Category Archives: General education

Mama Salma Kikwete umekosea sana! Hiyo inaitwa institutionalized discrimination!

Hivi ule usemi wako wa “mtoto wa mwenzio ni wako” uliufuta baada ya kuvua kofia ya u-FirstLady!! Bado najaribu kukutafakari nia yako haswa ni nini?! Wahenga walisema “uchungu wa mwana aujuae ni mzazi” lakini mimi saa nyingine napingana na huu usemi kwani kuna watu hawajawahi onja machungu ya uzazi wala malezi lakini wanaumizwa na kuguswa na watoto wa wengine kuliko baadhi ya wanawake walio zaa! Hapa simuongelei  mwingine bali ni aliyekuwa mkuu wangu ya shule ya Kowak Girls Secondary school Sister Magdalena (R.I.P). 

Miaka 23 iliyopita, nilipopata ujauzito nilikuwa form 2 pale Kowak Girls Secondary school Wilaya ya Rorya, mkoa wa Mara. Shule ilikuwa inaongozwa na wamishonari wa Catholic na huyu Sister Magdalena ndio alikuwa Headmistress (yeye alikuwa Mmarekani) na msaidizi wake alikuwa Sister Nyambosa  ambaye alikuwa Mtanzania. Sasa Sister Nyambosa kulingana na the so called “mila na desturi, sheria za Tanzania na dini” alitaka nifukuzwe shule!! Eti hiyo ndio adhabu yangu nikajifunze! But guess what?!! Sister Magdalena akasema NO! Hato hidhinisha hiyo barua ya mimi kufukuzwa shule kwani haoni logic ya hizo mila na desturi, pamoja na sheria za Tanzania. Yeye aliamini kuwa kitendo cha mimi kuwa mama kwa umri ule ni adhabu tosha! Pia nilikuwa mmoja ya wanafunzi wazuri pale shuleni hivyo hakuona kwanini aniharibie future yangu kwa kunifukuza shule ambayo technically angekuwa anaharibu future ya watoto wawili (mimi na kiumbe kilichokuwa tumboni mwanangu wakati ule).

Kufupisha story hii, wakafikia makubaliano yakunipa sick leave mpaka nitakapokua tayari kurudi shule basi wao walikuwa tayari kunipokea au kunipa uwamisho kwenda shule nyingine! Miezi sita baada ya kujifungua nilitafuta shule nikahamia, uhamisho wangu ulitumwa bila tatizo!! Shule niliyo hamia ilikuwa ni Nurulyakini Secondary school pale Mwembe Yanga, Temeke. Nilirudia form 2 kwani nilikuwa sijafanya mtihani wa form 2 nilipokuwa nimetoka Kowak. Wanaonijua vizuri wanaweza kushuhudia kuwa hata siku moja sijawahi kuwa ashamed kusema kuwa mimi nina mtoto. Kwani miezi mchache tu hapo shuleni nilianza kuwaambia wanafunzi wenzangu na hatimaye story zikafika hadi kwa walimu wote wa shule! Guess what?! Hakuna aliye jali wala kunifanya nijisikie vibaya kuwa mimi ni mama katika umri ule!! Walichojali ni academic records zangu! Tulipoingia form 3, nikachaguliwa kuwa Assistance HeadGirl, na nipofika form 4 wakanichagua kuwa HeadGirl na hiyo yote ni kwasababu ya jinsi nilivyo kuwa hapo shuleni walimu walipenda sana na kuniona as a blessing to their school.

Nakumbuka siku moja dada aliyekuwa ananiangalizia mtoto alikuwa anaumwa hivyo hakuweza kukaa na mtoto siku hiyo. Ilikuwa ni wiki ambayo tunafanya final exams review kwa ajili ya kuanza final exams za form 4!! Nilikuwa na 2 choices; ama nisiende shule nibaki nyumbani nimuangalie mwanangu au nimbebe mwanangu niende naye shule! Sikiliza mama, jinsi walimu wangu na wanafunzi wenzangu walivyo nifanya nijisikie wakawaida kama wao, yani wala sikufikiria mara mbili!! Nikamuogesha mwanangu nikajiandaa nikaendanae shuleni. Nipo darasani nasoma na mwanangu yupo pembeni yangu! Hakuna aliyeniona waajabu wala nini!  kila mtu alikuwa anamfurahiya mwanangu!! And for the records nilifaulu vizuri sana form 4!

Mama yangu sikiliza, tatizo lolote lile hata liwe kubwa kiasi gani ilikutafutiwa suluhisho la kudumu inategemea na attitude ya jamii husika na viongozi wake! Embu tafakari kama Sister Magdalena asingeweka msisitizo kuwa hato hidhinisha hiyo barua ya kunifukuza shule mimi ningekuwa wapi leo?!! Vipi kama walimu na wanafunzi wa Nurulyakini wangenibagua na kunitenga je mimi ningeweza endelea na masomo yangu?! Je, maisha yangu na ya mwanangu yangekuaje kama nisingepatiwa nafasi ya pili ya kufanya matengenezo?! Maana hivyo vyeti vyangu I mean my academic records ndio vilivyonileta hapa nilipo leo hii!! Labda nikwambie tu kuwa Nurulyakini ni shule ya Waislamu!

Hii tabia ya kutokutoa nafasi ya pili kwa “wakosaji” ndio inaleta matitizo mengi ndani ya Tanzania kama mambo ya vyeti feki, na forgeries nyingine! Viongozi wenye mtazamo kama wako ndio wanao changia matatizo kama hayo niliyo yataja katika jamii yetu!

