Hongera sana Mr and Mrs Davis Kateti!

Mr and Mrs Kateti
Hongera sana mdogo wangu Davis Kateti na wifi yangu Ester Kateti kwa kula kiapo KITAKATIFU. Mungu awaongoze katika kila jambo jema mlitendalo! Akapate kuwa ngao na kimbilio lenu wakati wote siku zote katika nyakati zote za raha na tabu! Akabariki uzao wenu hata kizazi cha tatu na cha Nne! Nyumba yenu ikawe hekalu ndogo; amani, upendo, furaha vikadumu ndani yenu! Hongereni sana wapendwa!

Bwana harusi na wazazi wake pamoja na mke mwema!
Kwa faida ya wengi, bwana harusi ni mtoto wa mama yangu mdogo. Mama yake (pichani juu ☝) anamfuata mama yangu mara ya 6 katika kuzaliwa. Mama yangu ni mama yake mlezi. Harusi ilifungwa katika kanisa la Wasabato Ukonga, na sherehe ilifanyika ukumbi wa Jeshi la Magereza Ukonga, Dar es salaam siku ya JumaPili, tarehe 07/ 09/2017.
Babu yake bwana harusi na mdogo wake bwana harusi Geoffrey Kateti
Harusi ilishuhudiwa na babu mzaa baba mzee Kateti ambaye alitoka kijijini Utegi na ndugu wengine wengi toka Utegi, Musoma, na Arusha ambapo wazazi wa bwana harusi wanaishi!   mawifi wa bibi harusi katika nyuso za furaha    mama mlezi mama Igogo na babu wa bwana harusi mzee Kateti   Shangazi wa bwana harusi upande wa baba (kati kati) pamoja na maharusi  wanandugu ndugu na jamaa pamoja na marafiki wazazi na maharusi mama wa bwana harusi na mkamwana wake! Mama mkubwa / mama mlezi mama Igogo akiwapiga picha wanawe  mabinamu / dada wa bwana harusi Magreth na mama Ngosha Kwamara nyingi tena, hongereni sana. Mbarikiwe wote! ?❤

Leave a Reply