Category Archives: Lifestyle!

Watoto wanahitaji malezi ya mzazi! Mali na pesa siyo malezi!

Wahenga walisema kulea mimba si kazi kazi kulea mwana! Ukiwa mjamzito kike kiumbe ulichobeba hata kama hutaki kikuwe kitakuwa tu! Sasa ni hiyari yako kula vizuri na kujijali ili uzae kiumbe chenye afya bora na salama. Mama uliyebeba hicho kiumbe ni jukumu lako kutafakari matendo na tabia zako wakati wa ujauzito huo kwani huyo mtoto anauwezekano mkubwa sana wa kuhakisi tabia zako akiwa tumboni mwako!  Huo ni mtihani wa kwanza katika malezi ya mtoto!  Jana nilisoma post ya Jackie ikanikumbusha mtihani wa pili katika malezi ya mtoto ambapo wazazi wengi huwa wanafeli! Pia ikanikumbusha kuhusu wazazi fulani ambao wapo kwenye  reality show fulani inaitwa “Married to Medicine” wote ni madaktari na mama anaumizwa na kitendo cha wao kuwa busy na kazi kiasi kwamba wanakuwa hawana nafasi ya kukaa na watoto zao! Napia ikanikumbusha interview ya Naomi Campbell aliyofanyaga na Oprah Winfrey mwaka 2010 ambapo Naomi alisema kuwa siku zote amejisikia mpweke toka akiwa mdogo kwani wazazi wake wahakuwa nae karibu. Mama yake Naomi yeye aliamini kuwa anafanya kitu kizuri kufanya kazi sana ili kuweza kumpatia mtoto wake vitu vizuri, kusoma shule za private n.k ………. Soma na tazama video hapo chini ?@Regranned from @j_n_mengi – Dear parents, I know you’re busy working hard to feed and raise your kids but please remember that your physical presence is very important to your child. You need to invest more than money to your child, they need to talk to you, they need your hugs and reassurance and most importantly they need you to teach them to be good human beings.”

Pesa na mali ni vizuri kama ukiwawekea watoto wakawa navyo kwani hilo ni jukumu lako kama mzazi! Kumbuka “Pesa na mali ni urithi mtu apataye kutoka kwa babaye” hayo ni maandiko ya Biblia siyo mimi! Lakini kabla ya kuwapa hizo pesa na mali ni vyema ukawafundisha jinsi ya kupata hizo pesa na mali ili nao waweze fundisha watoto zao! Hata hivyo, kabla ya kuwafundisha jinsi ya kutafuta pesa na mali watoto wanatakiwa kufundiswa maadili!

Watoto wanatakiwa kuonyeshwa upendo iliwajifunze kwa matendo, watoto wanatakiwa kufundishwa elimu ya Mbingu kabla hujampa elimu ya duniani! Kwamfano, kabla ya kumfundisha mtoto wako kuhesabu embu hakikisha anajua kusali au kusema sala ya Bwana kwanza! Mfano mwingine, kabla hujamfundisha mtoto wako kusema “naomba” mfundishe kushukuru kwa kila kitu anachopewa, hakikisha anajua kusema “asante” kwanza kabla ya kusema “naomba”!

Kumvalisha mtoto wako nguo za designer maharufu siyo malezi! Surely, itamfanya aonekane vizuri lakini haita msaidia kuwa kiumbe bora! Kumlaza mtoto wako kwenye nyumba ya mamilioni ni vizuri lakini haita mpa confidence au kuacha kuwa muongo na mwizi! Watoto wanahitaji malezi ya wazazi! Pesa na mali siyo malezi!!

My son enjoying his New Year breakfast!