By no means, siungi mkono maswala ya wanafunzi wa kike kupata mimba wakiwa mashuleni. Hata mwanangu analijua hilo kwani niliongenae mapema mno nilipo ona anaakili za kutosha kuelewa kile nitakacho mueleza. Lakini naomba uwelewe kuwa tatizo si kupata mimba, tatizo ni familia, jamii, na serikali imeshindwa kuelewa kuwa kuna uhitaji mkubwa wa kuelimisha familia pamoja na jamii nzima kuhusu swala la kujamiiana na changamoto zake haswa kwa watoto wakike! Leo hii unasema waliopata mimba wasiruhusiwe kuendelea na shule, ok! Fine! Vipi wanao adhirika na magonjwa Kama HIV, gonorrhea, genital herpes, syphilis, n.k  hao mnawafanyaje?! Kwani hayo pia siyanatokana na ngono??! Hauoni kama kuna haja ya kuwataka madaktari wawataharifu shule mara tu wampatapo mwanafunzi anaugonjwa wowote wa zinaa ili nao wafukuzwe shule?? Mbona mnawaonea wanaopata mimba peke yao?! Ooh! Au mnaonaje muanzishe sheria ya watoto wakike kukagualiwa kama wako sexually active au bado kabla ya kuingia shule katika kila muhula?! Labda hiyo ingetoa fursa sawa kwa mabinti wote! Na wanaume je mgewafanyaje?!!! Acha ubaguzi na unyanyapaaji mama yangu?!

***ITAENDELEA……… ***

“msichana nilieona kila aliezaa amepoteza dira, kiufupi ni kama shughuli imeisha…..”~~~~~Zamaradi Mketema

“Nakumbuka kama miaka sita nyuma nilikuwa msichana tu, tena msichana nisie na ndoto hata za kuwa na mtoto, msichana niliyekuwa na picha tofauti juu ya wale wanaozaa, msichana nilieona kila aliezaa amepoteza Dira, kiufupi ni kama shughuli imeisha.

Lakini leo nimezikana hisia zangu mwenyewe baada ya kuwa na watoto (sio hata mtoto mmoja) ninapogundua kumbe maisha ndio YAMEANZA, kumbe kuna raha ambayo hata ningehadithiwa bado nisingeweza kuelewa hisia zake, kumbe hakuna kuchoka, na zaidi lwa wale walio single Mamaz bado una nafasi ya kutakwa na yoyote yule na akakuona kama bado wa jana na kukuheshimu na kukupa thamani ya hali ya juu, kiufupi unaweza hata ukawakimbiza ambao hawaijui leba ?? na yote ni kwakuwa bado unapendeza, bado unavutia, hakuna kilichopungua zaidi ya kuongezeka kiufupi ni hisia tamu mno

Kama wewe ni MAMA na unajivunia kuwa MAMA huku ukiendelea bado kujiamini embu nyoosha mkono juu!! Nafikiria kuandaa kitu cha kutukutanisha WAMAMA WOTE WA KISASA ambao hawajajitupa na huku bado wako proud na UMAMA wao iwe siku ya kuonyrsha how fabulous you are hata kama una mtoto / watoto, iwe ni siku yetu ya kujidai na kupendeza, iwe ni siku ya kuprove wanaona kuzaa ndio kuisha na kuchoka…Bila kusahau RED CARPET MOJA YA HATARI MNOOOO.

WANGAPI WANGEPENDA KUSHIRIKI KITU CHA NAMNA HII!!??  SEXY MAMAS ARE YOU OUT THERE!!??” Zamaradi Mketema

MAONI YANGU MIMI ALPHA: Sijashangazwa na mtazamo ambao Zamaradi alikua nayo huko nyuma. Kwani hivyo ndivyo govt. System nyingi za Africa zimeweka mfumo wa kuwafanya wasichana walio zaa bila ndoa kuwa hawana maana wala faida kwa jamii. Na hii mifumo ya serikali zetu inaundwa na jamii zetu husika ambazo ni jamii zilizo jaa fikra potovu za kuhukumu na kuadhibu watu bila kutafuta chanzo na suluhisho la tatizo liliopo. Kuzaa sio mwisho wa maisha! …….Enjoy the party! 

 

Mama Salma Kikwete umekosea sana! Hiyo inaitwa institutionalized discrimination!!

Sipendi kuongelea maswala ya siasa tena kwa hii blog ila kuna mambo ambayo nikiona kuna umuhimu wa kutoa maoni yangu basi nitafanya hivyo. Mama yangu mama Salma Kikwete unajua nakupenda sana. Jambo kuu katika sheria za upendo ni kumwambia mtu ukweli pale anapo kosea. Basi nami naomba nikwambie kuwa  mama yangu umekosea sana!

Nimesikiliza kwa makini hoja yako juu ya wanafunzi wanaopata MIMBA wakiwa mashuleni ikanigusa kwa masikitiko makubwa sana kwani huyo mwanafunzi ambaye wewe unamuongelea LEO alikuwa ni mimi MIAKA 23 iliyopita! Siamini leo hii baada ya miongo miwili kupita hili swala bado halijatafutiwa suluhisho chanya ndani ya Tanzania na leo hii inabidi nisimame kuwatetea waathirika wote wa mimba za utotoni/ mashuleni?!

Awali ya yote naomba utambuwe kuwa hakuna binti yoyote anayependa kupata mimba akiwa shule. Lakini hiyo haimaanishi kuwa wanaopata mimba ni wanadhambi kuliko wale ambao hawajapata mimba au wanaotoa mimba. Hii stigmatization na discrimination kwa wanafunzi wanaopata mimba au mabinti wanaopata mimba kwenye umri mdogo lazima jamii ikemee kwa nguvu zote. “Structured” life style ndio tatizo kubwa sana katika familia na jamii  nyingi za Kiafrika haswa Tanzania!!

Pili nani alisema mimba ni ugonjwa unaomzuiya binti kuendelea na masomo yake?!! Mnapo mzuiya huyu binti kuendelea na masomo yake vipi kuhusu mwanaume aliye mpa huyu binti mimba?! Yeye anapewa adhabu gani?? Kwanini watoto wakike ndio wamekuwa wa kubebeshwa lawama na mizigo yote bila kuangalia both sides of the coin?? Hivi hizi mimba huwa wanajipa wenyewe au?! Na vipi wale ambao wanapata mimba kwa njia ya ubakaji nao wapo kwenye hukumu hii au?!!

