sababu hatujui hizo kubwa tutafika lini. Tuache watu wafurahi, tunavyopokea aibu zao basi na ushindi wao tuupokee, sio kila kitu tukitafutie namna ya kukichafua na kuona kama unaoneshewa wewe, hata MUNGU hupenda kushukuriwa na sio malalamiko kila siku bila kuangalia Baraka nyingine. Sasa pia kwenye maisha ya kawaida kwanini tuoneshe yanayotupa tabu tu bila kugusa na yanayotupa furaha pia, unapofurahia kitu utasikia watu wenye roho za kichawi "na ukifeli/ukianguka pia utuoneshe!!"  
Jamani KUANGUKA KUPO TU ni sehemu ya maisha, na ndio huko kunakotufanya tufurahi tunaposhinda. Tunafurahi kwa kipindi hiko na kushukuru, hakuna ubaya wa kufurahi pia tunapopata, na ukimuona mtu anafurahia ushindi wake muache, tusilimitiane na kuhukumiana, hujui kwake ina maana kiasi gani ama amepigana kwa namna gani, ama ameomba MUNGU mara ngapi kufikia hapo, hata kama kwako ni kawaida. Tumeagizwa kufurahia na kupokea nyakati zote, so usisubiri mpaka upate kubwa ndio usherehekee, ENJOY THE MOMENT, ya mbele anayajua MUNGU.

 

Faraja Nyalandu: Matokeo yake, wengi wao leo hii wana hii tabia pia, hawavunji tu ‘kibubu’ kwasababu imetokea harambee ya ghafla ya kumchangia binamu fulani.

“Nimeamua kufuatilia rafiki zangu waliolelewa na wazazi wafanyabiashara, kutunza hela sio tu ni muhimu ilikuwa lazima. Walikuwa wanaambiwa hawana hela kwasababu zishawekwa kwenye savings au kuongezwa kwenye mtaji. Walijifunza kwa maneno na vitendo, na maumivu of course. Matokeo yake, wengi wao leo hii wana hii tabia pia, hawavunji tu ‘kibubu’ kwasababu imetokea harambee ya ghafla ya kumchangia binamu fulani. Ila hii ni tabia, mtu yoyote anaweza kuwa nayo. Tuanze kuwafundisha watoto wetu kutunza hela. Kutunza faida. Kutunza nyongeza (hata kuitengeneza nyongeza). Njoo @nmbtanzania – mfungulie Chipukizi au Mtoto akaunti #NMBKaribuYako P. S This video for #NMBWajibu is coming soon” Faraja Nyalandu——

LeMutuz: cha ajabu ni wasiokuwa na akili kabisa ndio katika hii new generation wanakuwa maarufu sana na kukubalika sana na Public

EXTRA LIVE STRAIGHT TALK:- ...Mwanamke Shujaa ...Mwanamke Jasiri ...Miss Tanzania 1999 na Balozi Maalum wa Umoja wa Mataifa Tanzania @hoycetemu ...unfortunately Dunia inapitia transition ya One Generation to another .....in our new generation ni Wadada wasiokuwa na Maadili, wasiokuwa na heshima, Wanaogombania waume za watu in the Public, wanaotembea nusu uchi, wanaojua kutukana sana matusi in the public, wasiokuwa na pa kuishi, wasiokuwa na kazi, na cha ajabu ni wasiokuwa na akili kabisa ndio katika hii new generation wanakuwa maarufu sana na kukubalika sana na Public Ila sio tena wadada wanaojitambua kama wewe ambaye una Mume, una Familia, una kazi inayojulikana, unapigana kusaidia Jamii, una pa kuishi pazuri, unaheshimika kwa jamii inayokuzunguka una elimu kubwa ....Wadada wenye Maisha kama wewe hushambuliwa left and right na Wadada wasiokuwa na Maisha ambao hushangiliwa sana na Public ya wasiokuwa na Maisha kama washambuliaji ...yakikutokea hayo ya kushambuliwa na our "DEAD LIVING DOGS" usijali kumbuka hata kwenye Biblia Wana wa Israel walipopewa Choice ya kuchagua nani asulubiwe kati ya binadam mwenye Maisha Yesu au yule Jambazi asiyekuwa na Maisha Barnabas walimchagua Jambazi asiyekuwa na Maisha kama wao ndio maaa hata leo Dada mwenye Maisha kama wewe anashambuliwa na wasiokuwa na Maisha na wanaoshangiliwa na wasiokuwa na Maisha wenzao USISHANGAE WALIMFANYIA HATA YESU ...kumbuka siku zote kuwa UKISHANGILIWA NA MUNGU lazima utachukiwa na Shetani ambaye ana watu wengi sana hapa Duniani ila endelea kupigana kukubaliwa na Mungu na kuwa mfano kwa Jamii....Salute @hoycetemu I LOVE U MY SUPER SISTER! - le Mutuz

“KAMA HAJAKUOA BASI SI MUME WAKO SOMA KISA HIKI CHA HUYU DADA.”