Yaas! That is my son! Enjoying his New Year breakfast in Nairobi. At age 2 1/2 he got all his table manners in place ?? way to go son! Wasichana itabidi wajipange sana tu! Kama hawakufunzwa ustarabu na mama zao wakwende huko hatuwataki sisi ?? We are raising a gentleman right here I hope someone is raising a Queen for him ??  maana Mimi mama mkwe nitamkagua kabla hajaingia ndani ya nyumba ya mwanangu ??? chezea mama mkwe wa dotcom! Kama tunataka tuondoe unyanjasaji na ukiritimba kwa wanawake inabidi wakina mama muwe teyari kulea vijana wenu katika maadili, na mambo yanayofaa! Na mambo hayo huanzia katika umri huu! Usisubiri akifika sijui miaka 6 that is way too late! Pia watoto wakike muwafunze tabia njema, kujithamini, good touch and bad touch mara tu wanapojua kuongea na kutembea! Usingoje mtoto sijui aote maziwa ndio unaanza "kubwabwaja"!! Kama tunataka ukombozi wa mtoto wa kike na mabadiliko ya tabia za wanaume wa Kiafrika basi wakina mama lazima mkubali kubadilisha tabia ya malezi yale ya kizamani kuwa mtoto wa kiume ni "King" na mtoto wa kike ni "servant"!! Kuwa mtoto wakiume haitaji kupewa malezi yenye maadili ya jinsi ya kuwa kaka, baba, mume, na raia mwema isipokuwa toto wa kike tu! Yeye ndiyo anatakiwe afunzwe kuwa dada mwema, mama mzuri, mke bora, na raia mwema,  swali linakuja awe mwema kwa nani?!! Mwaume mbakaji? Au mwanaume katili? Au a cold-hearted killer? Au mwanaume mnyanyasaji asiye hata na chembe chembe ya hofu ya Mungu?!! Mothers I'm raising my gentleman because I don't want him to be part of that ugly statistic!!What about you!! .........Happy New Year everybody!

Mlee mtoto katika njia impasayo!

  Kwanza naomba mniwie radhi wapendwa wangu ambao ni Waislam. Mimi ni Mkristo hiyo mambo mengi nikiongea nita refer to the Holy Bible kwani hicho ndicho kitabu nakijua na pia sipo hapa kwaajili ya dini hivyo sitokaa ni compare Quran na Bible! Sasa Biblia katika kitabu kile cha Mithali 22:6 inasema mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa  mzee! Hizi picha za birthday ya Nillan ambazo zinaonyesha wako mezani wakila chakula na kunywa zimenifanya nikumbuke hilo fungu la Mithali 22:6!  Hivi wazazi wangapi mnawalea watoto wenu kwa kuwafundisha kuwa chakula ni kitu cha kuheshimiwa hivyo ukila lazima uwe na nidhamu?! Kuwa hupaswi kutembea huku unakula kama mkimbizi au mtu aliye vitani!! Unamfunza mtoto kuwa ni lazima ukae chini / mezani wakati wa kula napia ni marufuku kuongea nachakula mdomoni!!  Kama wewe ni mzazi unaye ishi katika mazingira mazuri na ungependa mtoto wako aende mbali zaidi ya hapo ulipo wewe, je umemwandaa mtoto wako kukabiliana na mazingira hayo?! Kwamfano, ungependa mtoto wako awe na uwezo wa kwenda naye kwenye 5* hotel nakula chakula mbele za watu nilazima umfunze mwanao kukaa mezani wakati wakula na atulie mpaka atakapo maliza chakula. Nilazima umfunze mtoto kutumia visu, uma, na kijiko tena umfunze mara kwa mara ili azoee kuvitumia kama Zari alivyofanya kwa watoto wake. Hao watoto kukaa mezani kwa utulivu hivyo nakula kwa ustarabu si kitu ambacho wamefanya mara moja, hapana! Hao watakuwa wamefunzwa na wamezoea! Ni malezi mazuri sana haswa kwa karne hii ya 21 ambapo dunia imekuwa kama kijiji  huwezi jua ni wapi na nani mwanao atakutana naye hivyo lazima kujua jinsi ya kumudu mazingira!  Nilipokua nyumbani Tanzania mwanzoni mwa mwaka huu, watoto wake mdogo wangu walikuja kunitembelea. Sasa wakati wakula mie nikamwambia dada wa kazi kuwa haina haja ya kuweka chakula mezani aweke mkeka tukae chini tule! Tuliokulia kwenye mikeka utatujua tu ???  mwe! Kwani hao watoto waliweza kula?! Mara namuona yule mdogo anaangaika kuvuta kiti karibu na mkeka  na mkubwa  wa kike kalalia tumbo huku akijaribu kula ?? Nikawa nashanga, ndio mama yao akasema unajua wanangu hawajui kula huku wakiwa wamekaa kwenye mkeka!! Akasema "Wakenya hao wanajua kula ni mezani tu" ?? mbona yalinishuka ikabidi tuhamishie chakula mezani, basi wakawa na amani wakala kwa furaha!  Mdogo wangu alipoona hizi picha za Tiffah akanitumia na kusema kama mtoto wake angepiga picha hiyo ambayo ameshikilia glass ya juice baada ya picha za birthday ya Nillan kutoka basi baadhi ya watu angefikiri kuwa ameiga kumbe hivyo ndivyo alivyo walea watoto wake!...... Wazazi embu achaneni na kuwapa watoto glass za plastic kwanza zinaleta Cancer ??  honestly, bora umpe mtoto kikombe cha bati kuliko plastic! Nunua zile glass ngumu mfundishe mtoto kushika na kutumia bila kuvunja ili siku ukiwanae 5* hotel upati shida kwani kazoea! #Mlee mtoto katika njia impasayo naye hataiacha hata atakapokuwa mzee!!