Mama yangu, umesema vitabu vyote vya dini Qur’an na Bible eti vinakataza watoto wa kike kupata mimba kabla ya wakati?! Ni wakati gani huo unao uongelea wewe?! Mimi sijui juu ya Qur’an lakini naelewa Bible takatifu inasema “waacheni watoto wote waje kwangu maana ufalme wa Mbingu ni wao” haikusema watoto waliozaliwa na mama wa umri gani wala katika mazingira gani!! Bible imekataza UZINZI tu! Na hilo ndio swala ambalo jamii yetu bado ipo kwenye koma ya mawazo mgando halitaki kuliongelea kinaga ubaga!!

Unaongelea mila na desturi za Mtanzania halafu unachanganya na Biblia?! Unajua hapo ndipo watu wengi wanapojichanganya! Kama mnataka kuongelea mila basi msimame na mila zenu bila kuingiza vitabu vya Mungu! Halafu muache kwenda kule Ukuryani na Umasaini kuwaambia waache kukeketa watoto wakike kwani hata wao wanafuata na kutunza mila zao!! Mnaongelea mimba za watoto washule na kuwahukumu kwa kutumia neno la Mungu, vipi wababa wanao zaa nje ya ndoa hao mnawapa adhabu gani? Vipi wanaume wa Kikristu  waliofunga ndoa na wana vimada nje au wameowa wake wawili wakati Biblia hairuhusu?!

Mama Salma, dunia yote sasa hivi inaongelea jinsi ya kumnyanyua mtoto wa kike ili aweze kupambana na maisha hata kama atakuwa amepata changamoto za aina gani, sasa wewe unataka kuzidi kuwakandamiza watoto wa kike kwa sababu ipi haswa?! Je, unajuwa waathirika wakubwa  wa hii institutionalized discrimination yako ambayo unaipigia debe ni wale watoto wanaotoka kwenye familia duni?! Kwasababu ninahuwakika nyie wanenu wana uwezo wa kwenda kupata vidonge vya mpango wa uzazi wakati wowote hivyo hawa wa wenzenu ndio mnawaona wadhambi sanaaaa!!

****ITAENDELEA……****

 

“You can never be faster than destiny.”

You can never be faster than destiny:Until its GOD’S time, it can never be your turn. When GOD is ready, everything and everybody will be forced to be ready. They will have no option than to work in your favor. Your helpers will have no rest until they locate you. Protocols will be broken for you to be promoted, elevated and celebrated. You will be unstoppable. (Collected)
#Akininspirational

“Strategic plan yako unaijua? Ipoje?” -Dr Blandina

Hii ni very late post, lakini mtaniwiya radhi kwani I only blog at my spare time! Wenzetu wanasema “better late than never”! Nitukio ambalo lilikuwa limeandaliwa na organization ya Vital Voices wakishirikiana na Dare To Dream foundation! Kiongozi wa shughuli yote alikuwa ni Emelda Mwamanga (Mrs) ? ambaye ndie Mkurugenzi Mkuu wa Dare To Dream foundation, Bang Magazine, na pia ni “mshika bendera” a.k.a Ambassador wa Vital Voices Tanzania! Mgeni rasmi alikuwa ni Mh. Devota Likolola  (Mbunge viti maalum) 

Janeth Igogo (left), Mh. Devota Likolola, Myself, na TV host Marion Elias

Tukio zima lilifanyika siku ya Jumamosi, tarehe 08, March, 2017 katika ukumbi wa Danken Hall pale Mikocheni. Ambapo yalianza kwa kutembea kidogo huku wanawake wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali kuwakilisha sauti ya vilio vya wanawake wote inchini Tanzania na dunia kote! 

Dhumuni haswa la hii shughuli ilikuwa kuwakutanisha wanawake wote ili kuadhimisha siku ya Wanawake duniani na pia kujifunza mambo mbali mbali toka kwa wanawake ambao wamethubutu kufata ndoto zao na kufanikiwa japo kwa changamoto mbalimbali ambazo zingewafanya wakate tamaa! Pia kulikuwa na mambo mengine ya kujifunza kutoka kwa wanawake wengine katika makundi yao kama VIKOBA! Katika shughuli hiyo kulikuwa na baadhi ya Motivational speakers ambao waliongea  mambo mbali mbali yanayo husu nafasi ya mwanamke katika kuendeleza uchumi wa familia na jamii kwa ujumla. Waongeaji hao alikuwepo Mh. Devota Likolola, Dr. Blandina, Chris Mauki, Mkandarasi bora wa kike-2017 Ms Waziri (Nimesahau jina la kwanza) na wengine wengi!

Alpha (left), pamoja na Mr and Mrs Chris Mauki

Waongeaji wote waliongea vizuri sana na ifuatavyo ni sehemu ndogo ya maongezi ya Dr. Blandina ambapo aliwasihii sana wanawake kuwa na tabia ya kujifanyia tathimini wao wenyewe badala ya kufanya vitu kwa kufata mkumbo wa marafiki / mashoga! Pia aliwataka wawe na tabia ya kujiwekea malengo na strategy plan ya maisha yao kama kweli wanataka kuingia kwenye dunia ya kujenga viwanda kama wanaume! Na zaidi aliwasihii kutokuogopa kutumia neno HAPANA pale panapo bidi kutumia neno hilo! Tafadhali msikilize mwenyewe. ….?

Shughuli hii kwakweli ilikuwa nzuri sana! Binafsi nilijifunza mengi, tulifurahi na kuburudika.  Ngoja nikuonjeshe kidogo ?

Asante sana Emelda Mwamanga na timu yako yote! Salome thank you much! Be blessed!

“Love is peace, not competition.”

“When you were using your own star you can’t afford a bike. When your wife bought you a new car, you and your family said she is spiritually using your star.