KAMA HAJAKUOA BASI SI MUME WAKO SOMA KISA HIKI CHA HUYU DADA.

Kuna watu wengine ambao unakutana nao katika maisha halafu wanaishia kukupa hasira tu, unawaza hivi ni kwanini sikukutana nao miaka kadhaa kabla nakutana nao sasa, lakini yote ni mipango ya Mungu.

Miaka mitatu iliyopita nilikua katika kipindi cha kupigania ndoa, kipindi ambacho nililazimika kufanya vitu vingi vya ajabu ili tu mwanaume anikubali, nilikua nadhindani na wengi hivyo nikiamini kua mimi ndiyo napendwa zaidi nilijua nitaolewa mimi.

Lakini mpenzi wangu hakujali hilo, baada tu ya kunipata alinigeuza kama ka ATM kake, wote tulikua wafanyakazi wa serikali, alitaka kununua gari, hakua na pesa za kutosha na aliniomba nimkopeshe. Nikiwa najua kabisa hatanilipa nilitoa kiakiba changu cha miaka miwili ambacho nilipanga kufungulia biashara na kumpa. Hiyo ilikua ni baada ya kumbembeleza na kumshauri sana kuwa kwanini afanye vile, kwanini tusingejenga kwanza.

Jibu lake lilikua yeye ni mwanaume siwezi kumpangia. Aliniambia kama nataka kumpanda kichwani wakati bado hajanioa akinioa itakuwaje? Niliufyata mkia nikanyamaza nikampa zile pesa lakini hata gari yenyewe hakununua, aliishia kuhonga Malaya wake.

Nilijua kwani walinipigia simu kunitukana kua mimi natafuta na wao wanahongwa, niliumia sana lakini baada ya kumaliza zile pesa basi alikuja kuniomba msamaha. Alijutia sana na kama unavyojua mwalimu wetu kipofu aliniambia msamehe, hakuna mwanadamu aliyakamilika.

Lakini sasa nilimpa mashariti kua tunapaswa kuwekeza katika maisha yetu, aliniambia anatafuta pesa anunue kiwanja na anataka kunioa. Kama kawaida ukisikia ndoa unchanganyikiwa, ingawa kwetu walikua wanamfahamu lakini sa alijitambulisha rasmi.
Alinivalisha pete ya uchumba kuonyesha kua alikua siriasi na mimi. Maisha yaliendelea na baada ya kuvalishwa pete nilivyokua mpumbavu nikageuka kua mke tena, nikijua kuwa nikikaa naye ndiyo nitamdhibiti nilihama kwangu na kwenda kuishi kwake, ndiyo ni upumbavu kuwa mke kabla hujaolewa.

Kabla hata sijaolewa basi tulianza kuishi pamoja nikiamini pete ndiyo cheti cha ndoa. Nilihamishia vitu vyangu kwake na tukawa mwili mmoja, hapo ndipo nilianza kuona chungu ya pilipili. Sio kwamba tu alizidi kuninyanyasa lakini alinipiga pia.

Akichelewa kurudi nikiuliza napigwa ananiuliza mimi ni Malaya tu kaniweka ndani na si mke. Lakini sinishavalishwa pete nilivumilia kwa wimbo uleule wa ndoa ni uvumilivu sijui hata nilikua navumilia nini wakati ndoa yenyewe hata sikua nayo.

Alinunua kiwanja kitu ambacho nilikua namshauri kila siku na akataka tuanze ujenzi, hapo nilijua mwanaume kabadilika, kwakua kipato chetu cha kawaida si unajua mishahara yetu hii basi aliniambia nichukue mkopo ili tukichanganya na kipato chake kidogo basi tujenge.

Nikijua kuwa tutakuja kufunga ndoa karibuni nilichukua mkopo, ujenzi ukaanza na Mungu si Athumani alijalia pamoja na vidilidili vyake vya kazini basi tulifanikiwa kumalizia ujenzi. Katika kipindi chote hicho tunajenga aligeuka na kua malaika, akiwahi kurudi na kufanya kila kitu kama mume mwema.

Lakini baada ya kumaliza kujenga, nikitaka kuhamia hapo ndipo ilizuka kasheshe. Wanaume ni washenzi ndugu zangu na hapa ndiyo najuta kwanini Kaka iddi sikukuona mapema nikasoma makala zako. Unakumbuka makala moja ulisema kama mwanaume hajakuoa si mumeo chako ni chako na chake ni chake. Hilo ndiyo lilinitokea, nikijua najenga na mume wangu mtarajiwa kumbe nayeye alikua anajenga na mtu mwingine.