""* Picha zote za Tiffah nimezitoa kwa Instagram page ya princess_Tiffah***

My 2017 best Tweet: “You are the air that I breathe”Kuna comment nyingi kwenye hii tweet ambazo zinachekesha sana sema nimechagua hizo tu!    

Ngoja niwaambie, kwakweli hakuna kitu kizuri kama kumuona mtu kama Dr Mengi anajishusha na kumuheshimu. kumpenda  mwanamke namna hii! Yani inavutia sana kuona mtu mwenye elimu yake nzuri sana, anapesa zake, na all the power kwenye public and yet he can humble himself like that! "You are the air that I breathe"! Hivi niwanaume wangapi wa Kitanzania ambao wamesoma labda wana Masters tu wanaweza kusema maneno Kama haya kwa mkewe ambaye elimu yake ni sawa na "sifuri" kwake?!! Enyi vijana wa Kitanzania jaribuni kuiga wazee kama akina Dr Mengi mtabarikiwa zaidi! ........And Nope! Wakubwa hawafaidi!! Muheshimu na umpende mkeo kwa dhati in private and in public nawe uone kama hauta faidi!! Muache ukatili!!!...........Kwa maana hiyo hii imekuwa my best tweet for 2017! Kama mjuavyo hii blog upendo ndio dini yetu, basi tumefurahi sana na hii tweet!

Baba_Dangote: when I say I love you true means it agah!…..The only thing I have in my life is you!

Love in the air! Hivi mnakumbuka wakati nilimtakia mama Diamond kheri ya kutimiza  miaka 50 nikauliza where is "step dad" kwasababu miaka khamsini bado kijana kabisa! Embu soma hapa (kheriyamiaka50MamaDiamond) Eeh, unajua haikukaa sana tukaanza kusikia fununu kuwa mama yake Diamond kaolewa!

Mama Diamond siku ya harusi yake
Najuzi kati kwenye harusi ya Romy Jones akatokea naye pia  mama Diamond alisema rasmi kuwa kaolewa na tusubirie mziwanda anakuja ?? uzee mwisho 'kanda ya Ziwa' huku Pwani wote baby ???