WHICH STAR???????? Never take a woman’s kindnesses for wickedness in life. If your wife’s income and financial status is affecting your confidence as a man means your self esteem is dead. Unless she’s very disrespectful and arrogant you don’t have a point. Stop making her life miserable just because she’s richer than you. If you cannot be happy for her means you were never in love with her. Love is peace, not competition. Whoever makes more money shouldn’t be a problem as long as everyone knows and respects each other’s role as a husband and wife.”~~~~~~~~~~~ Akin Al-Ameen®™2017

***Zari’s picture has nothing to do with the story***

“The only difference between a 50yrs old boy and a 25yrs old man is not the age but the brain”

“AGE has nothing to do with BRAIN. Growing UP & Growing OLD are never the same. Growing old is mandatory while growing up is optional by choice. The only difference between a 50yrs old boy and a 25yrs old man is not the age but the brain. Perhaps the reason why GOD put the nose, eyes, ears and mouth in our head is because HE doesn’t want them too far from the brain. Knowledge is different from WISDOM. Education and common SENSE are never the same. It’s a million times better to have common sense without education than to have education without common sense. Education is light while common sense is the switch. Power is nothing without control.Knowledge is common while wisdom is rare. When knowledge brags, happiness smiles. Humility is wisdom’s first child. Wise people don’t show off, only the fools display their foolishness. Avoid too much arguments even when you’re right. When arguments becomes a habbit it turns to disease. You can never be right all the time. Everybody has a right to their personal thinking, reasoning and opinions always respect it.

When people don’t see things the way you see it doesn’t make them a blind. If they don’t reason like you doesn’t make them a fool. The greatest foolishness is to think you know everything. No one will ever be considered wise or intelligent until he/she can wisely and peacefully deal with everybody’s level of understanding. “…….Akin Al-Ameen®™2017

**My nephew’s picture has nothing to do with the story!**

Family Feud: The Akothee Akothee’s family!

Kama mnavyo jua hii blog nilianzisha haswa kwa ajili ya ku-share furaha, mafanikio, changamoto, mahusiano (kati ya wazazi na watoto, wapenzi, marafiki) na njia za kutatua matatizo yetu ndani ya familia na nje ya familia! It’s all about inspirational stories and pictures / videos from our very own families, friends, and so forth! Mengine ni nyongeza tu!……..Basi jana nikiwa natazama Facebook yangu nikakutana na huu ugomvi kutoka kwa mwanamuziki mashuhuli kutoka nchini Kenya ajulikanaye kama #Akothee Akothee, nikasema ngoja ni share nanyi kwani unaweza fikiria kuwa ndugu wa “ajabu ajabu” wapo tu ndani ya familia yenu lakini ukweli watu wa namna hii au vituko vya namna hii vipo katika kila familia yenye UHAI! ………Angalia neno #uhai nimeandika kwa herufi kubwa hiyo ni kuonyesha msisitizo! Yani ninacho maanishi ni kwamba kitu chochote chenye uhai lazima kitakutana na changamoto mbalimbali ili kiendelee kuishi! Changamoto hizo zingine zaweza kuwa nzuri nyingine sinzuri lakini the bottom line kuwa utakutana nazo, and how you solve them hiyo ni juu yako wewe uliye vaa hicho kiatu kwani wewe ndio unajua ni wapi kinakubana!…….Haya enjoy the “drama” 🙂 🙂  

“POLITICS HAVE KILLED ME
one of my very close cousins , who I thought we love each other , came to me & told me that he is stuck with school fee for his daughter & he needs only 50k to enroll his daughter in form one , I gave him the money in a white envelope on a Friday , our first born brother drove him home , & on a Sunday! I recieved a call from home that he just declared that he wants to go for the same seat of mca that my mum is holding , & he used my money to buy people from my village to disgrace my mum , who has been there for the community , I had park afew of my cars in his office as I was looking for an office in Nairobi , when I came to pick the cars, they were already taken as a collateral, as they had not paid rent for months ,remember he wanted me to take over the office but I was too smart , remember he is the same causin I gave the contract to build my mums house, the battle is on , please be carefull of those who kiss you on the forest head & kiss you frequently! I have forgiven you I SAW YOUR SEVERAL CALLS BUT PLEASE! I HAD TO THROW AWAY THE PHONE TOGETHER WITH THE SIM CARD , GOD BLESS YOU IN YOUR FUTURE PLANS
I SHARE BECAUSE I CARE” Anyway, in the end always mshukuru Mungu kwa kila jambo. Kama ni Mkristu utaenda zako kanisani kusali na kutoa sadaka ya kushukuru kama unavyo mwona Akothee hapo na watoto zake akienda nao kanisani ?? Basi na kama wewe ni Muslim utaenda Msikitini kuswali, na kama wewe ni mpagani basi utajijua wewe na mashetani yako ??…….

**Undugu ni gharama ambayo haiepukiki**

“Tusimame pamoja kama Watanzania kupambana na uovu kwenye jamii” -ShyRose Bhanji

CHADEMA HAINA HATI MILIKI YA KUWA UPINZANI PEKEE NCHINI. -Peter Sarungi

 Nilipokuwa natafakari maamuzi ya kwenda kugombea Spika wa bunge niligundua kuwa kama wewe ni mchezaji mzuri wa mpira wa miguu na unajiamini basi si lazima usajiliwe na timu kubwa kama Simba, Yanga ana Azam ili ucheze ligi kuu, kumbe unaweza kucheza ligi kuu hata kupitia Mbao Fc, Ndanda Fc, majimaji au hata Costal Union. Kinachotakiwa ni siku timu yako ikikutana na Simba ama Yanga hakikisha unafunga walau goli moja tu hata kama wao wataifunga timu yako kwa magoli 10. Hilo goli lako wataondoka nalo likiwa na jina lako. Hii ni bora zaidi kuliko kusajiliwa Simba ama Yanga halafu ukakaa benchi kwa sababu wachezaji ni wengi. Nchi yetu ni nchi ya demokrasia na nchi yenye kufunya siasa ya vyama vingi. Kuwepo kwa wingi wa vyama vya siasa ni moja ya tendo la demokrasia tunayo ikubali kila siku. Tanzania kuna vyama vya siasa zaidi ya 25 vyenye usajili wa kudumu vinavyo ruhusiwa kushiriki katika siasa zote za nchi. Ni kwa bahati mbaya Chama tawala hakijawahi kupoteza kushika dola huku vyama vya upinzani viki badilika badilika katika kuwa na wafuasi na nguvu za kisiasa hadi kupewa kijiti cha kuitwa chama kikuu cha upinzani. TLP, NCCR Mageuzi na CUF zimewahi kuwa na nguvu katika chaguzi zilizopita na kuwa chama kikuu cha upinzani wakati huo vyama kama Chadema Tanzania vilikuwa vipo chini sana na vilikuwa havijulikani kwa Watanzania walio wengi. 

