Category Archives: Mother and daughter moment

Mama na mwana: Hakika wema na fadhili zako zitanifuata siku zote za maisha yangu!

Ni kwa neema tu! Nasema ni kwa neema yake Mungu kwani akili yangu haikuwai kuwaza kuwa ipo siku kama hii! Hivyo namshukuru sana Mungu kwani ni hakika wema na fadhili zake zitanifuata siku zote za maisha yangu, nami nitadumu ndani yake! Nimeweza kuona ukuu wa Mungu kwa kufanikisha uumbaji wake! Amenibariki na rafiki wa kweli ambaye upendo wetu utadumu milele na milele! ย ………Najua tunamipango mingi sana naomba Mungu azidi kutuwezesha katika kila jambo! Moja ya vitu ambavyo nasubiri kwa hamu sana ni passport ya mwanangu!! Yes! her American passport!! Ee Mwenyezi Mungu mimina baraka zako!! Yani can’t wait!! Maana tutatembe hii dunia mpaka ndege zinune ย zigome kabisa kuruka ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ ……..Anyway, namshukuru Mungu kwa mbaraka ย wa huyu mtoto! Naomba azidi kunilindia na kumuongoza katika kila jambo haswa kiroho, asikae mbali naye!

Mother and daughter moment

Akothee na mama yake mzazi

๐Ÿ˜…๐Ÿ˜… ngoja nicheke kwanza, maana Akothee ananifurahisha sana! I think she is a sister I need ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…๐Ÿ˜… ……. Yani Akothee anajua how to do a “role” change! Akiwa kanisani siku ya Sabato utamjua ndo yeye anavaaga Vi-min na kukatika kwa stage ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ Yani hadi kilemba ile Luo style anafunga siku ya Sabato na sadaka anakusanya. ย Na akiwa anakula #bata ni anakula kweli kweli. Sasa kama hapa yupo na mama yake mzazi, muangalie alivyo tega masikio kwa usikivu utafikiri sio yeye. So funny! Wamependeza sana! …….Akothee I know you are my loyal reader, but I want you to be my sister please, I know my sisters love me but they don’t mind to share with you at all ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ We will drive this world crazy, I can tell ๐Ÿ˜๐Ÿ˜……. Nice pic Akothee, say hello to mama!

Mother and daughter moment!

Nimependa sana hii picha ya Mwamvita Makamba na mama yake! Wamependeza sana. Ilikuwa ni sherehe ya mdogo wake Mwamvita ina itwa “bag” party mie ndo nimeona leo mwe kama kawaida yangu kama kitu nilikuwa sijui basi nawaeleza tu ukweli! Watu walipendeza sana. Nimeipenda!

Mother and daughter moment!

Beautiful Emelda Mwamanga na binti yake Gabby! So nice! Nivizuri kuwapenda watoto wetu zaidi wakiwa katika umri huu mdogo kwani inawajengea kuamini, kutambua thamani yao wakiwa wakubwa, ย na kuwa wajasiri! Mtoto yoyote yule anahitaji muongozo, na mipaka lakini pia anahitajika kuwa huru haswa kifikra! Hivyo nijukumu la mzazi kumjenga mtoto wazingira huru ya kujieleza na kutafakari ambayo yana boundaries at the same time!
Mtoto siyo mdoli jamani, mfunze mtoto maadili mema, na jinsi y kuweza kukabiliana na hali zote za maisha. Kwamfano hapo Gabby unaona amefundishwa kupika na kuchanganya vitu kwa kutumia blander hivyo hata akienda kwa watu ambao wanatumia "high tech" kitchen appliances hashangai sana. Napia anajua jinsi ya kutumia mikono yake kushika vitu! Nilishawahi kuona kwa macho yangu mtoto wa miaka nane (8yrs old) bado anatawazwa akimaliza kutumia choo ๐Ÿ™ˆ๐Ÿ™ˆ Yani anajisaidia haja kubwa halafu anita dada wa kazi au mama yake amsafishe! And the mother was very OK with it ๐Ÿ™Š๐Ÿ™Š Jamani!! Anyway, those are rich people problems, maskini kama sisi tutayawezea wapi? ๐Ÿ˜…๐Ÿ˜…

 

Ndugu wanapokutana…….!

Pale ndugu wanapokutana ni furaha kwa kwenda mbele! ........mama akipata kumbukumbu ya picha na binti yake kwa furaha ya kuonana tena baada ya miezi kadhaa kupitia! Magreth akimpokea dada yake Elline kwa furaha sana!.......... ย kwafaida ya wasomaji wangu, Elline ni dada yetu mkubwa, mimi ndio namfuata. Yeye alikuwa anaishi Geita lakini mwezi uliopita wamehamishiwa kikazi Makao Makuu (Dodoma). Hivyo sasa ni wakazi wa Dodoma! ........Tunamshukuru Mungu kwa yote!ย 

Mother and daughter moment!

Mama na mwana wakiwa katika mazingira safi kabisa ya Kisumu International Airport, hapo nchini Kenya! Hii Airport kwa muonekano tu wa nje inaonekana ni safi zaidi ya ile ya kwetu pale Bongoland! Japo hii ipo nje ya mji wa Nairobi lakini inavutia kwa usafi sana........Ni nini haswa tatizo letu sisi Watanzania! Maana hata mazingira yatengenezwe mazuri vipi haichukui muda utashangaa jinsi yalivyo chafuliwa, na kuharibiwa! Saa nyingine tunailaumu serikali kwa mambo ambayo ni sisi wenyewe ni tatizo! Kweli aliyeturoga kafa!.........Picha hii imepigwa week na siku kadhaa sasa wakati mama Igogo alipokuwa amekwenda kwenye msiba kwa wakwe zake na binti yake!