Sasa naona kila mtu ameshakubaliana na hiyo hali na baba wa kambo naye kawa huru hata kumposti mkewe na familia yake kwenye social media! Baba kafa kazimia kwa mama, mpaka kaamua kujiita "baba Dangote" kwenye account zake za Instagram ili kuendana na jinsi mama yake Diamond anavyo jiita kwenye social media. Binafsi, I don't see a big deal at all!! After all ni mumewe halali siyo boyfriend so what the fuzzy is all about! Ingekuwa just a "strange man" sawa lakini huyu kaka kafuata mila na sheria zote za dini ya Kiislamu kuoa hivyo sasa kunatatizo gani mtu kumposti mkewe wapekee hakuna maswala ya ukewenza kusema anampendelea?!! Jamani life is too short let others be!

Baba na binti yake
Maisha ya wanawake wengi wa Kiafrika ni ya shida, many don't get the privilege to enjoy their youth! Yani kuna maisha yaliyopangiliwa na familia pamoja na jamii mtu binafsi hupati nafasi ya Ku experience life and choose what is best for you! Nakama bado haitoshi, wengi wanafiikiria ndoa zitawapa furaha matokea yake emotional abandonment is all they experiencing!!.......... Kama kwa wenzetu Waislam wanaruhusiwa kuachana kiurahisi hivyo wanawake wengi wanaishia kuteseka kulea watoto wenyewe bila msaada wa baba zao! Hivyo, pale mwanamke anapopata mtu wa kumfanya ajisikie 16 again why not?!! Let her enjoy the youth life that was once snatched away from her!! Mimi hizi double standard za Wabongo hata sizielewi!! Wanaume wanaoa wasichana ambao wamepishana hata zaidi ya miaka 30 na watu mnaona sawa tu! Lakini mama wa watu wamepishana miaka kumi tu inakuwa shida?! Ni wivu ama?? Tatizo Nyota aa  ???  Haya, wenzenu wako honeymoon South Africa wakati nyie mnaojiona wasichana wabichi mnaambulia kupelekwa  Ramada Inn Bagamoyo, kwani mmekuwa waganga wa kienyeji  ??  ??? napenzi kama bia nileweshe ee chupa kilo mia nibebeshe ee ??  Halafu Baba Dangote handsome boy kweli kweli, he truly needed a "Nanny" to babysit him ?? BTW, hivi huyu stepdad hana watoto eeh? Mbona anasema "the only thing I have in my life is you"?! Kama hana basi hapo bi Sandra ata enjoy sana maana hakuna mambo ya ada za shule sijui uniform za watoto, Mara oh, watoto wanaumwa makamasi ?? inahusu?!????  #RULE YOUR LIFE