Leo Bunge la Tanzania lina vyama 5 vyenye uwakilishi Bungeni huku CHADEMA kupitia muunganiko wa UKAWA wakiwa ni chama kikuu cha upinzani. Ukawa inabebwa na wabunge kutoka CUF, CDM na NCCR huku ACT ikiwa iko peke yake lakini katima kapu la upinzani ikiwa na haki zote kikatiba na hata kwa sheria za uchaguzi na za bunge.

Kumetokea taharuki kidogo juu ya nafasi za wabunge wa Afrika Mashariki hasa kwa upande wa vyama vya upinzani. Mnyukano ulikuwa ni kati ya UKAWA na ACT wazalendo juu ya nafasi 3 za upinzani. Mnyukano huo umeendelea hadi yalipo patikana maamuzi kutoka kwa Speaker juu ya mgawanyo.

Kilicho nisikitisha katika mnyukano huo wa hoja ni baadhi ya makada wa CDM kwa makusudi ama kwa kutojua kuhamisha mjadala wa kibunge na kuuweka kwa wananchi huku wakitoa lawama, matusi, kejeli na hata dharau kwa hoja iliyo tolewa na ACT kupitia mwakilishi wake Mh. Zitto Zuber Kabwe iliyotaka ACT wapate nafasi ya kugombea ubunge wa Afrika Mashariki. 

ZZK ametukanwa sana na baadhi ya makada wa mtandaoni wa CDM huku wakiamini wao ndio wapinzani pekee walio teuliwa na Mungu kuja kuwasemea watanzania. Mimi niwakumbushe tu makada wa CDM kwamba hata wao walikuwa kama mchicha kipindi CUF wakiwa Upinzani imara, Pia wakumbuke hata wao hawana HATI MILIKI ya kuwa UPINZANI pekee nchini. Wasikasirike, kubeza na kupinga wanapoona mbegu zingine za upinzani zinapo chepua kwa kasi, ipo siku mtahitaji ushirika wao ili kufikia malengo yenu.

By the way, inasemekana hata mgogoro wa CUF unawafurahisha sana CDM kuliko CCM, Maana wapo tayari na wamefungua milango kwaajili ya kuwasajili akina Seifu, Mtatiro na wengine pindi chama hicho kikifutwa kama alivyo sema Lissu kwenye mahojiano ya Azam… Daah kufa kufaana.

Msijisahau mkalewa kwa sifa na ubinafsi, ni kweli umoja ni nguvu lakini ni umoja wenye maslahi sawiha ulio Imara na wenye Nguvu.

Wasalam.

SIASA ZENYE MLENGO WA UCHUMI. -Peter Sarungi

SIASA ZENYE MLENGO WA UCHUMI.

Peter Sarungi (The next time)

Kuna Siasa za kuegemea uchumi (Political Economy), Siasa za kisayansi (Political Science) na Siasa za Kisanii (Political Art).

Hizi aina zote zina faida na hasara zake na kila moja ina nafasi yake katika kustawisha jamii.

Nimegundua kuwa serikali ya JPM inafanya siasa zenye kuegemea uchumi. Nasema hayo kutokana na budget ya sasa inayoonesha vipaumbele vya utawala huu ni vile vinavyo chochea uchumi ikiwa ni sector ya usafirishaji na miundo mbinu. Tunaona budget ikitupilia mbali miradi mipya ya afya, elimu, michezo, kilimo, viwanda, maji, umeme, utalii, uvuvi, ajira na kukuza sector binafsi. Budget imeweka mkazo kwenye Ujenzi, Ujenzi,Ujenzi pamoja na ununuzi wa ndege.

Kwa budget hii, fedha nyingi bado zitakwenda kwa wageni ambao watahusika na ukandarasi wa ujenzi wa Reli inayokusudiwa, ujenzi wa fly overs zinazokusudiwa na kampuni ya kutengeneza ndege. Kwa maana hiyo bado pesa haitakuwepo kwenye mzunguko wa ndani wa fedha, matokeo yake ni UKATA, UKATA. 

Aina hii ya siasa ina faida ya kukuza uchumi wa nchi na serikali yake baada ya mda wa miaka 3 na kuendelea. Serikali inakuwa na uchumi mzuri kuliko sector binafsi, Serikali inakuwa imejiingiza katika kushikilia vyanzo vya kuendesha uchumi. Ubaya wa aina hii ya siasa ni wananchi kudhoofika kiuchumi kiasi kwamba wanakuwa tegemezi kwa kila kitu kwa serikali yao. Tatizo lingine ni kwa serikali kuwa na tabia ya  kujiondoa katika kusimamia na kuendeleza miradi yenye kutoa huduma za jamii kwa wananchi wake, hili ni Tatizo kubwa sana mbeleni.

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU-2 -Peter Sarungi

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU 2

Peter Sarungi (The next time)

Sehemu ya II – Ijue Sector ya Madini Tz

Sector ya madili ilianza kutambulika rasmi wakati wa utawala wa awamu ya tatu chini ya Raisi mstaafu Mh. Ben Mkapa kupitia sera ya uwekezaji. Mh. Mkapa aliamini maendeleo ya nchi yatasaidiwa ikiwa tuta ruhusu uwekezaji mbalimbali ikiwemo sector ya madili. Aliamini nchi itafaidika kwa kupata teknolojia mpya, mitaji mikubwa, elimu mpya katika sector hiyo pamoja na kuongeza ajira kwa wananchi na mapato ya serikali. Wawekezaji wakubwa walianza kujitokeza mwaka 2001 Geita na Kahama. Madini yanayopatikana nchi ni mengi kwa aina tofauti kama vile dhahabu, almasi, ruby, Tanzanite, Copper, Silver na mengine mengi ingawa zaidi ya 80% ya machimbo nchini yanajihusisha na uchimbaji wa madini ya Dhahabu. 

