Maisha……!

Kuna dada alikaa miaka kumi na zaidi akimsubiria mwanaume ambaye alimuahidi kua atamuoa. Dada wa watu akajitunza na kumcha Mungu kwa bidii akimsubiria mchumba wake. Wanaume wengi walimtaka wengine kwa nia njema kabisa ya kutaka kufunga naye pingu za maisha  lakini aliwakataa wote.

Baada ya miaka kama kumi na mbili hivi yule mchumba akarudi Tanzania, akafuata taratibu zote za kimila na kidini na kufunga naye ndoa. Miaka mitatu ndani ya ndoa mwanamke akaanza kuugua alipokwenda kupima damu akifikiria ni marelia sugu akaambiwa ameathirika na HIV! Dada yule hakuamini, akaenda   hospitali kadhaa kupima na vipimo vyote vilisema hivyo!!  Ikabidi amuulize mumewe kulikoni? Baada ya mazungumzo mazito mume akakubali kuwa hakuwa muaminifu na nikweli yeye ndio ameleta ugonjwa huo na amekuwa akitumia dawa takribani mwaka mmoja!!

Dada yule alipatwa na mshtuko mkubwa sana. Hivyo baada ya mwaka mmoja akafariki akaacha mtoto wake wakiume bila mama. Yule baba yeye bado yupo anakula maisha Bongoland kwasababu anatumia dawa!!

Nachosema ni hivi there's a lot of fish in the ocean why going for Jellyfish?? Unamsubiria mtu zaidi ya miaka kumi only to end up with HIV+?? No! kama hawezi kubadili mipango yake kwa ajili yako sasa kwanini wewe unasimamisha na kubadilisha mipango yake kwaajili yake?!! Kuna vitu vya kusubiria lakini siyo mwanaume ambaye hajakuoa! Live your life now!

*** Hii story imetokana na kisa cha kweli kabisa siyo yakutunga. Picha yangu haina huusiano wowote na story***

One thought on “Maisha……!”

Leave a Reply