Crush diets vs Healthy eating

@Regranned from @open_kitchen2014 – Naomba leo kutoa ka elimu kidogo hizo picha mbili zote ni za mwaka huu hiyo ya kushoto ilikuwa mwezi wa nne na hiyo ya kulia ni december ila utaona kuwa kuna tofauti kubwa sasa hapo ndio uelewe tofauti ya bad crush diets na healthy eating with lots of muscle buiding kipindi cha mwezi wa tatu mpaka wa nne nilijaribu kila mbinu ili nipungue kilo 10 za mwisho zilikuwa zinanitesa sana sasa nikaanza crush diets na mazoezi yaani kwanza nilipozitoa zile kilo 10 ndani ya mwezi mmoja mwezi unao fuata zilirudi zote na zaidi nikawa very upset ndio nikaanza kusoma na kujifunza kuhusu crush diets vs healthy eating na pia nikaamua kuaza weight lifting vs cardio maana with cardio nilikuwa nanyooka tu sitengenezi shape at all nilikuwa kama mti wa fenesi ?????? lakini sasa hivi kidogo Alhamdulillah hata kijingu cha kukorogea uji kinaonekana japo sio cha kusimamisha chupa ila maji yanatuama kidogo ??????? .
So naomba ujue kuwa crush diets are not healthy kabisa kwasababu kwanza sukari yangu ilikuwa inashuka sana because nilikuwa nakula kidogo nafanya mazoezi zaidi and that was very dangerous nakumbuka kuna siku nimetoka kukimbia 10k nikahisi kuzimia nakuja kupima sukari ipo 3 yaani i was so scared so ni muhimu kuelewa madhara ya crush diets na pia ngozi yangu ilikuwa mbaya sana yaani nilikuwa najitahidi sana ku moisturise lakini bado ilikuwa haina mvuto mda mwingi ilikuwa inabebwa na make up ???? na pia nilikuwa so weak mda mwingi nina fatigue sana so i stopped huo ujinga kabis a .
..
Sasa hivi navaaa size 14/16 mwili wangu upo shaped vizuri na ninaendelea kila siku kuutengeneza sitaki kupungua zaidi ya hapo nimeridhika kabisa mimi sina skinny body frame so mwili wangu hauwezi kuwa kama beyonce never ever ???? lazima uwe na target inayoendana na body frame usije ukawa kama a walking zombie maana kila nguo ukivaaa unaoneka kama imetundikwa , uso mpaka unakosa nuru mtu akikuangalia sura inakuwa kama inamzomea ????mambo gani sasa hayo ..
. . So sasa hivi yes mwili wangu unaoneka thicker na abit more masculine and i love it AMKA TWENDE HATA WEWE UNAWEZA –

Mama Salma Kikwete ndani timu ya netball!

Mama yetu kipenzi mama Salma Kikwete ndani ya kivazi mwanana kabisa teyari kwa kuingia uwanjani kucheza mashindano  ya netball za timu za Wabunge wa Africa Mashariki hapo juzi kati! Inapendeza sana, inavutia, na kutia moyo wanawake wengine na mabinti unapo ona powerful figure Kama mama yetu hapo akijishusha kwa unyenyekevu na kufurahia maisha na watu wengine! Safi sana na hongera nyingi mama yetu!………… Mwaka jana naye Dr. AshaRose Migiro alituonyesha ujuzi wake wakupiga dana dana  tazama ?? BigUpDrAshaRoseMigiro

Mama Diamond amsifia mkwewe!

Pale mama mkwe anapokuwa msemaji wa penzi lako! Well!! Inakufanya ujisikie vizuri lakini bado huwalisia utabaki pale pale! Kama mwanaume hakupendi kwa dhati nawala hakuheshimu hata mama mkwe akupende vipi haitobadili kitu! Heshima na mapenzi yako kutoka kwa mumeo ni lazima mumeo haonyeshe mwenyewe nasio mama mkwe wala wifi zako au ndugu wa mumeo! …..anyway, yangoswe hayo ngoja tumuachie ngoswe mwenyewe!

Womanhood

Madam Rita katika ubora wake ? Kuna ubuyu fulani nautamania sijui niseme ?? simnaona kitu Cha Diamond kwa kidole cha madam?! So who is the “mystery man” behind that bling-bling? Wapenda ubuyu mtatujua tu ??……….  Anyway, madam wetu kapendezaje sana. I hope the mystery man is worth it all,  a woman like you who hassle like that deserves more than an average man! O’hello!! Can we talk?!!! she’s Madam Rita Paulsen for people’s sake! ?????

Womanhood!

The one and only Dr. Ellikunda Kihengu a.k.a Dr. Elly Kihengu kutoka Houston, Texas! When we talk about Tanzanian women in the diaspora, women with brain and integrity you can’t miss her name  unless you are hater ?? mzurije sasa, beauty and brain =Extra extra beauty in madam Rita Paulsen’s voice ?

Womanhood!