UZALISHAJI WA DHAHABU

Mpaka sasa tuna machimbo makubwa ya dhahabu yapatayo sita ambayo ni Bulyanhulu(BGM), Geita(GGM), Buzwagi(BZGM), Biharamulo, North Mara na New Luika. Kwa mwaka migodi hii huzalisha 1.37Million troy ounce ambayo ni zaidi ya kilogram 50,600 ya dhahabu safi kwa mwaka huku GGM ikiongoza kwa uzalishaji wa 38.6% na ya mwisho ikizalisha 1.5%. Kwa viwango hivi, Dhahabu inachangia zaidi ya 90% ya uzalishaji wa madini yote inchini kwa mwaka.

               NJIA ZA UZALISHAJI

Uzalishaji wa dhahabu upo wa aina mbili maarufu ingawa kuna nyingine ya tatu, aina hizi zinatokana na utofauti wa miamba ambayo dhahabu hupatikana. Kuna miamba ambayo ina oxide na zingine zina sulphide.

Dhahabu inayopatikana katika Miamba yenye oxide ina zalishwa kupitia njia za gravity na Cabon process (cabon in loucher CIL na cabon in pulmp CIP). Njia hizi ni common na zipo nyingi katika migodi yetu hadi kwa wachimbaji wa kati. Migodi yenye miamba ya oxide inayotumia njia hii ni nne kati ya zile sita yaani GGM, North Mara, Biharamulo na New Luika. Hivyo uzalishaji katika migodi hii hufanyika na kumalizika ndani ya nchi. Migodi hii haisafirishi mchanga kwenda nje.

Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina zalishwa kupitia njia ya gravity, caborn process na kuhitimishwa na smelter. Njia za gravity na Carbon process huzaliza 40% pekee huku smelter ikizalisha 60% ya dhahabu. Dhahabu inayopatikana katika miamba yenye sulphide ina ugumu wa kunyonywa kupitia njia zilizopo nchini kutokana na dhahabu hiyo kuungana na madini mengine ya copper na silver, hivyo ili kuitoa dhahabu hiyo ni lazima uwe na tanuru kubwa (smelter) lenye uwezo wa kuyetenganisha madini hayo kutokana na utofauti wa melting point za madini hayo. Hivyo ni lazima mchanga unaozalishwa baada ya mchujo kwa njia za kwanza usafirishwe kwenda nje kwaajili ya kuzalisha 60% iliyobaki. Migodi yenye miamba yenye sulphide inayotumia njia hizi zipo 2 kati ya sita nazo ni BGM na BZGM. Migodi hii ndioyo husafirisha mchanga kwenda china na japan ?? kwaajili ya uchenjuaji.

Mpaka hapo kama kuna swali unaweza kuuliza kabla sijakwenda mbele zaidi. Uliza ndani ya maelezo hayo, usitoke nje maana bado kuna makala nyingi zinakuja

Asanteni.

“A vindictive askofu……….askofu Gwijima……” Chege Kilahala

Continue reading “A vindictive askofu……….askofu Gwijima……” Chege Kilahala

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU -Peter Sarungi

KATAZO LA KUSAFIRISHA MCHANGA WA DHAHABU

Peter Sarungi (The next time)

Sehemu ya I – Utangulizi

Mkuu wa Kaya ali ahidi kusimamia sector ya madini kwa umakini ili sector hiyo iweze kuleta tija na faida kwa Taifa. Hivyo serikali ya Mkuu wa kaya imezuia usafirijashi wa mchanga wa dhahabu kwa makampuni ya uchimbaji yaliyopo nchini kwa muda usio julikana.

Lengo la zuio hilo lililotokana na kauli za mkuu wa kaya ni kuhakikisha serikali ina ondoa mianya ya kuibiwa madini hayo ambayo yana chujwa nje ya nchi huku sisi tukipewa mrejesho ambao kwa hisia za mkuu wa kaya anao mrejesho bado una ukakasi. Lakini pia mkuu wa kaya alitamani kabla ya kuwa Mkuu na anaendelea kutamani kujengwa kwa hilo Tanuru kubwa la kuchuja dhahabu, shaba na copper hapa Tanzania ili kufikia ndoto za kuwa na Tanzania ya Viwanda.

Pamoja na dhamira njema ya mkuu wa kaya, ni vizuri na sisi watanzania tukajua kinachoendelea katika sector hii ili tupate kujua faida na hasara za zuio hili ikiwa ni pamoja na changamoto za kufikia shauku la mkuu wa kaya la kuwa na Tanuru hilo lijulikanalo kama Copper Concetrate Smelter  Hivyo nita toa makala ya kueleza hali halisi za sector hii ikiwa ni sehemu ya kwanza na makala nyingine ya kueleza faida, hasara na changamoto ya kufikia ndoto ya mkuu wa kaya ya kuwa na Tanuru la kuchuja madini hayo Tanzania.

Nitatumia vikao mbalimbali nilivyoweza kuudhuria vya wataalum wa madini, ripoti mbalimbali kutoka TMAA na machapisho mbalimbali ya kimataifa kama vyanzo vya habari katika kusapoti andiko langu.

Asanteni

“Republicans and their “pipe dream” of appealing and replacing Obamacare.” – Chege Kilahala

Republicans and their “pipe dream” of appealing and replacing Obamacare…….

If you can’t marshal enough votes in a house (the congress) where you have a comfortable majority. Then your chance of passing it the senate where you have a very thin majority is non-existent…..

Now, we can toast and celebrate that, Obamacare is the law of the land….and it will carry on being so…….I look forward to seeing a universal healthcare system in the USA; one day soon. Just like whats found in Canada and Scandinavian countries….

UKIMWINDA SANA MJUSI ANAGEUKA NYOKA. -Peter Sarungi

UKIMWINDA SANA MJUSI ANAGEUKA NYOKA. 

Peter Sarungi (The next time)

Huu ni msemo wa wahenga ambao uhalisia wake unaonekana mara chache porini lakini hutokea sana kwa maisha ya binadamu. Naamini kuna watu walisha wahi kumwinda mjusi kipindi walipokuwa watoto na katika kumwinda mjusi gafla walipo toa jiwe wakakutana na nyoka, inapofika hapo lazima hali ya hatari itatokea.