Motherhood!

Mama na mwana! Pendeza sana mama yetu so beautiful! ย Happy belated Mother’s Day to you mama yetu we love you ๐Ÿ˜ Btw, Dinnah na mimi tulisoma wote CBE Marketing major natulikuwa roommates. ย Dinnah ni ana akili usipime hata waliosoma naye UD watashuhudia! Plus msafi sana kama mimi vile ๐Ÿ˜๐Ÿ˜

 

Mother and daughter moment!

Wema atinga Chadema bega kwa bega na mama yake! Limekuwa si jambo la kushangaza sana kuona mama Sepetu akiwa mguu kwa mguu katika maswala yanayo muhusu binti yake Wema Sepetu, japo kwa safari hii imekuwa tofauti kidogo na matukio mengine anayo yafanya!…….Wema amemwaga manyanga ya CCM na kubeba manyanga ya Chadema juu tena kwa madaha na mbwembwe nyingi huku mama yake mzazi akiziunga mkono na kuzibariki mbwembwe hizo!……. ย Je, nguvu ya mrembo huyo yatosha kumng’oa Magufuli ย / CCM madarakani?!! Mimi sijui kwani Siasa isn’t my cup of StrawberryMango smoothie! Bali naweza sema tuombeane uzima ili tushuhudie mambo 2020!……wishing her the best in her handover!

Nitarejea…….!

Hello wapendwa wasomaji wangu, natumaini wote hamjambo. Mie mzima wa afya hofu na mashaka ni nyie mlio mbali na upeo wa macho yangu ๐Ÿ™‚ ๐Ÿ™‚ ๐Ÿ™‚ ……..wapendwa nime wamiss sana ila naomba mnivumilie tu simnajua nipo Bongoland na mambo ni mengi lakini soon tutarudi katika hali yetu ya kawaida na kwa nguvu mpya!…..Hata hivyo nawashukuru sana Halotel kwa ย internet ย ya uhakika! Nawasii wote tumieni mtandao wa Halotel kwa mawasiliano yenye viwango vya kimataifa!……..Nitarejea….!

Mother and daughter moment

Katika wazazi ambao nawahurumia pia na mu-admire sana ni mama yake Wema Sepetu! Ni mmoja wa wazazi ambao wanapitia changamoto nyingi sana katika maisha ya kila siku kutokana na maisha ambayo binti yake ameamua kuishi; hivyo kahilo namuhurumia sana! Lakini kama nilivyowai kusema huko nyuma (somahapa) kuwa ni mama ambaye ananifurahisha sana na jinsi anavyo simama bega kwa bega na binti yake, katika mabaya na mazuri! Kwa wazazi wa Kiafrika ni ngumu sana! Wachache mno wanaweza fanya afanyavyo mama Sepetu! Na kwasababu hiyo anakua mfano mzuri sana wa kuigwa! Mtoto wako ni mzigo wako mpaka kifo. Huwezi mkana au mkataa mtoto wako eti kwasababu tu haendani na maisha utakayo! Big up mama Wema!

 

Mother and daughter moment!

Mimi hapa na mommy anguย ๐Ÿ™‚ย hapa ni siku ya Juma Mosi iliyopita tukiwa nyumbani Keko Juu teyari kwa mtoko wa harusi ya mtoto wa jirani yetu and a good friend to mamaโ€ฆโ€ฆ.Jamani sasa hivi tunaishi mbali hivyo tukitaka kwenda kwenye sherehe za maeneo ya Tabata, Mbezi n.k inatubidi tulale kwenye mji wetu wa zamani (Keko Juu) kwani wakati wakurudi kuna kuwa mbali na kabla ya kufika home kuna pori fulani hivi huwa hatupendi kupita usiku sanaโ€ฆ.Sasa hivi nafikiri itabidi kuangalia sana sherehe za kwenda kwani usalama wetu ni muhimu sana japo so far hatujawahi sikia kitu chochote kile ambacho ni cha kutishia amani au usalama wa eneo hilo!

mother and daughter moment!

Foster na mama yake wakiwa Dubai wakati wa family holidays vacation ya 2016! Wamependeza sana

What a lovely picture of Nambua na mama yake, beautiful and inspiring! ……by the way ushawahi kusikia Cassandra Lingerie?! Wanakwambia “Mwanamke vazi la ndani”! Yani huko ndipo mambo iko kwa wasichana na wanawake wanaojijali na kujithamini fika Cassandra Lingerie ukajionee mwenyewe!

Mama Foster na binti zake waki enjoy vacation yao, so cute!

Mother and daughters moment

screenshot_2016-11-22-13-16-52-1fb_img_1479842379658Raha sana pale watoto au mtoto wako ndio anakuwa rafiki na shabiki wako number moja! Yani ni mbaraka wa pekee kwani kuna wamama wengine mmmh! Wamama wa DotCom yani hata watoto zao wanawakimbia! ๐Ÿ™†๐Ÿ™†๐Ÿ™† Yani LB namfananisha na Kris Jenner mama yao Kim Kardashian jinsi alivyo karibu na watoto wake hadi raha!
fb_img_1479842349202
Wamenoga eeh! Wanavutia sana! Hata kama huwafahamu lakini lazima utakuwa unajisikia furaha kuwatizama!…….. Mbarikiwe sana LB na familia yako!