“Your mental growth totally depends on you and the effort you’ll make towards that growth. Feed your brain with the right information and you’ll see positive changes in your life, feed it with rubbish and that’s exactly what you’ll end up with. You only have one life to live, choose wisely!” JNM

Malia Obama ndani ya “hot topics”!

Ule usemi uliotumika sana na  wahenga wetu kuwa “mtoto umleavyo ndivyo ukuavyo” unaweza usilete maana sana katika kulewa watoto wa karne hii ya 21! Hivi karibuni kama wiki na siku kadhaa zilizopita binti wa Mstahafu Rais Baraka Obama, ajulikanae kama Malia Obama alikutwa akibusiana na mwanaume ambaye aliaminika kuwa ni boyfriend wake katika viwanja vya chuo kikuu cha Harvard university na pia alionekana akivuta sigara. Tazama kwenye hii video kuanzia dakika ya 22.50 kama inavyoelezewa na gwiji wa “hot topics” Wendy Williams  ?

Sipati picha Michelle Obama alikasirikaje, unaweza zimia bila “kizimio” ?? Halafu sasa kutokana na sheria za huku Malia Obama anatambulika kama mtu mzima ambaye anaweza fanya maamuzi yake binafsi na wazazi wanatakiwa kuyaheshimu! Najua hata Africa ukishafika 18+ unatambulika wewe ni mtu mzima kwenye karatasi za serikali lakini kiuhalisia wazazi wetu wengi bado wanakuwa na mamlaka juu yetu na kutufanyia maamuzi mengi juu yetu. Ni mfumo wa tamaduni zetu ambao unafanya watu wengi kutokuwa na mawazo huru na kufanya maamuzi ambayo yanampendeza yeye na kwafaida yake kwanza. Funguo za furaha zetu zipo mikononi mwa watu kama wazazi, marafiki, na jamii na ndio maana wengi ni wanafiki na waongo kupita kiasi!  Lakini vile vile lazima tukubaliane kuwa kila familia lazima iwe na identity yake! Kila mtu anazaliwa tofauti lakini kama familia lazima muwe na kitu kimoja ambacho watu watajua na kuwatambua nacho. Hivyo sishangai kwanini Michelle na Baraka wamekasirishwa na kitendo hicho. ……..Mungu atusaidie sisi ambao tunataka kuzaa na wale ambao wanalea katika karne hii ya 21 kwani changamoto ni nyingi mno!

JNM: Where there’s passion, perseverance and dedication there’s always a reward. Keep going!

“Where there’s passion,perseverance and dedication there’s always a reward. Keep going!” ———-JNM

Zarinah Hassan: We have been created so different, the type of humans who can multi task

“There is so much in a woman that most people don’t know. We have been created so different, the type of humans who can multi task. A man can watch a game and not hear what one said while a woman can watch a movie and still hear, still know the stove is on, and so on (the list is endless). So here is to all the multi tasking women juggling through life as mothers, wives, momprenuers aka business women, caregivers and many more. You are appreciated! It’s all about knowing what comes 1st #prioritize. Salute? help me tag one woman who inspires you. @lukambaofficial ?” ——-Zarinah Hassan

Tamar Braxton amekwenda mahakamani kuomba talaka!

Nashindwa kuelewa ni kitu gani huwa kinatokea, ndani ya miezi michache watu wanakataa kabisa kuwa ndoa yao ipo sawa na hizo rumors ni maneno tu yamtaani!! Wanathubutu hata kumtaja Mungu!! Halafu hamjakaa sawa mnasikia wame file for divorce kuwa wameshindwana! Sasa najiuliza why lying!?! Kama ndoa inamatatizo si unasema tu, kuwa ndoa yetu haipo sawa lakini we are working on it, just pray for us!! Kuliko kudanganya!! Kama hapo ?kwenye video Tamar na mumewe walivyo jieleza kwenye Wendy Williams show mwezi wa tatu mwaka huu embu wasikilize

Kana kwamba hiyo haitoshi hata mwezi uliopita alipo ulizwa akasema yupo teyari kufanya chochote kile kulinda ndoa yake. Na hivyo kitu chakwanza ambacho anafanya ili kuokoa ndoa yake ni kuachana na "showbiz business" ataacha kutengeneza album za nyimbo mpya! Sasa within 30 days inakuwaje mtu huyo huyo ndio anakuwa wakwanza kudai talaka ??  I don't get it!.......