Yule mwanaume hakutumia hata senti tano katika lile jengo, alikua na mwanamke mwingine ambaye naye kama mimi alichukua mkopo tena wakwake wa benki kibiashara na kuwekeza kwenye ile nyumba. Lakini yule mchaga alinizidi kete, wakati mimi nasubiri kuambiwa tuhamie yeye alihamia kabisa.

Ndiyo kwa mbinde alianza kuishi pale kwenye ile nyumba, nilipotaka kwenda na mwanaume alikataa hakutaka twende, nilipokazania sana alinipiga na kunifukuza, ndiyo alinifukuza na kuniambia sina changu, nililazimika kuondoka na kwenda kuishi na rafiki yangu.
Wakati nikiwa huko nikagundua kua nina ujauzito wa wiki mbili, namuambia ananiambia hanijui. Yaani sijui nini kilitokea lakini nilisikia katangaza ndoa na yule mwanamke aliyekua akiishi naye, kabla hata sijastuka naambiwa wameoana ndoa ya kiserikali.

Ndiyo nikabakia na mimba yangu, yaani nilibaki nalia tu, nilitamani hata kujiua lakini maisha ilikua ni lazima yaendelee. Ilinibidi kuanza upya kwani mbali na ujauzito lakini mshahara mzima ulikua unaishia kulipa mkopo wa nyumba ambayo nilishanyang’anywa.

Mpaka leo hii nalipia mkopo na mpaka leo hii nawaona tu wakipita wapo na furaha na maisha yao. Yaani mimi nina mtoto wangu na wao yule mwanamke kumbe alishazaa naye mtoto mmoja mimi sijui na sasa ana mimba nyingine.

Natamani hata niende niichome moto ile nyumba kwani napata uchungu kila siku nikiangalia Salary Sleep yangu, kwa bahati mbaya wote tunaishi hapahapa Dar hivyo haiwezi pita wiki sijawaona. Nina hasira sio kwasababu nimedhulumiwa tu bali nina hasira na wewe Kaka Iddi kwanini sikukujua mapema nikasoma makala zako mapema. Nina uhakika asilimia mia nisingefanya upuuzi nilioufanya. Kama unakumbuka tulishaongea niliponunua kitabu chako.
Nimeandika hivi ili wanawake wenzangu ambao wanabembelezea ndoa nao waamke na wasiwe mabwege kama mimi. Natamani hata kila siku uirudie ile makala yako kuwa kama mwanaume hajakuoa basi mali zake hazikuhusu.

Kuna wengi tu humu mnajifanya mnapendwa lakini siku likiwatokea mnawalaumu wahusika kumbe makosa ni yenu. Nimejifunza maisha yanaendelea ila nashukuru Mungu nilikupata kwani nilishakata tamaa, ila kwa ushauri wako kaka nimeanza biashara na inaenda vizuri.
Nashukuru kwa kitabu chako pia kimeniamsha sasa najielewa. Sipo kwenye ndoa wala mahusiano kwa sasa ila najua kabisa kuhusu wanaume, nimejifunza mengi kupitia makala zako na zaidi katika kitabu chako, kaka umeniponya.  Sasa hivi nataka kulipa kisasi, sitaki kulipa kisasi cha kuchoma nyumba yao moto bali cha kujenga nyumba yangu na kufanikiwa zaidi. Nakumbuka siku ya mwisho tulipoongea uliniambia hakuna kisasi kizuri kama kua na furaha zaidi ya mtu aliyekuumiza kumuonyesha kuwa humhitaji yeye kufurahi Ahsante kaka Iddi.

 

#Nimekopi kutoka Facebook na kuleta hapa kwa blog. Sijui muhusika!

“I’m Charles McCater. I’m going to die Charles McCater”

“I’m Charles McCarter. I’m going to die Charles McCarter. I don’t even know why you’re here. Call Brenda and get my kids. where are my kids?! I asked you to do one little thing and you can’t even do that after 18 years get out……”

Kuna watu hata uwe mwema kwao kiasi gani they will never ever appreciate you or respect what you did / doing to them! …..Sasa ndio kama huyu “Charles McCarter” mtu ambaye ameokoa maisha yake tena wakati akiwa na kila sababu ya kumuacha afe yeye ndio kwanza anamdharau na kumuongezea hasira!! ……..Eti “I’m Charles McCarter. I’m going to die Charles McCarter”!! Jamani, lazima tukubali kuwa kuna watu hawawezi kubadilika isipokuwa kwa uwezo wa roho mtakatifu pake yake!! Na wengine hawawezi badilika kwani roho wa Mungu alisha hama ndani yao! Watu wa namna hii hata kama unawaombea waombee tu lakini kaanao mbali kwani wanaweza wakakufanya ufanye maamuzi ya hasira bila kutegemea kama huyo mama!! …….huu usemi wa Maya Angelou “when people show you who they are believe them” kwakweli nimejikuta siku hizi nautumia sana katika kuangalia ni watu wa namna gani I want around me! Mtu akisha kuonyesha dalili zote za kuwa yeye labda ni mchonganishi, mmbea, tapeli, tafadhali wala usisite kuamini kuwa she / he is less than what your  instinct is telling you!! Some people are “Charles McCarter” and they will die “Charles McCarter”! Just leave them alone!  ***Picha yangu haina huusiano wowote na story nimeitumia tu****