Naiona nchi yangu kwa mbali inakaribisha hali ya hatari. Mkuu wa kaya alianza kuongoza nchi yake kwa misingi ya sheria huku akijitambulisha kuwa yeyeni mkali kwa maneno na matendo yake. Baada ya kuwa mkali sana watoto wakaanza kulalamika huku wakionesha kuto ridhika na maamuzi ya baba. Watoto wakaanza kumwinda baba kwa vifungu vya sheria huku wakimtangaza baba kuwa ni dikteta. Na kwa jinsi baba alivyo na msimamo, hakuwahi kurekebisha makosa yake hasa yale yaliyovunja sheria na hata kuonesha upendeleo wa wazi wazi huku akiwagawa watoto wake kwa kauli na matendo.

Kwa sasa hali imekuwa mbaya maana watoto wameanza kumkana baba yao kwa kutumia mama yao Katiba. Wana mshawishi mama yao (Katiba) awaoneshe baba mwingine kwa kutamka kuwa huyu sio baba mzazi na wamtafute baba mwingine.

Kwa hatua ya mawindo yalipo fikia,  nawaona watoto wanahisi wanaye  mwinda ana fanana na Mjusi hivyo wanaongeza jitiada za makusudi wakiamini nguvu za mjisi zipo mkiani na wala sio nguvu za kuogopesha kiasi cha kutaka kumtoa kwenye pango lake.

Lakini nahofia sana hasira za baba, baba akikasirika na kuamua kutumia nguvu zake basi anaweza akawalazimisha watoto kuendelea kuitwa baba kwa kumtishia mama na hata kuwa adhibu vikali watoto wanao kwenda naye kinyume, na akiona bado anapingwa basi anaweza kumbadili mama mwingine na kufunga ndoa ya kudumu. Kwa hatua hii, baba hatakuwa tena mjusi bali atakuwa ni nyoka.

Kwa sasa watoto wajiandae kukutana na nyoka katika mawindo yao, wasidhani wataendelea kukutana na mjusi walie mzoea kumwinda. Wajiandae na plan B,C na hata C ya kukutana na Nyoka.

By the way baba amesha geuza kichwa bado mkia wa nyoka tu aanze mashambulizi kwa watoto wanao winda. 

“Be careful and watch it” Mkuu wa kaya 24/3/2017

“Did Magufuri’s decision to appoint him as the RC base on the qualification he claimed to have?!!!” -Chege Kilahala

If I apply for a job that requires a qualification A and I get offered the job on the basis of my qualification A, then if my employer finds out that, I didn’t possess that qualification, he/she will have the “legal basis” to terminate my employment on that fact……….But if I apply for a job that does not specify that it requires any qualification, but I falsely put down that I possess qualification A, my employer WOULD NOT HAVE any legal basis to terminate my employment on that fact. It is because, his decision to employ me was not influenced by the fact that I have  or have not had that particular qualification.

For that reason, why do people ask for the resignation of Paul Makonda from the RC position? Did Magufuri’s decision to appoint him as the RC base on the qualification he claimed to have?!!! Do you need to even have a standard 7 qualification to be appointed as an RC??!! Leave the guy alone………….!!!

“Sikiliza Zitto Kabwe” Jerry C. Muro

Sikiliza Zitto Kabwe

Mungu amewapa wenzetu “wazungu” baraka ya utajiri wa technology.

Na pia ametupa sisi watanzania baraka ya utajiri wa Udongo wenye thamani.

Ili technology yao ifanye kazi inahitaji malighafi kutoka kwetu.

Sio busara na hekima kuwapelekea malighafi wao mana haiwezi kuhamishwa, ILA TECHNOLOGY INAHAMISHWA.

WAJE WALETE TECHNOLOGY TUTAZUNGUMZA NAO. Jerry C. Muro

Machame, Hai

Kilimanjaro.

26/03/2017

KAMA NAPE KAFANYIWA HAYA, VIPI KWA MTI MKAVU?. -Peter Sarungi

Peter Sarungi (The next time) Injili ya yesu ilipata kumnukuu Nabii Issa (Yesu Kristu) alipokuwa njiani kusulubiwa baada ya kukutana na wamama wakimlilia kwa uchungu,  sehemu ya nukuu inasema ” ikiwa wanafanya haya kwa mti mbichi, je itakuwaje kwa mti mkavu???? 

Kwa kawaida mti mbichi una sifa za kuvumilia shida, ni mgumu kuvunjika lakini vilevile ni mti unao onesha uhai, wenye kuwa na afya ya kustawi na ni mti unao weza kuzaa matunda tofauti na sifa za mti mkavu ambao kwa ujumla unatambulika kama mti ulio kufa.

Namfananisha Mh. Nape Nnauye na mti mbichi ndani ya CCM. Kila mtu anajua mti huu mbichi ulivyo kuwa na uhai, wenye afya na aliyeweza kuitetea chama hadi kupata matunda ya kushika hatamu. Nape amesema alilala porini siku 28 kwaajili ya kuhakikisha chama inapata ushindi, amekipigania chama hadi kufikia kutoa utu wake kwa kukubali lawa, dhiaka na chuki kutokana vita ya kutetea chama kipindi kigumu cha uchaguzi 2015. Inawezekana ile kauli ya Bao la Mkono aliyosema Nape ndio aliyokuwa akitumikia porini kwa siku 28.

Lakini leo, Mti huu hauna tena dhamani mbele ya bashite, mti unatendewa yale wanao tendewa wapinzani wa leo. 

Ikiwa haya yametendwa kwa mti mbichi kama Nape, Je ni nani aliye salama hasa kutoka mti mkavu kama mimi?????

Pole Nape, najua sasa zile akili za kushikiwa na chama utakuwa ume waachia wengine ambao bado wana imani ya kuchukua nafasi yako.

By the way wewe unaye jiita mwana CCM na mkereketwa wa zidumu fikra za mwenyekiti, anza kujiandaa kisaikolojia ili usije pata strock kwa maamuzi kama haya. Chama kwa sasa kina mwenyewe….