Lakini ukiangalia kwaundani utagundua huyu Tamar kuacha kuimba siyo kwasababu alikuwa anataka kuokoa ndoa yake bali ni njia ya kumuondoa mumewe kuwa Manager na producer wake. Kama mnakumbuka how Lady JayDee alivyo mfanyia Captain Garnder Habash ?? smart lady huh! .......Jamani let your husband be your husband! Mambo ya mumeo kuwa Manager wako kwakweli naona ndoa nyingi zinavunjika ni wachache mno wamefanikiwa. Labda kama huyo mumeo hachukui pesa yoyote kwenye hiyo production yako. Your husband / wife is your business partner and advicer but not someone to manage you everyday, no no! You can only meet at the board meetings or kwenye weekly business meeting. Lakini kila mtu awe na ofisi yake na wafanyakazi wake nafikiri kwa njia hii itapunguza tension fulani zisizo na ulazima!

Halafu pia kitu ambacho nimeona wanandoa wengi ambao wako kwenye the same industry ndoa zao hazidumu au zinakuwa na matatizo sana. Kwamfano, hapa Tamar ni muimbaji na reality TV star wakati mume wake ni producer mkubwa kwenye music na TV show hivyo wote wapo kwenye spotlight na mzunguko wa watu hao hao kila wakati! Lazima wanandoa wawe makini sana mnapokuwa kwenye maswala ya business ili ndoa yenu iwe na amani.  Sasa Tamar na Vince walipo owana hawakupeana "prenuptial agreements" kwani walikubaliana kuwa divorce is NOT an option! Sasa pale divorce inapokuwa ni the only option sijui itakuwaje kwani Tamar anataka full custody ya mtoto wao na pia anasema Vince asipewe spouse support. Kumbuka wakati Tamar anaolewa na Vince, Vince ndio alikuwa anatengeneza pesa nyingi lakini baadaye Tamar akawa super star na kutengeneza pesa nyingi zaidi ya Vince hivyo sasa itabidi Tamar amlipe Vince pesa za kujikimu baada ya divorce..... Vince ni yatima na kwao alizaliwa mwenyewe hivyo hana ndugu wa tumbo moja wala wazazi! So sad!

Couple nyingine ambayo imeshangaza watu ni ya huyu mwanadada wa The Real talk show ?? Jeanie Mai na mumewe Fredy! Hapa mwanamke ndiye aliyesema kuwa yeye hataki kuwa na watoto kwani haoni kama atakuwa mama mzuri kwani kulea kiumbe kingine na kumfanya awe ni kiumbe bora is a tough job ambayo yeye hawezi. Pia kwasasa yupo busy na "carrier" yake wakati mumewe anataka wazae watoto kitu ambacho hawezi fanya. Kutokana na history yake ya kutoka kwenye familia duni wazazi wake waliangaika sana wakaja Marekani kutafuta maisha bora haswa kwa watoto wao. Hivyo kuwa na watoto kuta slow down dream zake ambazo yeye na wazazi wake wameteseka sana kuzipata. Nabado kuna watu masikini kwenye familia yake ambao anaona kuwa anawajibu wa kuwasaidia hivyo kuleta watoto duniani itakuwa ni mzigo mwingine wa watu wanao mtegemea! Hayo ni maisha ya Marekani kule kwetu Africa masikini ndio wanazaa zaidi ya matajiri wanajua mjomba/ baba mdogo au shangazi atawalea tu bila shida ??