Peter Sarungi: UPANDE WA GIZA NA MWANGA WA BINADAMU

Na Peter Sarungi (The Next Speaker)

UPANDE WA GIZA NA MWANGA WA BINADAMU.
Binadamu ameumbwa katika ukamilifu ulio kusudiwa na Mungu na ndio maana akiwa kichanga anakuwa mtupu asiye tambua baya wala zuri. Binadamu huyu anaanza kuondoa ukamilifu wake pale anapo ona, kusikia, kusoma na kutenda mambo yaliyo najisi.

Akisha tambua baya na zuri ndipo anapo kuwa sio kiumbe kikamilifu. Binadamu huyu sasa anakuwa na pande mbili ya maisha yake. Kuna upande wa mwanga wenye matendo mazuri yaliyo wazi kwa watu na upande wa giza wenye matendo mabaya yaliyo fichwa gizani yasionekane kwa watu.

Kila binadamu ana maovu yake ila kinacho saidia ni kufichika kwa maovu hayo, ninacho shangaa ni kuwepo kwa tabia ya kuhukumu, kudharau na kutoa adhabu kwa binadamu ambao uovu wao umefichuliwa. Sijui logic hapo ni ipi ikiwa anaye toa adhabu na kuhumu naye ni mwenye maovu yaliyo jificha???

“The Art of a Close Minded Society ni tatizo linalotusumbua sana hili Taifa kuanzia wananchi wengi mpaka Viongozi”~~~~~ LeMutuz

LIVE STRAIGHT TALK:- The Art of a Close Minded Society ni tatizo linalotusumbua sana hili Taifa kuanzia wananchi wengi mpaka Viongozi tuna tabia ya kutopenda kufikirisha Akili kabisa na very soon hili Tatizo litatugahrimu sana as a Nation cause najua linatugharimu wananchi individually kila siku in our daily lives

I mean bado ninakumbuka yote yaliyotokea kwenye vita ya RC na Madawa ya kulevya we almost drove out from the post the best ever RC of our all history as a Nation kisa na mkasa habari za kusikia tu from One Side bila kujali the second side like how the Americans taught me kwamba BINADAM USIFANYE MAAMUZI YA AINA YOYOTE IN YOUR LIFE MPAKA UHAKIKISHE UNA PANDE ZOTE MBILI ZA HABARI ULIYOISIKIA 
Hii sheria ya maisha ni ngumu sana kwetu Wabongo juzi nimekutana na mtu msomi alikuwa nje ya Nchi kwa muda mrefu sana na wakati wa ile Vita ya RC alikuwa akinitumia sms za ajabu sana akimshambulia RC sikuwahi kumjibu ila nilisubiri arudi kwanza now majuzi nikamuomba kwamba hebu jaribu kusikiliza upande wa pili wa habari maana najua unayo ya upande mmoja yaani wa Gwajima tu now alisikiliza mpaka alipoona hadithi yangu inamtoa kabisa kwenye box lake akaanza ku protest kwamba hakujua nimsamehe ingawa alisema neno moja la msingi sana aliniomba nimuombee msamaha kwa RC ...hili huwa ni neno gumu sana nowadays kulisikia kutoka kwa Vijana wa kisasa ni almost halipo tena in our National vocabulary inasikitisha sana cause inaenda straight to the core of our Education System kwamba inahitaji a serious ovehauling maana we are ctreating a time bomb society
Imagine 65% ya Taifa letu from 55M people ni Vijana ambao hawawezi kabisa kufikiria kwamba any new story in life ina Pande Mbili na unahitaji kuzijua zote kabla ya kutoa uamuzi ndio maana sasa tuna namba kubwa sana ya Divorce na infact sasa hivi as a Nation we are so vunerable that likitokea Taifa au Taasisi yoyote kutoka nje ikatuvalia njuga kutuvurugia amani yetu wala hawatapata shida cause tumetengeneza wenyewe kwa kutumia mfumo wetu mbovu wa Elimu Taifa la Vijana wasioweza kufikiri kabisa nje ya box la maisha waliomo

Guys tujifunze basi hata on our own kujua pande mbili za ishu kabla ya kuruka na hukumu! - le Mutuz