Baba yangu Dr. Magufuli mbona unatuangusha hivyo?!!- Alpha Igogo

Baba naomba nianze kwa salamu; shikamoo baba!…….Baba naomba nikwambie dhumuni la barua hii si kukuomba hela za matumizi kwani hilo si tatizo langu kwa sasa! Pesa zipo tena wewe wenyewe ndio umeziweka hivyo nipo vizuri baba!

Alpha Igogo, Blogger

Baba ninachotaka kukwambia leo hii nakuomba utege masikio yako kwa makini sana baba yangu kwani mwanao nimejawa na hofu nyini sana! Wewe ni baba yangu ninaye kupenda sana na siku zote nilitembea bara-barani na kulala usingizi mnono sana nikijua tupo katika mikono salama! Lakini, sasa hivi uwoga umenishika sana, siyo tu kwa watu ambao siwajui bali hata kwa hawa wakuu wa mikoa yetu ulio wachagua. Na mbaya zaidi imani yangu juu yako imeshuka kwa kiasi kikubwa sana kitu ambacho si kizuri kabisa kwani wewe ni baba yangu!

Baba, naomba unisaidie kuelewa, kwani unampango wa kung’ang’ania madarakani? Au unataka nchi yetu iwe kama Rwanda ile ya mauwaji?  Au kama Uganda ya Mseven? Au unatamani Tanzania iwe kama Congo ya Kabila, na Burundi ya Nkurunzinza?! Au iwe nchi ya ukabila kama ile nchi ya Jomo Kenyatta?!! Mimi sijui baba lakini natamani kujua, tafadhali nijuze ili nijuwe kama nianze kuomba ukimbizi nchi za jirani?! Nakama ni hivyo je, zitakua ni nchi zipi katika bara hili la Africa?!!

Baba, niwapi mimi binti yako nikimbilie maana dalili zinaonyesha kama hali itaendelea kuwa hivi na wewe ukaendelea kubariki kwa mikono yako miwili basi mimi mwanao sina budi kuanza kukimbia kuomba hifadhi nchi za jirani hata ng’ambo ya Magharibi kama itaibidi! Japo natafakari sana je nitakimbia mwenyewe au nimchukuwe na mama? Vipi kuhusu bibi na babu? Bila kumsahau mjukuu wako kipenzi! ooh! vipi na yule dada yako wa pekee aliye olewa kijiji cha Koromije mkoani Mwanza? tena yeye ni mlemavu wa miguu! Na binamu yako Zainabu ambaye ni mlemavu wa ngozi huwa awezi tembea juani! Hawa wote nawapenda sana na itakuwa ngumu sana kwangu mimi kuishi mbali nao, nifanyeje baba? Hivi mida ipi itakuwa mizuri kwetu sisi kuanza mwendo; mchana au usiku? Baba, nguvu zinaniishia! Baba kwani niwapi tulikosea? Mbona mambo yanakuwa tofauti na ahadi zako? Mimi niliwashawishi ndugu zetu wote, majirani, marafiki, na Watanzania wote kwa ujumla kuwa wakupigie kura ya “ndio” kwani nina imani nawe, na kwa uchapa kazi wako ulionyesha kuwa wewe unafaa sana! Nao kwa furaha na nderemo wakakupitisha kwa kishindo kuwa Rais wa nchi yao. Nami mwanao nikatembea kifua mbele tena kwa mikogo na madaha mengi sana kuwa sasa Tanzania mpya inakuja! Tanzania ya amani tele, iliyo jaa demokrasia nyingi na uhuru wa kujieleza bila vitisho! Tanzania ya viwanda na miundo mbinu ya kisasa!

Baba, sasa mbona mambo yanakwenda sivyo?! Uliahidi kuleta uongozi bora ulio tukuka, uongozi wa haki na wakufuata sheria. Uliahidi kutulinda sisi wanawake na watoto, ukatuhakikishia kuidumisha amani ndani ya nchi yetu tuipendayo sana! Imekuaje sasa? mbona wavunja sheria ndio unawatukuza na kuwatunuku shahada za uongozi bora?! Baba ni wapi tumekukwaza? Mbona viongozi wanao tishia usalama wa maisha yetu kwa kuvamia sehemu zetu za kazi kwa mitutu ya bunduki ndio unao wapenda sana? Usalama wetu upo wapi? Mbona ndugu zangu hata hawaruhusiwi kuongea kwa uhuru bila kutolewa silaha za moto?!

Baba, nampenda sana kaka yangu ambaye ulimchagua kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam. Nimchapa kazi sana hilo halina upinzani lakini baba yeye si mkamilifu, ana mapungufu yake kama mwanadamu yoyote yule; hivyo kubali kuwa sanyingine naye hukosea. Basi anastahili kuadhibiwa kama unavyo tuadhibu sisi wanao wengine kwa makosa tunayo yafanya au pale tunapo kukwaza!

Baba, sababu ya mimi na Watanzania wengine kuomba umuadhibu huyu kaka yetu, si mbaya hata kidogo! Hatuna nia ya kumkomoa au kumuumiza bali nikutaka kuweka mfano mzuri kwa wadogo zetu ambao wanakutizama iliwajifunze kitu fulani kuhusu utawala bora wa sheria na haki. Maamuzi yako  yatatuaminisha kuwa unamaanisha kile usemacho. Kufanya hivyo kutaondoa hofu tulionayo Watanzania. Au unaogoapa hutopata mchapa kazi kama yeye? mbona kule kanda ya ziwa wapo wachapakazi wengi sana, tena watiifu, na waaminifu, hawana uonevu wala kiburi?!

Baba, naomba nimalizie kwa kusema samahani sana kama tumekukosea. Lakini ukumbuke tu kuwa wewe ni baba wa wengi na si wa mtu mmoja tu, hivyo tunaomba utupende, na utulinde wote bila ubaguzi wa aina yoyote! Usitugawe baba sisi sote ni wana wako. Sisi ni ndugu moja japo wengine ni wembamba na wengine wanene. Japo wengine wafupi na wengine warefu, wengine weusi wa rangi ya ngozi na wengi ni maji ya kunde; sisi ni ndugu moja. Usitubague wala kututenga!

Asante sana baba.