Hivi, mimi nashindwa kuelewa hivi dunia hii kunawatu wanaowana bila kujadili kama wanataka watoto au hapana!! Hivi si vitu vinajadiliwa kabla hata ya kuchumbiana au mie ndio sijui ?? nielewesheni ?? mie I would love to know what am I signing up for, sorry naogopa sana kujifunga kitanzi mwenyewe! Naogopa surprises .........Kumbuka Tamar Braxton alikuwa kwenye show hii kabla ya ufukuzwa mwaka jana!

 

Mpende akupendae…….!

Mpende akupendae asiyekupenda achana naye! Acheni wenye ndoa zao halali wajishaue babu! Kwa raha zao ??

The C.E.O herself! #Molocaho

Nani Kama Jacqueline!! The C.E.O of Molocaho furniture katika ubora wake!  Nampendaje sasa!! Mzuri wa sura, shepu, mpaka roho! Kuna wanawake wengine japo ni wazuri wanavutia lakini usiombe ukae nao karibu utajuta!! Wana roho mbaya mfano hakuna, hawapendi kuona wengine wanafuraha kwani maisha yao ni vilio kila siku!! Halafu maendelo ya wengine ni chungu kwao kumeza kama mwarobaini!! ……Ubarikiwe sana Mrs Billionaire ?? 

A day in the life: Siku ya maisha yangu na Emelda Mwamanga

Emelda Mwamanga (Kushoto) pamoja na Dorothy Kipeja ambaye ndiye mmiliki wa show hii ya A day in the life

Wow! I’m super happy Bang Magazine is coming back!!! My wishes came true! Ni miezi michache iliyopita nilikuwa nauliza kuhusu Bang Magazine kama itarudi sokono (SomaHapa), na katika video hii fupi inayo onyesha maisha ya Mama / Mke / C.E.O / Entrepreneur lady / Motivational speaker and now what an Author?!  (ma’am this lady can do it all huh!! I only have this blog and can’t even keep up with it ????)  Emelda Mwamanga ambaye ndiye mmiliki wa Bang Magazine ametamka kuwa Bang Magazine inarudi sokoni muda si mrefu! ………So happy for you Emelda! Nice show, good job! Love it!!

OMg! Huyu ndio yule shemeji yetu walimuita “mission town”!?!

Jamani njooni muone Zamaradi anatenda miujiza!!! Sitaki kuamini kuwa huyu ndie yule shemeji yetu wa taifa aliyeitwa “mission town” na wale Shilawadu (SomaHapa), Eeh! Hata mwezi haujafika tangu waowane teyari Zamaradi kaweza kumbadilisha mission town to “brown sugar” ???  You all know that movie “Brown Sugar” right?! Siunaona anataka kufanana na Dre (Taye Diggs) ??? shemeji yetu kaogeshwa akatakata, anapendeza na kuvutia hadi raha!! Sasa najua kwanini yule mtu mzima alilia kwa uchungu vile utafikiri alipata taharifa “Professor” kafa ???  Hongera sana Zamaradi you are a real woman, najua soon tutasikia nayeye anamiliki entertainment media fulani amazing hivi! O’yes! He can ??…….. Mbarikiwe sana

Lieutenant Major General ndani ya jiji la Dar!

Yessss!! The Lieutenant Major General of Tanzania and Uganda ndani ya jiji la Dar es salaam! And Paparazzi couldn’t give her a space!! ?? I guess they missed her so badly ?? …………

You go Zari!! Tell them you have been and always will be the “Queen of the castle”!  Nawaache mfanye kazi! hizi zama za Mgufuli ni mambo ya #Hapa kazi tu!  hakuna hela za mission town ?? ……… BTW, I love they way you have decided to separate  your platforms! Msaidiane katika kila jambo but don’t step on each other platform! Na maswala ya mapenzi weka private unless you want to share with me ???? please msininyime hizo love story zenu ??